Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Kanisa huingilia siasa kuinua watu

Mlezi na Mshauri wa Christian Professionals of Tanzania (CPT), Padri Vic Missiaen (katikati mwenye fimbo), akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa CPT kwenye mafungo yaliyofanywa na wanachama hao katika Parokia ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili - Mavurunza, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. (Picha na Mathayo Kijazi) Mlezi na Mshauri wa Christian Professionals of Tanzania (CPT), Padri Vic Missiaen (katikati mwenye fimbo), akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa CPT kwenye mafungo yaliyofanywa na wanachama hao katika Parokia ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili - Mavurunza, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. (Picha na Mathayo Kijazi)

DAR ES SALAAM

Na Mathayo Kijazi

Imeelezwa kuwa Kanisa halijiingizi katika siasa, bali lina wajibu wa kushauri inapohitajika, ili siasa hiyo iwasaidie watu katika maisha yao.
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Mlezi na Mshauri wa Wanataaluma Wakristo Tanzania (Christian Professionals of Tanzania: CPT), Padri Vic Missiaen, wakati akizungumza katika Mafungo ya wanachama wa CPT yaliyofanyika Parokia ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili - Mavurunza, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.
“Kwa hiyo sisi kama Kanisa, hatuna kazi ya kuingia katika siasa, bali tu tuna wajibu wa kushauri ili siasa hiyo iweze kufanya kazi ya kuwasaidia watu,” alisema Padri Vic Missiaen.
Padri Missiaen alisema kwamba kujenga Kanisa, kulikuja kwa lengo la kuwasaidia na kuwainua watu katika maisha yao ya kiroho.
“Lengo la kujenga Kanisa Mahalia au Local Church, kulikuja kwa lengo la kusaidia na kuwainua watu katika maisha yao ya kiroho,” alisema Padri Missiaen.
Padri Missiaen alibainisha kuwa licha ya watu wengi wanalipenda Kanisa, lakini ni wachache ndio wenye  msimamo wa kiroho tu katika maisha yao.
Aliwasihi wanachama wa CPT kutambua kwamba wao kama wasomi, ipo haja ya kutumia usomi wao kupeleka mbele mawazo yao ili kusambaza mafundisho ya kiroho kwa jamii.
“Naamini wanaCPT tuna uwezo wa kufanya hivyo, na tuna wajibu. Tukijijengea uwezo imara, tutaweza kusambaza vyema mafundisho hayo,” alisema Padri huyo.
Vile vile, aliwasisitiza kujitafakari na kuamua kusema ukweli mbele za Mungu pale wanapokosea, kwani wengi wao hawako tayari kueleza ukweli.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei Parokia ya Mavurunza, ambaye pia ni mwanachama wa CPT, Casmir Nkumba aliwashukuru wote walioweza kushiriki katika mafungo hayo yaliyofanyika katika Parokia yao, akisema kwamba Parokia hiyo imejifunza mengi juu ya mafunzo yaliyotolewa.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.