Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Mlezi wa Seminari Kuu ya Segerea, Padri Siegfried Rusimbya Ntare, akibariki matoleo ya waamini wakati wa adhimisho la Misa Takatifu ya Alhamisi Kuu iliyoadhimishwa katika Parokia ya Mtakatifu Kizito, Kilongawima, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. Kushoto ni Dekano wa Dekania ya Mtakatifu Thomas More, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Romwald Mukandala.

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Halmashauri ya Walei wa Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Daima, Kimara- Korogwe, jimboni humo baada ya Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika parokiani hapo.

Paroko wa Parokia ya Familia Takatifu, Mburahati, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Vitalis Kassembo (katikati mwenye kanzu nyeusi), akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Halmashauri ya Walei wa Parokia hiyo, baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Sikukuu ya Pasaka iliyoadhimishwa Jumapili ya Pasaka parokiani hapo. (Picha zote na Yohana Kasosi)

Mwenyekiti wa UWAKA Dekania ya Segerea, Emmanuel Tibaijuka akitoa neno la shukrani kwa UWAKA Parokia ya Mtakatifu Bonaventura, Kinyerezi, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, kwa kumkaribisha katika sherehe ya UWAKA DAY parokiani hapo.

Mlezi wa Seminari Kuu ya Segerea, Padri Siegfried Rusimbya Ntare, akiwaosha miguu waamini wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Alhamisi Kuu iliyoadhimishwa katika Parokia ya Mtakatifu Kizito, Kilongawima, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.

Waamini wa Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Daima, Kimara- Korogwe, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wakiwa katika Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika parokiani hapo hivi karibuni.

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba (katikati mwenye fimbo ya kichungaji) pamoja na Mapadri wakiwa katika picha ya pamoja na waamini kutoka Parokia mbalimbali za Jimbo hilo, baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Sherehe ya Utume wa Kwaya Katoliki Tanzania (UKWAKATA), Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, iliyoadhimishwa Parokia ya Mtakatifu Bonaventura, Kinyerezi.

Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Bonaventura, Kinyerezi, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Francis Hiza (katikati waliokaa), Paroko Msaidizi wa Parokia hiyo, Padri Benson Mapunda (kushoto kwa Paroko), na Didas Ndyemela, Mwenyekiti wa UWAKA Parokia hiyo (kulia kwa Paroko), wakiwa katika picha ya pamoja na Wanaume Wakatoliki (UWAKA) Parokia ya Kinyerezi baada ya hafla fupi ya UWAKA DAY, iliyofanyika Jumatatu ya Pasaka parokiani hapo. (Picha zote na Yohana Kasosi)

