Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Waimarishwa watakiwa kuwa Manabii wa kweli

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Parokia ya Mwenyeheri Antonio Rosmini -Mpiji Magohe, Karoli Kadeghe, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Kipaimara. (Picha na Yohana Kasosi) Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Parokia ya Mwenyeheri Antonio Rosmini -Mpiji Magohe, Karoli Kadeghe, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Kipaimara. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Laura Chrispin

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwai’chi amewataka waimarishwa kuwa Manabii wa kweli na kusikiliza sauti ya kichungaji wanapoitwa na Mungu.
Askofu Mkuu Ruwa’ichi alisema hayo wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kipaimara iliyoadhimishwa katika Parokia ya Mwenyeheri Antonio Rosmini - Mpigi Magoe, jimboni humo.
“Muimarishwa unaitwa kuhubiri Habari Njema za Kristu, pamoja na kufanya mambo yaliyo mema na yenye kumpendeza Mungu, na si kuwa nabii wa uwongo,” alisema Askofu Ruwa’ichi.
Aliongeza kuwa zama za sasa zimekuwa na manabii wengi wa uongo, ambao lengo lao ni kudanganya, na si kutangaza Neno la Mungu.
Aidha, Askofu Mkuu Ruwai’chi alisema kuwa Mkatoliki aliyebatizwa, hapaswi kuwaamini manabii wa uongo, bali anatakiwa kuishi katika imani yake.
Aliwakumbusha Waamini kwamba manabii wa uwongo wamekuja kwa kazi ya kutafuta fedha tu, na si kwa ajili ya kuhubiri Neno la Mungu, akiwasisitiza kusimama imara katika imani yao.
“Nabii wa kweli hutokana na kusema ukweli, na siku zote maisha yao si rahisi, kwa sababu ndani yao mara zote kumejaa manyanyaso ya kusakamwa, ya kusutwa, pamoja na kudhulumiwa,” alisema Askofu Mkuu, na kuongeza,
“Hata katika Somo la Kwanza anazungumziwa Nabii Yeremia ambaye ni kati ya manabii mahiri zaidi katika Agano la Kale, ambaye mara zote alikuwa anawaambia watu wamrudie Mungu kutokana na mambo yao waliyokuwa wakitenda.
“Lakini, kwa sababu alikuwa ni nabii aliyesimama katika ukweli zaidi, watu hao walimkamata na kumuhukumu kifo, lakini ni kwa sababu Yeremia aliwataka watu wabadilike kwa kutubu ili yasije kujitokeza tena yale ya Sodoma na Gomora. Hiyo inaonesha fika ni kwa jinsi gani Manabii wa ukweli wanavyoteseka.”
Aidha, Askofu Ruwa’ichi aliwakumbusha Waamini kutubu na kuamini Injili, ikiwa kama ujumbe wa Yesu aliowaachia wanafunzi wake, akiwataka kutokufanya maamuzi ya haraka, bali wafikiri zaidi na kutenda ili baadaye wasije kujuta.
Aliwakumbusha Waimarishwa kuwa siku ya Ubatizo walizaliwa mara ya pili kama hekalu la Roho Mtakatifu, akiwataka watambue na wajiheshimu kwa kuuishi vyema wito wao.
Aliwasisitiza kushuhudia matendo makuu ya Mungu, akiwaasa kuwa kipaumbele ni kuzungumza habari njema kwa watu, na kuwakumbusha kutokuwa manabii waliokufa, wala manabii wasiokuwa na uthubutu.
Hata hivyo, Askofu Mkuu aliwataka wazazi na wasimamizi kuwa mfano bora wa kuigwa na watoto, kwa kuwasaidia kuishi vyema wito wao siku zote za maisha yao.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.