Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Vikundi vya wapiga muziki Yerusalem

DAR ES SALAAM

Na Philip Komba

Pamoja na mji wa Yerusalemu kujulikana zaidi sana kutokana na umaarufu wake katika mambo ya dini, mji huo haujabaki nyuma katika masuala ya muziki wa kidunia.
Kuna kikundi kimoja kikongwe cha muziki cha hapo mjini Yerusalemu, kiitwacho kwa lugha ya kigeni “The Jerusalem Symphony Orchestra” yaani Kikundi cha Muziki wa Simfoni cha mjini Yerusalemu. Kikundi hicho kimekuwa kikitamba sana katika fani hii ya muziki kuanzia miaka ya 1940.
Kutokana na umaarufu wake, kikundi cha muziki cha Simfoni cha Yerusalemu kimewahi kutembelea nchi mbalimbali za Kimagharibi na Kimashariki na kujizolea sifa nyingi.
Kikundi kingine kikubwa cha muziki kinajulikana kwa jina la “The Israel Philharmonic Orchestra” yaani kikundi cha Kiisraeli cha Wapendao muziki. Makao makuu ya kikundi hicho yamo katika lile jengo la Kituo cha Kimataifa cha Mapatano- “The International Convention Center” ambacho kiko karibu na lango kuu la kuingilia mjini Yerusalemu.
Shughuli zingine zinazowakilisha sanaa mjini Yerusalemu ni nyumba za sinema, kumbi za muziki kama ule ukumbi  mmoja maarufu ulio upande wa kusini mwa mji, na zingine tena mbili, moja ulio eneo la Yemin Mosha, na mwingine eneo la Ein Keren.
Vilevile kuna uwanja mkubwa wa matamasha ya muziki wa nje unaotumiwa pia na wasanii wa kimataifa kwa michezo ya kuigiza  na kwa nyimbo.
Michezo ya aina hii imekuwa ikifanyika kila mwaka tangu mwaka wa 1961 na Yerusalemu imekuwa ikiratibu michezo hiyo. Ukumbi mwingine wa shughuli za ukumbi wa michezo wa mjini Yerusalemu ni ule ulio karibu na Jalbiya.
Ukumbi huu unajulikana kwa kuwa na michezo ya kimataifa, ambayo inafikia zaidi ya michezo 150 kwa mwaka. Kuna kikundi kingine cha aina yake ambacho kinapendwa sana kutokana na utaratibu wake wa kubadilisha wachezaji mara kwa mara.  Makao makuu ya kikundi hicho yako karibu na kituo cha reli cha zamani cha hapo mjini Yerusalemu.
Maeneo mengine ya kuvutia mjini Yerusalemu: Bustani ya wanyama wa kibiblia: Bustani hiyo kimekuwa kivutio cha kwanza kwa watalii wote wanaoitembelea Israeli. Eneo jingine tena ni lile la Nyumba ya Ticho.
Nyumba hii iliyopo sehemu ya kuelekea chini ya mji wa Yerusalemu ina shughuli nyingi za kibiashara. Imepewa hilo jina la Ticho kwa sababu ina michoro na sanamu nyingi za Anna Ticho na za mume wake aliyekuwa mtaalamu wa kuchunguza macho.