Mwanza

Na Paul Mabuga

Anna Nicodemus, mmoja wa wahariri katika kituo cha runinga cha Shirika la Utangazaji la Namibia (Namibia Broadcasting Corporation: NBC), yeye na timu yake wamepanga kufanya filamu halisi (factual film) kama sehemu ya mafunzo ya chuo kimoja katika jiji la Berlin nchini Ujerumani, na wameamua kuifanya kazi hii katika nchi yao.
Kwa hiyo, wanapanga kutengeneza maudhui ambayo yataonesha tofauti kati ya maisha ya kijijini na ya mjini, wakirejea hali ilivyo katika mji mkuu wa nchi yao- Windhoek. Lakini katika mazungumzo nao kama wanafunzi wenzao, inabainika kuwa walichodhamiria sicho walichokikuta huko walikokwenda kutengeneza filamu hiyo.
Walianza na kumchukua Mhandisi wa Mwanga katika kituo hicho, aliyetambulishwa kwa jina la Zuma ambaye anatoka katika kabila la Wa -Himba (omu himba akiwa mmoja na wakiwa wengi ni Ova himba), ambalo linatoka Kaskazini mwa nchi hiyo.Wa-himba kwa kiasi ni wafugaji, na wanasifika kwa kujipaka tope jekundu na kwa idadi wanakadiriwa kufikia watu elfu 25.
Katika filamu hiyo, Zuma ambaye ameacha mchumba wake katika jiji la Windhoek, anasafiri hadi katika kijiji chao kwa lengo la kusalimia mwishoni mwa juma. Anapofika huko, kitu cha kwanza ni kuelekezwa avue mavazi ya mjini, na kisha kuvaa lubega baada ya kujiisiliba udongo mwekundu uliochanganywa na mafuta ya ng’ombe.   Hapa ndipo anapofanana na watu wa jamii yake.
Pengine tofauti na mazoea, safari hii mjomba wake anatangaza katika kadamnasi kwamba ameamua kijana wake Zuma aoe, na mwanamke yupo amemchagulia, ni mama wa ki-hinba ambaye kwa umri ni mkubwa kuliko muoaji. Kwa Wahimba  mjomba ndiye mwenye mamlaka kwa kijana, na hata kwa kumtafutia mchumba. Jukumu hili hufanyika kwa umakini kwa sababu kwao mwanamke ndiye mkuu wa familia.
Mke ambaye ana watoto wanne aliozaa na wanaume wengine, sasa amepata kijana wa jijini Windhoek, na kwa taratibu Zuma hawezi hata kuleta fyoko na yule mchumba wake aliyemuacha mjini ambaye hatambuliki, kwani hana mamlaka ya kujichagulia, na lazima idhini itoke kwa mjomba.
Mke anatinga kwenye ndoa akiwa kifua wazi. Wanawake wa Kihimba ndivyo walivyo kijiji kizima, siku zote hawafichi matiti. Hakuna cha hereni za English Gold wala jeans, unafanya mchezo nini! Wametinga viurembo vya kujitengenezea wenyewe, na vijimavazi kuziba kiuno. Wamejisiliba udongo mwekundu na kujipaka mafuta ya ng’ombe. Kutoka hapo anapatikana Bi. harusi, mengine kama shela na saloon, ishia nayo huko huko.
Filamu hii ilipewa jina la Maisha Pacha ya Zuma (Double Lives of Zuma!), yaana Zuma wa jijini Windhoek anayeoongea Kireno na Kiingereza, na mwingine  wa kijijini Kaokoland, anayeongea Kiherelo na Kiafricana.
Kimoja cha kuchukua ni kwamba, familia inaonesha mamlaka na wajibu katika suala la ndoa, na kimsingi huu ndio uliokuwa utaratibu mzuri katika jamii zetu. Mathalan, mjomba anamwendea kijana wake na kumwambia kule kanisani ameona msichana mrembo ambaye anamfaa kuwa mke wake. Labda hana mkorogo, na nywele kazisuka vyema, siyo kama zile zilizosambaa mithili ya brashi bovu la shetani.
