Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

CHIPATA, Zambia
Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Chipata Gabriel Msipu, ametoa wito wa ugawaji sawa wa chakula cha msaada wakati Serikali ikikabiliana na uhaba wa chakula unaotarajiwa kutokana na ukame, na kusisitiza kwamba hatua zinapaswa kuchukuliwa ili kuzuia vifo vinavyotokana na njaa.
Akiwa katika ziara ya kichungaji katika Parokia ya Mtakatifu Atanazio, Askofu Msipu alisisitiza umuhimu wa ugawaji sawa wa vifurushi vya chakula, akiahidi ushirikiano kati ya Kanisa, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, na Serikali kuhakikisha hakuna anayeachwa na njaa.

VATICAN CITY, Vatican
Baba Mtakatifu Fransisko anatarajiwa kufanya ziara yake ya kichungaji kwenye mji wa Maji katika Kisiwa cha Giudecca, Aprili 28 mwaka huu.
Katika ziara hiyo baba Mtakatifu atakuwa na hotuba tatu na mahubiri wakati wa takriban saa sita katika jiji la maji.
Aidha, atatembelea kituo cha wafungwa cha wanawake na kuwasalimia wasanii wa Biennale.
Aidha, Ataadhimisha Misa katika uwanja wa Mtakatifu Marko kabla ya kuingia kwenye Basilika na kuheshimu masalia ya Mtakatifu mlinzi, Patriaki Moraglia, Shukrani kwa Baba Mtakatifu kwa sababu alitaka kuweka makini Veneto na Kaskazini-Mashariki,kuanzia mji wetu.
Mkutano gerezani na wafungwa na kwa ajili ya uzinduzi wa banda la Vatican lenye kauli mbiu ya  Afya; hatimaye kupita chini ya  daraja na pantoni kwenda katika Uwanja wa Mtakatifu Marko kwa ajili ya  Misa kuu, ikifuatiwa na sala ya kibinafsi kwenye kaburi la Mtakatifu Marko Mwinjili, mtakatifu msimamizi wa  Venezia  na watu wa Venezia.
Hizi ni nyakati tatu zitakazoadhimisha takriban saa sita za ziara ya kitume ya Baba Mtakatifu Fransisko huko Venezia, inayotarajiwa kufanyika inayoongozwa na  kauli mbiu: “Kukaa na umoja katika upendo wa Kristo” na inayohamasishwa na ukurasa wa Kiinjili kuhusu tawi na mzabibu.
Mpango huo rasmi umechapishwa  tarehe 25 Machi 2024 na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican na kuwasilishwa katika Chumba cha Tintoretto cha Kasri na  Patriaki wa  Upatriaki wa Venezia, Kardinali  Francesco Moraglia  ambaye alisema kuwa katika siku ile ni ya mfano ambao unachukuliwa kuwa “siku ya kuzaliwa ya Venezia”, ambayo kwa kawaida inaaminika kuwa ilianzishwa mnamo mwaka 421.
Baba Mtakatifu Fransisko ataondoka saa 12.30 alfajiri kwa helikopta ya Vatican na kutua karibu saa 2.00 kamili  asubuhi katika uwanja wa ndani wa Nyumba ya Gereza la Wanawake huko  Venezia, kwenye Kisiwa cha Giudecca, ambapo atakaribishwa na Patriaki Francesco Moraglia, msimamizi Maria Milano Franco D’Aragona, Mkurugenzi Mariagrazia Felicita Bregoli, na kamanda wa Polisi wa Magereza, Lara Boco.