Mtaalamu huyu ndiye aliyeanzisha kliniki ya kwanza ya macho katika jumba hilo hapo mwaka 1912. Jumba jingine mashuhuri mjini Yerusalemu ni lile la sanaa la Ah-Hoash lililoanzishwa mwaka 2004. Jumba hilo linatumika kwa kuhifadhia sanaa za Kipalestina.
Mwaka 1974 ilifunguliwa ofisi ya kuchunguza shughuli zote zinazohusiana na uonyeshaji wa sinema. Ofisi hii ilihamishiwa kwenye jengo jipya mwaka 1981 karibu na barabara ya Hebron kwenye bonde la Hinnom karibu na mji wa zamani.
Mji wa Yerusalemu ulitangazwa rasmi kama makao ya kitaifa ya ukumbi wa michezo ‘thieta’ ya Kipalestina inayojihusisha na shughuli za kuvumbua, kuhifadhi, na kuendeleza sanaa za Kipalestina. Makumbusho ya kitaifa ya muziki ya Edward Said ni mlezi wa kikundi cha muziki cha vijana wa Kipalestina.
Kikundi hicho cha vijana kimewahi kuzitembelea nchi za Kiarabu za Ghuba na nchi zingine kadhaa za Mashariki ya Kati hapo mwaka 2009. Jumba la Makumbusho la Kiislamu lililo kwenye Mlima wa Hekalu lilianzishwa mwaka 1923.
 Jumba hili linahifadhi vyombo vingi mbalimbali vya kale, kuanzia vile vidogo kabisa kama viriba vya wanja wa manga na miswada ambayo ni  adimu sana kupatikana siku hizi, hadi pandikizi za nguzo za marumaru.
 Pale Palestina inapokubali na kuidhinisha na hata kuziunga mkono za kifedha, baadhi ya shughuli za kitamaduni za Kiarabu, matukio muhimu ya Kiarabu yalipigwa marufuku kwa sababu yalifadhiliwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Kipalestina.
Mwaka 2009, kulifanyika tamasha la kiutamaduni lililochukua siku nne na kuhudhuriwa na watu zaidi ya 15000 kule Beit ‘Aman pambizoni mwa mji wa Yerusalemu.’
Mfuko wa Fedha wa Abrahamu na Kituo cha Kimataifa cha Yerusalemu vinasaidia kwa kushirikiana kuendeleza miradi ya pamoja ya Kiutamaduni ya Kiyahudi na ya Kipalestina.
Kituo cha Yerusalemu cha Muziki wa Dansi wa mtindo wa Kimagharibi na wa Kimashariki, kinatoa warsha na semina za mawasiliano ya mazungumzo kwa njia ya sanaa.
Kikundi cha Muziki cha Muungano wa vijana wa Kiyahudi na wa Kiarabu kinapiga muziki wa dhati wa Kimashariki na wa Kimagharibi pia.
Mwaka 2006 ilifunguliwa njia ya burudani inayoyafikia maeneo mengi ya kiutamaduni, viwanja vya michezo na bustani za mapumziko ya starehe ndani ya eneo la mji wa Yerusalemu na maeneo mengine yanayouzunguka mji huo.
Mwaka 2008 ilisimikwa Sanamu ya Kuchongwa iliyotayarishwa na Czeslaw Dzwigaj juu ya mlima kati ya eneo la Wayahudi la Armon HaNetziv na lile la Kiarabu la Jebl Mukaber, kama dalili ya kiu inayosababishwa na hali ya kukosekana kwa amani.