Pengine shangazi anamfuata binti yake na kumwambia kule kanisani amemuona kijana anayefaa kuwa mume wake, kwani kavaa vyema na hajaacha chupi nje, hajasuka wala kuvaa hereni hivyo hata wakioana na kukaa kwenye nyumba yao, atajulikana nani ni mwanamke na nani ni mwanaume. Yaani kijana mchumba  mtarajiwa hajajitindua bongo na kuweka boga  kichwani badala yake! Anajisimamia na hana mwelekeo wa kulelewa.
Siku hizi vijana wameachiwa demokrasia, wanaamua watakavyo! Waoe au kuolewa  sawa, na wasiolewa au kutooa nayo ni burudani tu kwao. Hili la mwisho ndilo limekuwa fasheni, na ushahidi ni takwimu kwamba asilimia 61 ya Watanzania  walio mijini na asilimia 55 ya walio vijijini, hawajoa wala kuolewa.  Hizi ni takwimu rasmi ambazo zimekuwa gumzo mitandaoni, huku Viongozi wa Dini wakiombwa kuingilia kati.
Takwimu hizi naana yake  ni kwamba karibu watu wawili katika kila watatu, ambao bila shaka wanapaswa kuwa kwenye ndoa unaokutana nao mjini, hawajaoa au hawajaolewa, huku katika  kila watu wawili  unaowaona kule kijijini, basi  ujue mmoja kati yao  hajaoa au hajaolewa. Hali hii pengine inakuja baada ya vijana kuanza kuona kwamba hakuna umuhimu wa kuoa  ama kuolewa, na kwao hiyo ni fasheni.
Pengine ni kweli kwamba kuoa au kuolewa na uamuzi unaohitaji umakini, kama mwanafalsafa mmoja anayenukuliwa mara kadhaa bila kutajwa, alivyowahi kusema kuwa, kati ya kuoa na kutooa, au kuolewa ama kutoolewa, lolote kati haya utakalochagua, utajuta! Lakini ni ukweli usiopingika kwamba  kuoa  ama kuolewa, ni wito wa lazima, labda kuwe na sababu inayokubalika.
 Mjadala wa takwimu hizi la lundo la Watanzania wasio katika ndoa, unapohamia katika daladala moja jijini Mwanza inayosafirisha abiria kutoka jijini kati kwenda Buswelu ambako unamkuta msafiri ambaye ni mwenyeji jamii moja kutoka kaskazini mwa Tanzania, na  anasema, “Tatizo ni wasichana hawapendi kuzaa, wanapenda kudondosha (kutoa mimba), lakini vijana wa kiume wakilazimishwa, wataoa, wao hawana shida.”
Yeye analiona tatizo ni kwa mabinti kutotaka kuolewa wakikwepa majukumu yao ya asili ya kuwa wake, kuzaa na kulea. Wakati huyu muungwana akisema hivi, Mwenyekiti wa mtaa mmoja jijini humo, anakuja na shauri la ajabu kidogo. Linahusu mama mmoja mwenye umri wa kati ya miaka 40 na 50 ambaye anadai kwamba kuna kijana  mpenzi wake amempa ujauzito na kumwibia pesa. Aliingia katika mahusiano na kijana huyo baada ya kufiwa na mumewe.
Unaposikia juu ya shauri hili, unamwangalia kijana mhusika na kugundua kuwa ana umri wa miaka kati 20 hadi 25. Lakini kabla mambo hayajaenda mbali, Mama mlalamikaji na mlalamikiwa, ambaye ni kama mwanae, wanaonekana wakiwa pamoja, wakipata kinywaji, na labda kulea mimba yao. Mwenyekiti ashauriwe, kwamba, hawawezi vijana wa kileo kwani wamenogewa kulelewa na kuwa “ndugu wakigombana, kamata jembe ukalime!”

