Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Mkurugenzi Mawasiliano Dar awakanya Waandishi Habari

Mkurugenzi wa Mawasiliano Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Joseph Massenge, akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani), kabla ya kuanza kwa Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Wanamawasiliano. (Picha na Mathayo Kijazi) Mkurugenzi wa Mawasiliano Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Joseph Massenge, akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani), kabla ya kuanza kwa Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Wanamawasiliano. (Picha na Mathayo Kijazi)

DAR ES SALAAM

Na Mathayo Kijazi

Waandishi wa Habari wametakiwa kutumia vyema kalamu zao kuandika habari zenye ukweli, na si zenye kuwachafua wengine, kwani wana jukumu la kueneza ujumbe wa matumaini, upendo na amani.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Joseph Massenge, katika homilia yake wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo kwa Wanamawasiliano wa Jimbo hilo, iliyoadhimishwa katika Parokia ya Bikira Maria, Mama wa Fatima, Msimbazi.
“Wanahabari tumieni vyema kalamu zenu kuandika habari zenye ukweli, epukeni kuandika habari zenye kuwachafua wengine. Mnatakiwa kueneza ujumbe wa matumaini, upendo na amani,” alisema Padri Massenge.
Padri Massenge ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tumaini Media, na Paroko wa Parokia ya Bikira Maria wa Rozari Takatifu - Makongo Juu, alitoa wito huo kwa wanahabari kuhakikisha Injili inafika kwa kila kiumbe.
Ageukia utunzaji mazingira:
Aliwasihi kupitia kazi zao wanahabari hao wahamasishe pia kuhusu  utunzaji wa mazingira, kwani kwa kutunza mazingira, watakuwa wamepeleka Injili kwa kila kiumbe.
“Hakikisheni Injili inafika kwa kila kiumbe, siyo kwa kila binadamu tu, ni kwa kila kiumbe. Kupitia kazi zenu hizo, nendeni mkahamasishe pia kuhusu utunzaji wa mazingira…Tunzeni mazingira ili yawatunze, mkifanya hivyo mtakuwa mmetangaza habari njema kwa kila kiumbe,” alisema Padri Massenge.
Aidha, aliwasisitizia wanahabari hao kuepuka kuwa waandishi wenye kuandika habari zenye maslahi ya papo kwa papo, bali wafanye kazi zao wakizingatia maadili ya uandishi wa habari.
Padri Massenge aliwasihi wanamawasiliano hao kuwaombea waandishi wote waliotangulia mbele za haki kutokana na kazi zao, akiwataka kuendelea kusimamia ukweli katika uwajibikaji wao.
Padri Mujuni awafunda Waandishi:
Kwa upande wake, Padri Audiphace Mujuni, Padri wa Jimbo Katoliki la Bunda, anayechukua masomo yake katika fani ya Uandishi wa Habari katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino (SAUT), Tawi la Msimbazi, jijini Dar es Salaam, alisema kwamba vyombo vya habari vina haja ya kuchangia kuleta upendo na mshikamano katika jamii.
Aidha, Padri Mujuni aliongeza kuwa waandishi wa habari ni vyombo vya matumaini katika ulimwengu, hivyo ni wajibu wao kufanya kazi kwa kufuata misingi inayowaongoza.
“Waandishi wa habari, tambueni kwamba ninyi ni vyombo vya matumaini katika ulimwengu. Kwa hiyo, ni wajibu wenu kufanya kazi kwa kufuata misingi na taratibu zinazowaongoza. Mnapaswa kuwa watumishi wa kweli, mkifahamu kwamba kila neno linaweza kuleta athari katika jamii,” alisema Padri Mujuni.
Aliwasisitiza wanamawasiliano kufanya kazi zao, huku wakimtanguliza Mungu, wakitambua kwamba uandishi wao usiwe sababu ya kuikosa mbingu.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.