Njia ya Mawasiliano:
Yerusalemu ni kituo cha Kitaifa cha kutawanya habari kwa njia ya radio na televisheni. Ofisi kuu ya Mamlaka ya Njia za Mawasiliano ya Israeli yako Yerusalemu pamoja na telivisheni na studio za radio ya Israeli idhaa Na. 2 na ya Na. 10 na sehemu ya studio za radio ya (British Broadcasting Corporation; BBC) taarifa ya habari.
Makao makuu ya magazeti ya “Jerusalem Post” na “The Times of Israel” la “KolHa’lr” na “The JerusalemTimes” na Kituo cha televisheni ya Kikristo kiitwacho “God Tv” yako pia Yerusalemu.
 
Uchumi:
 Kihistoria, uchumi wa mji wa Yerusalemu ulitegemea kabisa safari za hija za mahujaji waliokuwa wanafika kuhiji hapo Yerusalemu kwa  kuwa mji huo uko mbali na bandari za Jaffa na Gaza.
 Mambo yanayoipambanua Yerusalemu na kuwavutia wageni kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni, siku hizi ni yale yanayohusiana na itikadi za dini, na pia mambo ya kiutamaduni wa Kiyahudi.
Wengi wa wageni hao wanafika kuuona ule ukuta wa upande wa magharibi na ule mji mkongwe. Mwaka 2010 Gazeti la “Travel plus Leasure magazine” liliutaja mji wa Yerusalemu kuwa ni mji ulioongoza kwa safari za wakati wa mapumziko katika Mashariki ya Kati na katika Bara la Afrika.
 Mwaka 2013, asilimia 75 ya watalii milioni 3.5 waliitembelea nchi ya Israeli na kuzuru mji wa Yerusalemu.
Tangu Serikali ya Israeli ilipoundwa, serikali ya kitaifa imebaki kama msimamizi mkuu wa uchumi wa mji wa Yerusalemu. Serikali iliyo mjini Yerusalemu, hutoa nafasi nyingi za kazi na hutoa pia ruzuku na marupurupu kwa wafasiria mali na kwa wale wanaoonekana kuinukia katika masuala ya kibiashara.
Ingawa mji wa Tel Aviv unabaki kitovu cha uchumi kwa upande wa fedha, idadi ya makampuni yenye teknolojia ya hali ya juu inazidi kuhamia Yerusalemu leo kila kukicha.
Makampuni hayo yalitoa nafasi za kazi 12000 mwaka 2006.
Maeneo yenye shughuli nyingi za viwanda na utafiti wa kiteknolojia, ni yale yaliyo upande wa kaskazini na upande wa kusini wa mji wa Yerusalemu.
Upande wa kaskazini, kwa mfano, kuna kiwanda cha ‘Har Hotzvian’ pamoja na eneo la utafiti wa masuala ya kiteknolojia na wa maendeleo ya viwanda.
Upande huo wa kusini mwa mji wa Yerusalemu kuna pia viwanda kama vile viwanda vya madawa vya Intel, Cisco, Teva; IBM, Mobileye and Johnson, Medironic na vingine vingi.
Mwezi Aprili, 2015, Gazeti la “Time Magazine” liliuchagua mji wa Yerusalemu, kama moja ya kitovu kinachojitokeza kati ya miji mitano ulimwenguni likiutamka mji huo kwa kusema kuwa mji wa Yerusalemu umekuwa kitovu  kinachojitahidi kuendeleza uuishaji wa vifaa mbalimbali, kama kwa mfano, vifaa vya kufanyia usafi, vifaa vya uchangamshaji na urahisishaji wa ufanyaji kazi wa inteneti n.k.                             
Kukua kwa mji wa Yerusalemu kiuchumi na uendelezaji wa uchumi huo:
Ingawa takwimu zinaonyesha kuwa mji wa Yerusalemu kwa ujumla wake umekuwa ukikua kiuchumi kuanzia mwaka wa 1967, hali ya mji wa Yerusalemu ya mashariki si nzuri sana ikilinganishwa na ile ya magharibi kwa hali ya uchumi wake.
Hata hivyo, familia za jumuiya za Kiarabu zina watu wengi zaidi walioajiriwa ambao wamefikia asilimia 76.1, zikilinganishwa na zile za Kiyahudi ambazo zina asilimia 66.8 tu.
Idadi ya wale wasioajiriwa katika mji wa Yerusalemu, ambao ni asilimia 8.3 ni afadhali kidogo ikilinganishwa na wastani wa wasioajiriwa kitaifa, ambao wanafikia wastani wa asilimia 9.0.
Umaskini unabaki bado ni tatizo katika mji wa Yerusalemu kwa kuwa asilimia 37 ya familia katika mji huo zilikuwa zinaishi chini ya mstari wa umaskini hapo mwaka 2011.
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirikisho la Haki za Kijamii katika nchi ya Israeli, asilimia 78 ya Waarabu katika mji huo wa Yerusalemu walikuwa wakiishi kimaskini hapo mwaka 2012. Kiwango hicho kilikuwa kimeongezeka toka asilimia 64 mwaka 2006.