VATICAN CITY, Vatican

Baada ya Maaskofu, Watawa, familia nzima, vijana, wanafunzi, wanandoa, Wamisionari, wahamiaji, wakimbizi wa kivita, mwaka huu 2024 ni Papa mwenyewe ameamua kutayarisha tafakari ya Njia ya Msalaba ya siku ya Ijumaa Kuu katika njia ya Uwanja wa Colosseum (Magofu ya kizamani ya mateso ya Wakristo wa kwanza.
Hii ni kwa mara ya kwanza katika kiti cha upapa cha Jorge Mario Bergoglio (Papa Fransisko).
Kusali pamoja na Yesu katika njia ya Msalaba ndiyo tema iliyochaguliwa kwa ajili ya tafakari itakayoambatana na vituo kumi na vinne vinavyokumbuka njia ya  Yesu kuelekea Golgotha.
Tena inayotufanya kuelewa tabia ya “kutafakari kwa kina juu ya maandiko hayo ambayo, kama vile Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican  ilivyosisitiza, kwamba  itakuwa “Kitendo cha kutafakari na kiroho, na Yesu katikati.” Yeye atembeaye katika njia ya Msalaba na anajiweka katika safari pamoja nasi. Yote yanalenga sana kile ambacho Yesu anapitia wakati huo na ni wazi kwamba inapanua mada ya mateso ....”
Kwa njia hiyo rejeo la matukio la sasa litakuwa nalo moja kwa moja, kama katika miaka mingine  ya nyuma ambapo wakimbizi, waathirika wa biashara ya binadamu au watu kutoka nchi katika vita walihusika, au, mwaka 2023, na ushuhuda na midahalo iliyochukuliwa kutoka katika nchi walizojeruhiwa  na ambapo Papa alitembelea wakati wa ziara zake za kitume.
Hata kama katika Njia hii ya Msalaba,  miunganisho yake ni mipana zaidi, ikiwa ni maombi ya marejeo yanapanuka... Sala haiendi kwa kundi la watu, bali kwa hali. Kwa hakika, chaguo ni kuunganishwa na Mwaka wa Sala ambao Baba Mtakatifu Fransisko amechagua kuutangaza kuwa maandalizi ya Mwaka wa Jubilei 2025, katika tukio ambalo, kama alivyokuwa amesema, kwanza kabisa lina tabia ya kiroho.
Kuhusu uwepo wa Papa Fransisko kwenye Njia ya Msalaba, kwa kuzingatia hali ya afya ya Papa na kushuka kwa joto jijini  Roma, hakuna uthibitisho au kukanusha kutoka katika Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican: kile ambacho tayari kilitangazwa hapo awali kinabaki, ambacho ni kwamba Papa atakuwa huko Ijumaa usiku  katika Palatine.
“Kwa sasa hakuna mabadiliko ikilinganishwa na yale ambayo tayari yametazamiwa.” Maandishi ya tafakari yatasambazwa siku ya Ijumaa tarehe 29 Machi 2024 na siku hiyo hiyo kutakuwa na maelezo zaidi juu ya nani atabeba Msalaba, kando ya barabara za kale karibu na Colosseum. Hakika watu wanaobeba msalaba wameunganishwa na kutafakari katika kila kituo.”
Mwaka 2013, kwa  Njia ya Msalaba ya kwanza ya upapa wake, Papa Francisko alikabidhi tafakari kwa kundi la vijana wa Lebanon chini ya uongozi wa Kardinali Béchara Boutros Raï; (un gruppo di giovani libanesi sotto la guida del cardinale Béchara Boutros Raï;) mwaka 2014 ilikuwa ni zamu ya Asofu Mkuu  Giancarlo Maria Bregantini,) wa Campobasso-Boiano; (rej. ( monsignor Giancarlo Maria Bregantini); mnamo mwaka 2015, Askofu Mstaafu Renato Corti, wa Jimbo la  Novara;(rej. monsignor Renato Corti,); Mwaka 2016, alikuwa ni Kadinali Gualtiero Bassetti, Askofu mkuu wa Perugia-Città della Pieve, (rej. cardinale Gualtiero Bassetti,) na mwaka uliofuata alichaguliwa kuwa rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI.).
 Mwaka 2017, Papa Fransisko alichagua msomi wa kibiblia wa Ufaransa Anne-Marie Pelletier (rej. Anne-Marie Pelletier,) mwanamke wa kwanza kushinda Tuzo ya Ratzinger, kama mwandishi wa tafakari kumi na nne.

Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam (mwenye kofia ya Kiaskofu), Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Polycarp Askofu na Shahidi, Kilamba, Padri Timothy Nyasulu Maganga, na Padri Frank Mtavangu (wa kwanza kulia), wakiwa katika maandamano ya kutoka kanisani baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika ya Matawi parokiani hapo. (Picha na Mathayo Kijazi)

Mafrateri wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Uzinduzi wa Utunzaji wa Mazingira katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, jimboni humo.

Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Thomas wa Akwino – Kipunguni, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Nestory Damas akibariki Matawi yaliyoshikwa na Waamini wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sikukuu ya Matawi iliyoadhimishwa parokiani hapo.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi (mwenye fimbo ya Kichungaji), Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo (kulia kwa Askofu Mkuu), wakiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wengine, Mapadri, Mashemasi na Mafrateri, baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya kubariki Mafuta kuwa Matakatifu, iliyokwenda sanjari na Uzinduzi wa Utunzaji wa Mazingira katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, jimboni humo. (Picha zote na Yohana Kasosi)

Katika safu hii wiki kadhaa ziliyopita, tulisoma Historia ya Kanisa la Misri na Uinjilishaji wa Misri na Kanisa la Kaskazini mwa Afrika pamoja na kuangazia Uislam ulivyoingia Afrika. Leo tusome jinsi Uislam ulivyoiteka Afrika Kaskazini. Sasa Endelea…

