Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi (mwenye Fimbo ya Kiaskofu), akiwa na Maaskofu Wasaidizi wake, Mhashamu Henry Mchamungu (mbele kulia), na Mhashamu Stephano Musomba (mbele kushoto), wakiwa katika Maandamano ya kuingia katika viwanja vya Seminari Ndogo ya Visiga, kwa Adhimisho la Misa Takatifu ya Kilele cha Miaka 50 ya Jubilei ya WAWATA, Jimboni humo. (Picha na Yohana Kasosi)

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, akiwauliza maswali vijana wa Parokia ya Mtakatifu Dominiko Savio, Mikoroshoni, Jimboni humo kabla ya kuwapa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kutoa Sakramenti hiyo. (Picha na Yohana Kasosi)

Na Pd. Richard Mjigwa

Siku ya Kuombea Utunzaji Bora wa Mazingira kwa mwaka 2022, imebebwa na Kauli mbiu: “Sikilizeni Kilio cha Kazi ya Uumbaji.”
Baba Mtakatifu Fransisko anakazia wongofu wa kiikolojia; (COP27) utakaofanyika Misri, Novemba 2022, Umuhimu wa utunzaji bora wa mazingira na deni kubwa la kiikolojia. Wongofu wa kiikolojia ni dhana ya Mt. Yohane Paulo II wakati ambapo Mt. Paulo alikazia wongofu wa janga la kiikolijia
Siku ya Kuombea Utunzaji Bora wa Mazingira kwa upande wa Kanisa Katoliki inayoadhimishwa tarehe 1 Septemba 2022 inanogeshwa na kauli mbiu “Sikilizeni Kilio cha Kazi ya Uumbaji.” Siku hii ilianzishwa rasmi na Baba Mtakatifu Francisko tarehe 10 Agosti 2015, kama sehemu ya mchakato endelevu na fungamani wa maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya Huruma ya Mungu, 2015-2016.
Baba Mtakatifu aliwataka waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kusimama kidete kulinda, kutunza na kudumisha kazi ya uumbaji. Kwa kuthamini na kujali umuhimu wa utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote, maadhimisho haya yakachukua mfumo wa kiekumene na kilele chake ni hapo tarehe 4 Oktoba ya kila mwaka.
Hii ni Sikukuu ya Mtakatifu Fransisko wa Assisi, aliyejisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya maskini, amani na utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote. Hii ni dira na mwongozo wa maisha na utume wa Baba Mtakatifu Fransisko kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.
Hiki ni kipindi muafaka cha kumwimbia Mwenyezi Mungu utenzi wa sifa na shukrani kwa kazi kubwa ya uumbaji sanjari na kujibu kwa vitendo kilio cha Mama Dunia na Maskini, hawa ndio wale “Akina yakhe pangu pakavu tia mchuzi.”
Patriaki Bartolomeo wa kwanza wa Kanisa la Kiorthodox la Costantinopol katika maadhimisho haya anakazia umuhimu wa kulinda na kutunza mazingira nyumba ya wote kwa kujikita katika mchakato wa uwajibikaji, ushirikiano na mshikamano wa udugu wa kibinadamu kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.
Utunzaji bora wa mazingira hauna budi kwenda sanjari na huduma kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa vipaumbele vya jamii. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa ajili ya Siku ya Kuombea Utunzaji Bora wa Mazingira kwa mwaka 2022 anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema akisema: “Sikilizeni Kilio cha Kazi ya Uumbaji.”
Anakazia wongofu wa kiikolojia katika maisha ya kiroho, Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP27) utakaofanyika nchini Misri, Mwezi Novemba 2022, Umuhimu wa utunzaji wa bora wa mazingira nyumba ya wote pamoja na deni kubwa la kiikolojia.
Wongofu wa kiikolojia ni changamoto iliyoyolewa na Mtakatifu Yohane Paulo II wakati ambapo wongofu wa janga la kiikolijia ni dhana iliyovaliwa njuga na Mtakatifu Paulo VI, mwaliko wa kusikiliza na kujibu kilio cha Mama Dunia na Maskini, ili dunia iweze kuwa ni mahali pazuri zaidi pa kuishi.
Baba Mtakatifu Fransisko anasema, ikolojia ya maisha ya kiroho iwahamasishe waamini kuwa na shauku ya kulinda mazingira, kwa kufungamanisha maisha ya kiroho na utunzaji bora wa mazingira, kwa kutambua uwepo angavu wa Mungu katika kazi ya uumbaji, kwa kuonesha moyo wa ukarimu na kujali kwa kutambua kwamba, ulimwengu ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, mwaliko wa kujitoa sadaka kwa ajili ya matendo ya huruma.
Kazi ya uumbaji na kilio cha maskini ni mambo yanayopaswa kupewa msukumo wa pekee, bila kuwasahau watu mahalia ambao kimsingi wamekuwa wahanga wa athari za mabadililo ya tabianchi kama vile: ukame wa kutisha, mafuriko, vimbunga pamoja na ongezeko kubwa la kiwango cha joto duniani. Lakini, ikumbukwe kwamba, kilio cha maskini kina nguvu kwani kinapanda hadi mbinguni.
Uchoyo na ubinafsi ni sababu kubwa ya kilio cha Mama Dunia na maskini na kwamba vijana wanawataka watu wazima, kusimama kidete kulinda ikolojia ya ulimwengu huu, kwa kuheshimu kazi ya uumbaji; kwa toba na wongofu wa ndani, kwa kujenga na kudumisha urafiki mpya na Mwenyezi Mungu pamoja na jirani.
Changamoto ya utunzaji bora wa mazingira haina budi kupewa kipaumbele cha pekee kama ilivyo pia kwa sekta ya afya na vita sehemu mbalimbali za dunia, wito kwa wote ni wongofu wa kiikolijia unaosimikwa katika wongofu wa kijumuiya ili kuleta mabadiliko ya kudumu; mambo yanayopaswa pia kuvaliwa njuga na Jumuiya ya Kimataifa.
Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP27) utakaofanyika nchini Misri, Mwezi Novemba 2022 ni sehemu ya mchakato kwa Jumuiya ya Kimataifa kutekeleza kwa vitendo Makubaliano ya Mkataba wa Paris kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, COP21.
Kwa hakika kizazi cha Karne ya 21 kitakumbukwa kwa kubeba dhamana na wajibu wa utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote. Kiwango cha wastani wa nyuzi joto 1.5C ndicho kinachotakiwa vinginevyo, Jumuiya ya Kimataifa itakuwa inakabiliana na janga kubwa la uchafuzi wa mazingira nyumba ya wote.
Kumbe, changamoto ya kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa kwa asilimia 45% ifikapo mwaka 2030 ni muhimu sana. Umoja wa Mataifa unabainisha kwamba, kuna haja ya kutekeleza kwa vitendo upunguzaji wa nyuzi joto 1.5C kama ilivyobainishwa kwenye Makubaliano ya Paris chini ya mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi.
Kila nchi itaamua kiwango cha mchango wake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Kiwango hicho kitategemea uchumi wa nchi husika na pia kiasi cha uzalishaji wa gesijoto. Kuongeza uwekezaji wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa angalau asilimia 50% ya fedha za jumla za ufadhili wa umma wa mabadiliko ya tabianchi.
Yote haya yanahitaji wongofu wa kiikolijia, unaojikita katika mchakato wa utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote; maendeleo fungamani ya binadamu, mshikamano wa udugu wa kibinadamu sanjari na upendo.
Wongofu wa kiikolojia unahitaji haki jamii hasa kwa watu maskini ambao wanaathirika vibaya kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Mkutano wa 15 wa Umoja wa Mataifa wa Bioanuwai (COP-15) utafanyika kuanzia tarehe 7 – 19 Desemba 2022 huko Montreal, Canada.
“UN Biodiversity Conference (COP 15) 7 - 19 December 2022 Montreal, Canada.” Huku zaidi ya spishi milioni moja za wanyama na mimea zikitishiwa kutoweka na robo tatu ya mfumo wa ikolojia wa Dunia kubadilishwa na shughuli za binadamu, COP-15 lazima ianzishe mfumo mpya wa kimataifa ili kukomesha mmomonyoko wa bayoanuwai ifikapo mwaka 2030.
Baba Mtakatifu Fransisko anakaza kusema, mintarafu hekima ya kale, maadhimisho ya Jubilei ni muda muafaka wa: “kukumbuka, kurudi, kupumzika na kurejesha.” Lengo ni kudhibiti kuporomoka zaidi kwa bayoanuwai, inayojenga “mtandao wa maisha” ambao mwanadamu amekirimiwa na Mwenyezi Mungu.
Jumuiya ya Kimataifa inapaswa kufikia makubaliano juu ya Kanuni Nne Muhimu: 1. kujenga msingi wa kimaadili wazi kwa ajili ya mabadiliko yanayohitajika ili kuokoa viumbe hai; 2. Kupambana na upotevu wa viumbe hai, kusaidia uhifadhi na ushirikiano, na kukidhi mahitaji ya watu kwa njia endelevu; 3.
Kukuza mshikamano wa kimataifa kwa kuzingatia ukweli kwamba, bayoanuwai ni mafao ya pamoja ya Kimataifa yanayodai dhamira ya pamoja; na 4. Kutoa kipaumbele cha kwanza kwa watu walio katika mazingira magumu, ikiwa ni pamoja na wale walioathirika zaidi na upotevu wa viumbe hai, kama vile watu asilia, wazee na vijana.
Baba Mtakatifu Francisko anarudia kusema: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, naomba makampuni makubwa ya uchimbaji madini na mafuta; uvunaji misitu, mali isiyohamishika, pamoja na biashara ya kilimo kuacha kuharibu misitu, ardhi oevu na milima; kuacha kuchafua mito na bahari, kuacha kutia sumu kwenye chakula sanjari na kujali watu na mazingira.
Je, tunawezaje kushindwa kukiri kuwepo kwa “deni la kiikolojia” (Laudato si’, 51) lililofanywa na nchi tajiri kiuchumi, ambazo zimechafua zaidi katika karne mbili zilizopita; hii inadai kwamba wachukue hatua kabambe zaidi katika COP27 na COP15.
Mbali na hatua zilizoamuliwa ndani ya mipaka yao, hii ina maana ya kuweka ahadi zao za msaada wa kifedha na kiufundi kwa Nchi maskini zaidi kiuchumi, ambazo tayari zinakabiliwa na mzigo mkubwa wa mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi.
Inafaa pia kuzingatia kwa haraka msaada zaidi wa rasilimali fedha kwa ajili ya uhifadhi wa bayoanuwai. Hata zile nchi tajiri kidogo kiuchumi zina majukumu makubwa japokuwa zinatofautiana katika suala hili; kuchelewa kwa upande wa wengine kamwe hakuwezi kuhalalisha kushindwa kwetu sisi wenyewe kuchukua hatua. Jumuiya ya Kimataifa haina budi kufanya maamuzi magumu kwani hali ni tete sana.
Kipindi hiki cha Sala kwa ajili ya kuombea Kazi ya Uumbaji, waamini wamwombe Mwenyezi Mungu, ili kwamba, Mikutano ya COP27 na COP15 iweze kutumika kuunganisha familia ya binadamu katika kukabiliana barabara na athari za mabadiliko ya tabia nchi sanjari na kupunguza bayoanuwai.
 Jumuiya ya Kimataifa ikumbuke himizo la Mtakatifu Paulo, Mwalimu na Mtume wa Mataifa: la kufurahi pamoja na wale wanaofurahi na kulia pamoja na wale wanaolia (Rej. Rum 12:15), watu waguswe na sala ya uchungu kuhusu kazi ya uumbaji na kutikia sala hii kwa vitendo, ili kizazi hiki na vizazi vijavyo viendelee kumshangilia na kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa wimbo mtamu wa Kazi ya Uumbaji, Uhai na Matumaini.