Shirikisho la Haki za Kijamii linadai kuwa, hali hii imesababishwa na kukosekana kwa ajira, muundo msingi na mfumo wa elimu usiokidhi. Ir Amin, mmoja wa viongozi wa Kiarabu, hata hivyo, anailaumu hali hii, akisema kuwa imesababishwa na ile hadhi ya kisheria waliyopewa Wapalestina katika mji wa Yerusalemu.
Ujenzi wa maghorofa katika mji wa Yerusalemu: Kijadi, mji wa Yerusalemu, umekuwa muda wote na majengo ya urefu wa kawaida tu.
Kulikuwa na majengo 18 tu katika mji wa Yerusalemu yaliyojengwa kwa wakati tofauti, ambayo yalikuwa na urefu wa kwenda juu zaidi ya ule wa kawaida.
Majengo haya yalikuwa yamejengwa kuelekea upande wa seheme ya chini ya mji, wakati ule ambao hakukuwa na sheria zilizokuwa wazi kuhusu ujenzi mijini. Jengo moja kati ya hayo majengo 18 ni lile liitwalo jengo la “Holy Land Tower No.1”.
Jengo hili lenye ghorofa 32, ndilo jengo refu kuliko majengo mengine yote mjini Yerusalemu. Jengo jingine la kufanana na hili ambalo nalo litaitwa “Holyland Tower”, lakini No. 2”  ujenzi wake umekwisha kuidhinishwa na mamlaka husika. Jengo hili nalo litakuwa na urefu uleule wa ghorofa 32.
Mpango Mkuu mpya wa mji wa Yerusalemu una majengo mengi marefu yakiwa pamoja na yale ambayo ni marefu sana yatakayojengwa katika baadhi ya maeneo fulani teule kuelekea sehemu ya chini ya mji wa Yerusalemu.
Kwa kuzingatia mpango huo, kutakuwa na mstari wa majengo kandokando ya barabara ya Jaffa na pia kandokando ya mtaa wa “King George”.
Jengo moja refu kati ya yale yaliyopendekezwa kujengwa kandokando ya barabara ya Jaffa na kandokando ya mtaa wa “King George” litakuwa na ghorofa 65 na litakuwa jengo refu kuliko majengo mengine yote nchini Israeli.
Kwenye lango la kuingilia mjini Yerusalemu, karibu na Daraja la ‘Chords’ na Kituo cha Kati cha Reli, kutajengwa maghorofa mengine yatakayokuwa na urefu wa kati ya ghorofa 24 na ghorofa 33.
Majengo haya yatakuwa sehemu ya eneo litakalokuwa na nafasi wazi kwa shughuli mbalimbali na pia kutakuwa na kituo cha reli ya chini kwa chini.
Kituo hicho cha reli kitaunganishwa kwa madaraja na pia kwa barabara za chini kwa chini. Kituo hicho cha reli nacho kitatoa huduma kwa treni za mwendo kasi kati ya Yerusalemu na mji wa Tel Aviv.
Majengo kumi na moja kati ya hayo maghorofa marefu yatatumika kama ofisi au nyumba za kupangisha na jengo moja litakuwa hoteli kubwa ambayo itakuwa na nafasi za kutosha kwa watu 2000.
Majengo haya yanategemewa kuwavutia wafanya biashara wengi kutoka mji wa Tel Aviv na hivyo kupafanya mahali hapo  kuwa kitovu muhimu cha shughuli za kibiashara.
Zaidi ya shughuli hizo za kibiashara, kutajengwa pia katika eneo hilo hilo kumbi na ofisi za mahakama pamoja na ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali.
Katika eneo hilo kutajengwa pia majengo ya makao mapya ya Hifadhi ya Nyaraka za Kiyahudi na majengo kwa ajili ya Hifadhi ya Nyaraka za Serikali ya Israeli.
Majengo marefu yote yaliyojengwa mjini Yerusalemu yanategemewa kuacha nafasi kwa wananchi ya kuwawezesha kujiburudisha, nafasi kwa ajili ya mikahawa na nafasi kwa ajili ya maduka. Utaratibu huu unaweza kuichangamsha sehemu hii ya mji wa Yerusalemu.
Mwezi wa Agosti mwaka wa 2015, halmashauri ya mji wa Yerusalemu iliidhinisha ujenzi wa jengo refu la futi 344, lenye umbo la kipiramidi.
Mchoro wa jengo hilo ulitayarishwa na Daniel Libeskind kwa kushirikiana na Yigal Levi badala ya mchoro uliokuwa umeandaliwa hapo awali. Jengo hilo lilianza kujengwa mwaka 2019.

Rate this item
(0 votes)
Last modified on Friday, 02 September 2022 09:01
Super User

Selfies labore, leggings cupidatat sunt taxidermy umami fanny pack typewriter hoodie art party voluptate. Listicle meditation paleo, drinking vinegar sint direct trade.

www.themewinter.com

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.