Baada ya dola ya Kirumi Magharibi kuanguka, Wavandali waliokuwa wameiteka Afrika ya Kaskazini, walishindwa na Kaizari wa Mashariki katika dola ya Kostantinopoli. Kaizari alimweka gavana kutawala kwa niaba yake.
Mwaka 647 Gavana Gregori wa Kartago aliwaasi wakubwa zake wa Konstantinopoli. Waislamu walipokuja toka Misri chini ya Ukba Ibn Nafi, alidhania wanakuja kumsaidia dhidi ya Konstantinopoli, hivyo akawaunga mkono wakaingia kwa urahisi.
Baadaye walimgeuka na kuteka Afrika ya Kaskazini. Wakristo Wazungu yaani wenye asili ya Ulaya walikimbilia Ulaya na wakabaki Waberba wenye asili ya Afrika, kutetea Ukristo na nchi yao.
Mwaka 711, Mussa alimtuma Tarik (riq ibn Ziyd) jemadari wa Kiberba aliyeongokea Uislamu na jeshi lao la watu 7,000 kushambulia Uhispania. Walipoanza kupata mafanikio naye alikwenda na jeshi lake, wakateka pamoja Uhispania.
Katika kugawanya nyara hizo, Waarabu na Waberba wakawa marafiki. Guba la Gilbraltar ni ukumbusho wake ‘Gebel al Tarik’. Waberba wengi waliongoka na kuwa Waislamu kwa sababu bila kuwa Mwislamu, wasingepata sehemu ya hizo nyara na marupuuupu mbalimbali.
Mwishoni mwa karne ya 8, Afrika ya Kaskazini yote ilishakuwa ya Kiislamu. Wakati wa Mtakatifu Augustino, Afrika ya Kaskazini palikuwepo na maaskofu 700, lakini walipovamia Waislamu walibakia 35, na katika karne ya 12 walikosa maaskofu watatu wa kumweka wakfu mwenzao; na karne ya 14 hapakuwepo hata askofu mmoja.
Tofauti na Misri, ambapo ingawa lilidhoofishwa, bado Wakristo wapo licha ya unyanyasaji. Kanisa huko Afrika ya Kaskazini, maarufu kwa watakatifu na wanateologia kama Sipriani, Tertuliani na Augustino, lilitoweka kabisa.
Kosa kubwa la kwanza la Kanisa hilo ni kwamba lilijipenda na kujiendeleza kwa ndani, lakini likasahau kuinjilisha. Dini ilibaki tu katika mwambao wa dola ya Kirumi, tofauti na Misri waliotoka nje na kwenda Nubia hadi Uhabeshi.
Vilevile, dini ilibakia katika utamaduni wa kikoloni wa Kilatini hata wakawa Walatini kuzidi Roma. Hata mtakatifu Augustino ambaye mama yake alikuwa Mberba, hakuandika chochote katika lugha yao au kuingiza utamaduni wake katika Ukristo.
Wazawa walijua Ukristo kama waliingia utamaduni wa wakoloni wao. Hivyo wakoloni walipoondoka na lugha ya Kilatini, Dini ikatoweka pamoja nao. Misri waliendeleza lugha yao na kutengeneza ibada ya Kikopti, tofauti na Kigiriki.
Kanisa lisiloinjilisha na kutamadunisha, hufa. Hivyo, ile tabaka ya juu ya Walatini ambao ndio walikuwa Wakristo walipovamiwa na Waislamu, wao walikimbilia Ulaya pamoja na Maaskofu na Mapadre. Hili ni somo kubwa kwetu, Kanisa ili lidumu lazima liingie katika utamaduni na masiha ya kila siku ya watu, la sivyo litabaki kama vazi la Jumapili.
Waislamu katika Nubia (Sudan ya Sasa):
Baada ya kuiteka Misri, mwaka 641, Abdallah Ibn Saad aliishambulia Nubia. Ili kuhimili mashambulio hayo, falme mbili za Kaskazini Nobatia na Makuria ziliungana na kuwa ufalme wa makuria.
Kwa pamoja, zilishinda dhidi ya mashambulizi. Baadaye ufalme wa Makuria ulifanya umoja na ule wa Kusini wa Alodia na kupata nguvu kiasi kwamba mwaka 737 walituma kikosi hadi Aleksandria, Misri kumtoa mahabusu Patriarka aliyekuwa ametekwa na Waislamu.
Miaka kati ya 700 hadi 1250, kilikuwa kipindi cha maendeleo mazuri kwa Nubia. Walijenga makanisa mazuri, na hata mengine yamevumbuliwa na wachimbaji wa mambo ya kale. Alodia peke yake ilikuwa na makanisa zaidi ya 400 na monasteri nyingi. Pamevumbulika na maandishi mengi waliyoyaacha yakielezea ibada zao, na hasa sala.
Mwaka 1172 Misri ilitawaliwa na Waturuki wa Mamluki ambao walikuwa na nguvu na vilevile wakatili sana. Hawa walizonga Nubia, na ili kujihami, Misri iliweka Waislamu Kaskazini mwa Makuria kama ugo dhidi ya mashambulizi.