Frateri Gabriel Mtiti akiweka Nadhiri zake za Kwanza mbele ya Padri Dominic Somola, Mwakilishi wa Mkuu wa Shirika la Bikira Maria wa Mlima Karmeli nchini Tanzania, katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Kuweka Nadhiri za Kwanza na za Daima, kwa Mafrateri watatu wa Shirika hilo, iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli, Bunju, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. (Picha na Yohana Kasosi)

Waamini na Masista kutoka Majimbo Katoliki mbalimbali nchini Tanzania, wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Kuweka Nadhiri za Kwanza na za Daima, kwa Mafrateri wa Shirika la Bikira Maria wa Mlima Karmel, wawili ambao ni Frt. Felix Malimi na Frt. Gabriel Mtiti, wameweka Nadhiri za Kwanza, huku Frt. Dickson Sambala akiweka Nadhiri za Daima, iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli, Bunju, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. (Picha na Yohana Kasosi).

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu akiwa katika picha ya pamoja na vijana waliopata Sakramenti Takatifu ya Kipaimara wa Parokia ya Bikira Maria Konsolata, Makabe, jimboni humo. Kushoto ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Biju Pullapallyyil Joseph. (Picha na Elizabeth Chahoa)

Waamini wa Parokia ya Mtakatifu Dominiko Savio, Mikoroshoni, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa wamemshika mbuzi kwa ajili ya zawadi kwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kipaimara, iliyofanyika hivi karibuni Parokiani hapo. (Picha na Yohana Kasosi)

Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo (mwenye fimbo ya Kiaskofu), na Mapadri, wakiwa katika picha ya pamoja na vijana walioimarishwa katika Sakramenti Takatifu ya Kipaimara, iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Michael Malaika Mkuu, Kawe, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. (Picha na Yohana Kasosi)

