Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Watakiwa kuikingia kifua imani

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba-OSA, akimpatia Sakramenti Takatifu ya Kipaimara mmoja wa vijana wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kutoa Sakramenti hiyo katika Parokia ya Mtakatifu Agustino – Ukonga, jimboni humo. Wa pili kulia ni Paroko Msaidizi wa Parokia hiyo, Padri Joanes Kambadu. (Picha na Mathayo Kijazi) Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba-OSA, akimpatia Sakramenti Takatifu ya Kipaimara mmoja wa vijana wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kutoa Sakramenti hiyo katika Parokia ya Mtakatifu Agustino – Ukonga, jimboni humo. Wa pili kulia ni Paroko Msaidizi wa Parokia hiyo, Padri Joanes Kambadu. (Picha na Mathayo Kijazi)

DAR ES SALAAM

Na Mathayo Kijazi

Vijana wanapopokea Sakramenti Takatifu ya Kipaimara, wametakiwa kusimama imara, kujitambua na kuelewa wajibu wao wa kuishi maisha bora ya Imani Katoliki kama walivyofundishwa.
Kauli hiyo ilitolewa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba OSA, wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kipaimara kwa vijana 166 katika Parokia ya Mtakatifu Agustino – Ukonga, jimboni humo.
Askofu huyo alisema kuwa dhambi ni kikwazo katika ubinadamu, ambacho kinawafanya watu wawe vipofu na kushindwa kumwona Mungu katika maisha yao.
“Kwa hiyo ndugu zangu tutambue kwamba dhambi ni kikwazo katika ubinadamu, ambacho kinawafanya watu wawe vipofu na washindwe kumwona Mungu. Tuishi maisha ya kumpendeza Mungu,” alisema Askofu Musomba.
Vile vile, aliwasihi vijana waliopokea Sakramenti Takatifu ya Kipaimara kuepuka kuyumbishwa, huku akiwasisitiza kubaki katika imani yao Katoliki kwani wao wamekuwa ni Askari hodari wa Kristu.
Aliwaagiza Wazazi, Walezi na Waamini wote kwa pamoja, kushirikiana katika kusimamia malezi ya vijana hao, kwani kwa kufanya hivyo, Kanisa litapata watendaji walio bora.
Katika homilia hiyo Askofu Musomba pia aliwasihi Waamini kutokuisaliti imani yao na kutokuionea haya, akisema kwamba kufanya hivyo, ni kupotea katika imani.
Pia, alisisitiza kuepuka kiburi na majivuno katika mazingira wanayoishi, akiwasisitiza kuguswa na Roho Mtakatifu pamoja na kusikiliza kila wanachoelezwa.
“Epukeni kiburi na majivuno, kwamba bila mimi, hiki hakiwezi kufanyika. Jitahidini kuishi maisha ya kuguswa na Roho Mtakatifu huku mkisikiliza kila mnachoelezwa,” alisema Askofu Musomba.
Aliwataka Waamini kutambua kwamba ni wajibu wao kuiishi pamoja na kuishuhudia imani siku zote za maisha yao, kwani wao ni sura na mfano wa Mungu.
Katika hatua nyingine Askofu Musomba aliwashukuru Waamini wa Parokia ya Ukonga kwa ukarimu waliouonyesha kwake, kwani hiyo imemfanya ajihisi kuwa yuko nyumbani.
Kwa upande wake Paroko wa Parokia hiyo, Padri James Mweyunge alisema kuwa alipo Askofu, ndipo Kanisa lilipo, hivyo ni furaha kwao kusali pamoja na Askofu katika Adhimisho hilo la Misa Takatifu.
Padri Mweyunge aliwashukuru walimu (Makatekista) waliowafundisha vyema vijana hao hadi wameweza kufahamu mambo mengi yanayohusu Imani Katoliki.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.