Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Ataka Watoto wapewe malezi bora

Mlezi na Mwalimu katika Seminari ya Mtakatifu Antoni wa Padua – Ntungamo, Jimbo Katoliki la Bukoba, Padri Roland Kashaga (wa pili kulia), akibariki vipaji wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Ekaristi Takatifu kwa watoto 90, iliyoadhimishwa Parokia ya Bikira Maria wa Mateso - Mbezi Msakuzi, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. Kulia ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Fregiel Massawe. (Picha na Yohana Kasosi) Mlezi na Mwalimu katika Seminari ya Mtakatifu Antoni wa Padua – Ntungamo, Jimbo Katoliki la Bukoba, Padri Roland Kashaga (wa pili kulia), akibariki vipaji wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Ekaristi Takatifu kwa watoto 90, iliyoadhimishwa Parokia ya Bikira Maria wa Mateso - Mbezi Msakuzi, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. Kulia ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Fregiel Massawe. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Mlezi na Mwalimu katika Seminari ya Mtakatifu Antoni wa Padua – Ntungamo, Jimbo Katoliki la Bukoba, Padri Roland Kashaga, amewataka wazazi na walezi kuwapatia watoto wao malezi bora na yenye kumpendeza Mungu.
Padri Kashaga alisema hayo katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika, iliyokwenda sanjari na utoaji wa Sakramenti ya Ekaristi Takatifu kwa watoto 90, iliyofanyika Parokia ya Bikira Maria wa Mateso - Mbezi Msakuzi, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.
“Mkiwa mnawalea watoto wenu, mtambue kwamba hamjapoteza chochote, maana msipowapatia misingi bora watoto wenu, baadaye mtakuja kujuta wenyewe kwa sababu hamkuwapatia kile kinachotakiwa kuwapa watoto hao. Mkiwalisha mema na Matakatifu, hasa wawe watu wa kulishika Neno la Mungu, mtakuwa mmefanya vizuri,” alisema Padri Kashaga.
Padri Kashaga aliwasihi watoto waliopokea Sakramenti ya Ekaristi Takatifu, kuiheshimu, huku akiwasisitiza kuithamini, kwani hicho ni chakula cha uzima katika maisha yao.
Aliwapongeza Waamini wa Parokia hiyo ya Bikira Maria wa Mateso – Msakuzi, kwa kuwa na kanisa jipya ambalo tayari limeshatabarukiwa, akiwasihi kulitumia vyema kanisa hilo, ikiwemo kwenda kusali na familia zao.
Aliwasisitiza Waamini hao kuendelea kupendana katika maisha yao, kwani wao ni wamoja, akiwasihi kutokutengana ili waendelee kuijenga Parokia yao.
Kwa upande wake, Paroko wa Parokia hiyo Padri Fregiel Massawe, aliwaasa wazazi na walezi ambao bado hawajafunga ndoa, wafunge, huku akiwataka kufahamu kwamba kuishi kama mume na mke bila kufunga ndoa, ni dhambi.
Padri Massawe aliwashukuru Waamini wote wa Parokia hiyo kwa majitoleo yao wanayoyatoa kwa Kanisa, akiwaomba wasichoke kujitolea ili maendeleo yazidi kuwa juu katika Parokia hiyo.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.