Dar es Salaam

Na Arone Mpanduka

Kuimba ni kutamka maneno katika hali ya kimuziki, au pia twaweza kusema ni kutamka maneno moja baada ya jingine kwa sauti yenye lahani (sauti ya ala ya muziki,tyuni) au ghani (melodi).
Mwimbaji ni mtu yeyote mwenye uwezo wa kuimba kwa sauti yake  bila kutumia vyombo vya muziki.
Ikumbukwe pia kuwa katika vikundi vya uimbaji, wapo wale wanaoongoza wengine katika uimbaji (lead singers), na wengine kazi yao ni kuitikia (backing singers).
Kuna mitindo mbalimbali ya uimbaji. Wengine wanaimba huku wamesimama wima, wengine wanaimba huku wamekaa, na wengine wanaimba huku wakionesha ishara mbalimbali kwa mikono, miguu yao,au vyote viwili.
Mitindo ya uimbaji ni mizuri iwapo tu inasaidia kufikisha ujumbe kwa wahusika. Huduma ya uimbaji siyo “show.”

JINSI YA KUPATA WIMBO/MADA MPYA
Watu wengi wanapenda vitu vipya,mathalan kiatu kipya, gauni jipya, nyumba mpya,vyombo vipya, n.k. Vivyo hivyo, watu wanapenda kusikia nyimbo mpya. Lakini je, ni rahisi kwaya au watunzi wa nyimbo kutunga nyimbo mpya kila mara?
Mambo yafuatayo yanaweza kukusaidia kupata nyimbo au mada mpya.Ukisikia sauti ya wimbo (melody) moyoni mwako, fanya haraka kuirekodi kwenye kanda (kama una radio cassette na microphone au simu).ili usisahau.
Njia nyingine ni kusoma sana vitabu mbalimbali vya kisiasa, kiuchumi na historia za ndani na nje ya nchi, ili vikupe uelewa mpana wa kuimba maudhui unayoyataka.
Pia, unaweza kuwa mdadisi wa mambo kwa kuuliza wajuzi mbalimbali, na kufuatilia vyombo vya habari kuhusiana na yale yanayoendelea kujitokeza kila siku.
Wimbo unaweza kuwa na mada (topic) moja au zaidi. Lakini wimbo wenye mada moja ni mzuri zaidi. Kwa nini?
Wimbo wenye mada moja mara nyingi unaanza kwa utangulizi,baadaye unaelezea mada yenyewe, na kisha unatoa hitimisho.Kwa hiyo ni rahisi kukumbuka ujumbe wa wimbo huo.
Pia, hakikisha unakuwa na ufafanuzi wa kutosha. Beti 3 au 4 zinaweza kuzungumzia mada moja tu kwa kuifafanua. Mada ya wimbo inaweza kumlenga mtu mmoja au watu kadhaa.
Nyimbo nyingi zinaangukia katika makundi mbalimbali, kama vile nyimbo za mafundisho/maonyo, Nyimbo za Faraja, Nyimbo za Mahubiri,
Nyimbo za siasa, nyimbo za uchumi na nyimbo za kuburudisha ambazo ndani yake zinaweza kukosa ujumbe sahihi, lakini zikaishia kuwa na midundo mizuri kwa lengo la kusherehesha.

VYAKULA NA VINYWAJI KWA MWIMBAJI
Vilaji na vinywaji visivyofaa kabla ya kuimba, ni muhimu ili kuepuka kuimba  tumbo likiwa tupu kabisa. Kuimba ni kama riadha, inahitajika nguvu kwa ajili ya utendaji wako. Hata hivyo, ni muhimu pia kuepuka kuimba tumbo likiwa limeshiba sana.
Kumbuka kuimba ni kazi ngumu, unahitaji mafuta (you need fuel), hivyo inashauriwa kuwa na mlo wa kawaida wa saa moja au mbili kabla ya uimbaji.
Kulingana na mazoea yetu, vipo vyakula na vinywaji ambavyo ni vigumu kuachana navyo ghafla, mengine huchukua muda.

VYA KUZINGATIA UWAPO STUDIO YA MUZIKI
Mosi; Usikimbilie kwenye chumba cha kurekodia kabla hujawa tayari. Kusimama studio ili kurekodi inaweza kuwa ya kukatisha tamaa kwa waimbaji wapya. Hivyo, fanya mazoezi sana kabla ya kurekodi.
Pili; Jaribu kujirekodi mwenyewe kabla ya kuingia studio, na sikiliza kujua kile ulichokipenda, na kusahihisha usichokipenda. Chagua funguo sahihi ili kuweza kufikia nota za juu kwa wepesi, mbinu zako za kiuimbaji zinatakiwa kuwa nzuri kiasi cha kuzuia kupoteza muda katika studio kwa kurekodi mara nyingi, na kutumia tyuni nyingi.
Tatu; tumia vizuri microphone katika kuimba. Katika studio hakikisha kunakuwa na umbali fulani kutoka mdomoni mwako hadi kwenye microphone. Waimbaji wenye uzoefu mdogo kwenye microphones hujikuta wakiyumbisha vichwa vyao, kitu ambacho kinaweza kuharibu ubora wa sauti.Sogea karibu na microphone sauti inapokuwa ndogo, na mbali inapokuwa kubwa. Hii itakusaidia kuondoa tofauti ya kupanda na kushuka kwa sauti.
Nne; Epuka kusisitiza maneno yenye P na B ambayo mara nyingi huzalisha sauti yenye popp. Pia weka msisitizo kwenye maneno yenye F na S.
Tano; Dhibiti sauti za pumzi (kuhema kwa sauti). Kudhibiti sauti za pumzi wakati wa kurekodi itasaidia kuondoa usumbufu wakati wa kuhariri sauti.
Sita; Kabla hujaanza kurekodi, jaribisha aina tofauti za microphone kuona ni ipi inayofaa. Unaweza kurekodi ubeti mara kadhaa, na kusikiliza ipi inayofaa.