Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

DAR ES SALAAM

Bondia wa Masumbwi nchini, Hassan Mwakinyo amesema kuwa ujio wa pambano lake la ‘Usiku wa Utetezi wa Mkanda” ni sehemu ya kudhihirisha utemi wake kwenye mchezo huo.
Mwakinyo anautetea mkanda wake wa WBO Afrika aliouweka kama rehani ili kurudisha hadhi yake kwenye viwango vya ubora vya mchezo huo.
Pambano hilo litakalo fanyika Tarehe 16 Novemba 2024 katika ukumbi wa Werehouse Masaki Jijini Dar es Salaam, na litakuwa pambano ambalo litatoa taswira ya ubora wa bondia huyo kutoka hivi karibuni kuingia katika mvutano mkubwa na baadhi ya mabondia wenzake.
Hassan Mwakinyo amewaomba wadau na wapenzi wa mchezo wa ngumi kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuona ukubwa wake kwenye masuala ya ngumi.
“Maisha yangu siku zote mimi ni mapigano kutokana na dunia ninayoishi, hivyo hata mpinzani wangu atambua hilo kuwa sitamuacha salama kutokana  na maandalizi niliyoyafanya”, alisema Mwakinyo.

DAR ES SALAAM

Klabu ya soka ya Tabora United imesema kwamba timu yoyote inayotaka huduma ya mchezaji wao Offen Chikola, inapaswa kutoa kitita cha shilingi bilioni moja ili imsajili.
Chikola kwa sasa anaimbwa na wapenzi wa soka nchini kwa mabao yake mawili aliyofunga hivi karibuni kwenya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga katika uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es salaam.
Akizungumza na gazeti Tumaini Letu kwenye mahojiano maalum hivi karibuni, Afisa Habari wa Tabora United ambaye pia anakaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu, Christina Mwagala, alisema Chikola ana thamani kubwa kuliko watu wanavyodhani, na kwamba hiyo haitokani na kuifunga Yanga, isipokuwa thamani yake ni ya muda mrefu.
Alisema kwamba kwa kuwa mchezaji huyo bado ana mkataba wa muda mrefu na Tabora United, timu inayomtaka inabidi ijipange vilivyo kuvunja kibubu ili kumsajili.
“Sisi kila mchezaji wetu ana thamani kubwa.Huyu Chikola ni Mtanzania mwenzetu kutoka Morogoro tu pale. Wapo wale wa kimataifa, nao ukitaka kuwasajili bei yao imechangamka.Na thamani yao inaendana na wanachokifanya uwanjani.Sote tunaona Tabora United jinsi inavyocheza,”alisema Christina.
Alisema kuwa wachezaji wote wa Tabora wana ubora mkubwa, na kwamba hicho ndicho wanachojivunia kwa sasa huku wakiwa na matumaini ya kufanya vizuri katika msimu huu.
“Sisi malengo yetu ni kuwa mabingwa, na si vinginevyo.Tunaziheshimu sana timu za Simba na Yanga, lakini safari hii tunataka zitupishe kidogo ili na sisi tutambe na taji la ubingwa,”alisema.
Chikola ambaye ni kiungo mshambuliaji wa Tabora United, hadi sasa amefunga mabao matatu katika Ligi Kuu, huku akionyesha nia ya kutaka kuendelea kufunga mabao mengine.
Mabao hayo yote matatu amefunga kwa kutumia mguu wake wa kushoto, sawa na Nassoro Saadun wa Azam FC, na Joshua Ibrahim wa Ken Gold.

NEW DELHI, India
India imeliarifu Baraza la Kimataifa la Kriketi kwamba haitasafiri kwenda kwenye Kombe la Mabingwa, kulingana na wenyeji Pakistan.
Mvutano wa kisiasa unaoendelea, unamaanisha kuwa nchi hizo mbili hazijacheza nje ya mashindano makubwa ya wanaume tangu mwaka 2013, wakati India haijacheza nchini Pakistan kwa miaka 16.
Pakistan inatazamiwa kuandaa hafla ya kimataifa kwa mara ya kwanza tangu 1996 mwezi Februari, na Machi mwaka ujao, timu nane, zaidi ya 50 ya Mabingwa.
Lakini, Bodi ya Kriketi ya Pakistani (PCB) ilisema Bodi ya Udhibiti wa Kriketi nchini India imeiambia ICC timu ya India haitavuka mpaka.
“TAKUKURU imepokea barua pepe kutoka kwa ICC, ikisema kwamba BCCI imewafahamisha kwamba timu yao haitasafiri hadi Pakistan kwa ajili ya Kombe la Mabingwa wa ICC 2025”, alisema msemaji wa PCB.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza baada ya siku mia moja, tarehe 19 Februari. Ratiba bado inapaswa kuthibitishwa na ICC.
ICC haijajibu moja kwa moja taarifa ya PCB, lakini iko kwenye majadiliano na Pakistan na mataifa mengine saba yanayoshindana juu ya ratiba. BCCI imeombwa majibu.

LONDON, Uingereza
Mwamuzi wa Premier League, David Coote (kushoto) amesimamishwa baada ya video inayodaiwa kumuonyesha akitoa kauli za dharau kuhusu Liverpool na meneja wa zamani wa klabu hiyo Jurgen Klopp, kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Bodi ya Waamuzi PGMOL inasema kusimamishwa kutaanza kutumika mara moja na inasubiri uchunguzi kamili.
Video hiyo, iliyosambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii, haijathibitishwa na haijulikani ni lini ilirekodiwa au uhalisi wake.
Coote, 42, alichezesha ushindi wa 2-0 wa Liverpool dhidi ya Aston Villa Jumamosi na ni mmoja wa maafisa wa Premier League walio na uzoefu mkubwa, na amekuwa waamuzi katika ligi kuu tangu 2018.
Video inayoshirikiwa inaonekana kurejelea mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza ambayo Coote alisimamia mechi kati ya Liverpool na Burnley mnamo Julai 2020, ambayo iliisha 1-1.
Klopp alimkosoa Coote baada ya mechi, akisema mwamuzi alishindwa kutoa faulo kwa changamoto zilizowakabili wachezaji wa Liverpool.

Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Salamu Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.

Maria Mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.

Ndimi mtumishi wa Bwana, Nitendewe ulivyonena.

Salamu Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.

Maria Mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.

Neno wa Mungu akatwaa mwili, Akakaa kwetu.

Salamu Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.

Maria Mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu.

Amina.
Utuombee mzazi Mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo.

Tuombe:
Tunakuomba Ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika, kwamba Kristo mwanao amejifanya mtu;

kwa mateso na msalaba wake, utufikishe kwenye Utukufu wa ufufuko.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

Atukuzwe baba na mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina x3

Raha ya Milele, uwape Ee Bwana na Mwanga wa Milele uwaangazie, Wapumzike kwa amani. Amina x3

Mt. Yosefu, mfano wa watu wote wanaofanya kazi, unijalie neema ili nifanye kazi kwa bidii, nikifanya wito wa kazi zaidi kuliko kawaida;

nifanye kazi kwa moyo wa shukrani na furaha, nikiona heshima ya kufanya kazi na kuleta maendeleo kwa njia ya fadhili zitokazo kwa Mungu,

bila kujali matatizo na uchovu, nifanye kazi zaidi kwa nia njema, na kuepuka ubinafsi wakati huo daima nikiona kifo mbele yangu,

na hesabu ambayo nitapaswa kutoa kutokana na muda ninaopoteza, mema ninayoshindwa kutenda, mawazo batili ya mafanikio,

ambayo ni hatari kwa kazi ya Mungu. Yote kwa ajili ya Yesu, yote kwa ajili ya Maria, yote kutokana na mfano wako, Ee Baba Mt. Yosefu.

Hili litakuwa neno langu la kuzingatia katika Maisha na hata kifoni. Amina.

Ee, Mtakatifu Yosefu ulikuwa mtiifu kabisa kwa maongozi ya Roho Mtakatifu.

Unijalie neema ya kujua hali yangu ya maisha ambayo Mungu katika ukarimu wake amenichagulia.

Kwa furaha yangu hapa duniani, na Pengine hata kuhusu hatima yangu huko Mbinguni, itategemea uchaguzi huu,

nisiwe mwenye kudanganyika kwa kufanya hvyo. Nipatie mwanga wa kujua mapenzi ya Mungu,

na kuyatekeleza kwa uaminifu, na kuchagua wito ambao utaniongoza kwenye heri ya milele.

Sala Zetu...

Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, akiwa katika picha ya pamoja na Mapadri na Viongozi wa Kamati Tendaji ya Parokia ya Mtakatifu Vincent wa Paulo, Kibamba, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Rais wa Klabu ya soka ya Yanga, Injinia Hersi Said huenda akaanza kulipwa mamilioni yatokanayo na posho ya mwaka kupitia nafasi yake ya Uenyekiti wa Chama cha Vilabu Afrika.
Shirikisho la soka Afrika CAF linapendekeza posho ya kila mwaka ya dola 50,000 za Kimarekani kwa Mwenyekiti wa Chama kipya cha Vilabu vya Afrika, ikiwa ni ajenda ya Mkutano Mkuu wa 46 wa Kawaida wa CAF utakaofanyika nchini Ethiopia Oktoba 22 mwaka huu.
Kiasi hicho atakachopata Hersi kwa mwaka kwa pesa za Kitanzania ni shilingi milioni mia moja thelathini na sita na laki tano (136,500,000).
Uwezekano wa kupata kiasi hicho cha posho ni pale wajumbe wa Mkutano huo watakaporidhia kwa pamoja pendekezo la ajenda hiyo.
Ikumbukwe kuwa Desemba mosi mwaka jana, Hersi alishinda nafasi hiyo ya kuongoza Chama cha Vilabu Afrika.
Siku chache baadaye ndani ya mwezi huo huo, CAF ilimteua Hersi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi za Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) na Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN).
Hersi aliteuliwa kuingia katika Kamati hiyo kwa vile ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, nafasi aliyoipata baada ya kuukwaa uongozi wa Chama cha Vilabu Afrika.
Hersi aliingia madarakani Yanga akirithi mikoba ya Dk. Mshindo Msolla, ambapo katika uongozi wake amefanikiwa kuibadilisha timu hiyo kucheza soka la kisasa, huku ikifanikiwa kusajili wachezaji wenye viwango vya juu Afrika.
Timu hiyo msimu huu imefanikiwa kupenya na kuingia katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika sawa na msimu uliopita, ambapo ilifanikiwa kufika katika hatua ya makundi na kuishia robo fainali, na baadaye kutolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Mwaka juzi Yanga ilicheza fainali za Kombe la Shirikisho barani Afrika na kufungwa na USM Algier katika mchezo wa fainali.
Septemba 16 mwaka huu, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) (EXCO) ilitangaza kuwa Mkutano Mkuu wa 46 wa Kawaida wa CAF utafanyika Addis Ababa, Ethiopia mwezi Oktoba.
Awali, mji wa Kinshasa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ulichaguliwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa 46 wa Kawaida, lakini kutokana na sababu ambazo hazijawekwa wazi, DRC ilisema haiwezi kuandaa hafla hiyo.