Bahati mbaya Nubia ilikuwa imekatwa kutoka ulimwengu mwingine wa Wakristo, na baadaye pakawepo mfarakano katika urithi wa wafalme. Hata hivyo waliweza kuwahimili Waislamu hadi mwaka 1504 ufalme ulipotekwa na Waislamu kutoka Misri.
Kwa miaka 1,000 walikuwa na Ukristo imara. Wamisionari waliporudi mwaka 1845 hawakukuta alama zo zote za Ukristo. Ilibidi waanze upya kati ya Waafrika weusi wa Sudan ya Kusini.
Uhabeshi (Ethipia ya sasa) na Uislamu
Uhabeshi ilikuwa na bahati ya kunusurika kutekwa na Waislamu. Sababu za kunusurika kwake kwanza ni kwamba Muhammad alipofukuzwa kutoka Mekka, Waislamu wengine walikimbilia Axum, Mji Mkuu wa Uhabeshi na kupokelewa vizuri.
Kwa sababu hiyo, Muhammad aliagiza katika Korani kwamba Uhabeshi  isishambuliwe, labda kama ni kujikinga.  Mwanzoni agizo hilo liliheshimiwa sana. Pili, nchi ya Uhabeshi iko milimani na si rahisi kuifikia na kuishambulia.
Wote waliozunguka Uhabeshi walitekwa na Waislamu, na yenyewe ikabaki kama kisiwa. Hata hivyo, Waislamu wengine waliingia mipakani na kuishi pembezoni na Waislamu wafanya biashara walioingia ndani walipeleka pamoja nao mawazo ya dini yao.
Mara nyingine ilikuwa vigumu kumpata askofu (Abuna) kutoka Misri, na hivyo kukaa miaka bila askofu au uongozi imara. Ili kujikinga na Waislamu, Wakristo walikimbilia zaidi ndani na milimani.
Kwa kwenda ndani ilisaidia kuinjilisha wazawa wa ndani ya nchi, na kuingiza zaidi utamaduni wao katika maisha ya dini. Ndani ya nchi yalikuwemo makabila ya Wahabeshi (Abyssinia), na mchanganyiko ukazaa utamaduni mpya wa Kihabeshi wenye lugha ya Amharic, ambayo sasa ndiyo lugha rasmi ya taifa, lakini lugha ya ibada iliendelea kuwa ‘Gaez’, lugha ya zamani ya Axum.
Mwaka 1270 Mfalme Yekuno Amlak (1270 - 85) na baadaye Mfalme Amda Seyon (1312 - 1342), walifufua kwa nguvu ukoo wa ufalme wa Suleman ambao ulikuwa umepoteza madaraka kwa Wazagwe tangu mwaka 1137.
Mfalme Zara Yokob (1411-1468), alifikisha katika kilele ustawi wa ufalme wa Uhabeshi. Akitaka kuimarisha nguvu zake dhidi ya Waislamu Wasomalia waliosaidiwa na Waturuki, alituma ujumbe Roma kwa Papa kuomba msaada.
Kama Konstantino kwa Warumi, naye alilazimisha ustaarabu wa Kikristo kwa Wahabeshi wote hata kwa wapagani, yakiwemo maadili ya Kikristo kama ndoa ya mke mmoja. Mkuu wa Kanisa la Uhabeshi alikuwa ni ‘Abuna’ aliyetumwa kutoka Misri kama kiungo cha umoja na Kanisa mama.
Chini yake alikuwepo ‘Echege’ aliyemsaidia Abuna katika mambo ya utamaduni na desturi mahalia. Hata hivyo, kiongozi halisi wa Kanisa hilo alikuwa ni ‘Negus Negasti,’ ikimaanisha ‘Mfalme wa Wafalme’. Hii iliendelea  mpaka wakati wa Negus Haile Sellasie katika karne ya 20.
Malkia Helena akishikilia kama mlezi kwa ajili ya mtoto wake mdogo Negus Lebna Dengel, upinzani wa dola za Kiislamu za Kisomali uliongezeka kwa vita vikali, naye aliomba msaada kwa Wareno.  Mjumbe Mreno alipofika kukagua alikuta mfalme Lebna Dengel (1508-40) amekimbilia milimani, na nchi yake imeharibiwa na Wasomali wa Haral chini ya Ahmedi Ihn Ibrahim, wakisaidiwa na bunduki za Waturuki.
Mwaka 1543 Wareno walituma askari 400 wenye bunduki wakawashinda Wasomali, Ahmedi akauawa vitani. Hii ilinusuru ufalme wa Ethiopia na kufungua uhusiano na nchi za nje. Hapo kinaishia kipindi cha kwanza ambapo Ethiopia ilikuwa imefungwa bila uhusiano na nchi za nje za Kikristu.

Waamini wa Parokia ya Mtakatifu Polycarp Askofu na Shahidi – Kilamba, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiimba wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika ya Matawi iliyoadhimishwa parokiani hapo. (Picha na Mathayo Kijazi)

Waamini wa Parokia ya Mtakatifu Thomas wa Akwino – Kipunguni, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa kanisani wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sikukuu ya Matawi iliyoadhimishwa parokiani hapo.