Katika safu hii ya Chimba Chimba Historia ya Kanisa wiki iliyyopita, tuliwaletea jinsi Kanisa lilivyoanzisha Sheria za Kuendesha Kanisa. Leo tunawaletea jinsi Mashirika ya Kitawa yalivyoimarisha mwamko wa Ukristo Duniani.
Sasa endelea…

Kanisa Mlezi wa Elimu:
Katika kipindi hiki, Kanisa lilifufua elimu kuanzia ngazi ya parokia hadi chuo kikuu. Sasa kujua kusoma na kuandika ilikuwa ni fahari na kila mmoja alitamani na kuitafuta elimu.

Wakati huo, ni Kanisa tu ndilo lilikuwa na watu waliokuwa na ujuzi huo. Hivyo, liliongoza katika kuweka utaratibu wa elimu. Pole pole, Wafalme na Viongozi wengine walifuata baada ya kupata elimu toka Kanisani.

Kila Parokia ilikuwa na shule chini ya mwalimu au Katekista ambaye wakati huo huo alikuwa Msakristia, akisimamia usafi na mapambo kanisani, pamoja na kutayarisha mavazi na mambo mengine ya ibada.

Huyu alikuwa vile vile ‘kwayamasta’ akisimamia na kuongoza nyimbo wakati wa ibada, na alifundisha katekisimu kwa watoto wadogo na watu wazima waliojitayarisha kwa sakramenti mbalimbali.

Katika shule ya parokia, Katekista huyu aliwafundisha watoto kusoma na kuandika, pamoja na hesabu za msingi. Kama parokia ilikuwa kubwa, ilikuwa na Makatekista wengi kufuatana na mahitaji.

Wale waliofuzu parokiani na kufaulu, waliendelea na shule ya kati kwenye monasteri na kathedrali (cathedral), iliyokuwa kwenye makao makuu ya Askofu. Kuingia katika Shule ya Kati (Middle School), matajiri walilipia karo, lakini maskini wenye akili, walisomea bure.

Katika Shule ya Kati walijifunza masomo matatu ambayo wakati ule yalikuwa ya msingi (Trivium)  yaani Lugha (Grammar), Uandishi wenye mbinu za falsafa (Dialectics), na Usemaji au namna ya kutoa hotuba (Rhetoric).

Wakati huo huo pia waliwafundisha masomo ya sayansi manne (Quadrivium) yakiwa na Hesabu (Arithmetic), Geometry, Uwingu na Nyota (Astronomy), na Muziki.

Shule ya juu kabisa ilikuwa Chuo Kikuu. Chuo Kikuu cha kwanza kilifunguliwa mjini Paris, Ufaransa mwaka 1200 chini ya ulinzi wa Papa Innocent III.

Kuwa chini ya ulinzi wa Papa Innocent, kulikisaidia chuo hiki kisipate kubughudhiwa na watawala wengine, wakiwemo Wafalme, Watawala wadogo pamoja na Maaskofu waliomwogopa Papa.

Somo kuu katika chuo hiki kipya lilikuwa ni Tauhidi (Teolojia/Theology), elimu ya mafundisho ya dini. Baadaye vilianzishwa  vyuo vikuu vingine katika kila nchi na kila utawala.

Ilikuwa ni fahari kubwa kuwa na Chuo Kikuu katika mji au jimbo, hivyo Papa, Maaskofu, Wafalme na Watawala wengine walishindana katika kuanzisha Vyuo Vikuu.

Vyuo Vikuu vilikuwa na vitivo vinne; Teolojia, Sheria, Matibabu na Usanii; (Theology, Law, Medicine and Arts). Walikuwa na digri tatu, moja ya kuingilia waliyoiita ‘determinance’ ya pili ilikuwa ya kufuzu, yaani ‘baccalaureatus’ (bachelor), na ya mwisho likuwa ‘Licenciatus’, ambayo ni sawa kama Masters.

Udaktari haikuwa digrii ambayo mtu aliipata kwa kujifunza shuleni, bali kama mtu alifanya kazi nzuri na kujulikana, alitunukiwa hiyo kama heshima.

Sasa, bado kuna udaktari wa heshima, lakini mara nyingine huna la kufanya na kazi ya elimu ambayo mtu amechangia, na mara nyingine bahati mbaya, unanunuliwa.

Namna ya kufundisha chuoni ilikuwa kwa kufundisha (lectio/lectures), kuuliza maswali (questio/questioning) na kubishana (disputatio/disputatioing). Vyuo vikuu hivi vilichangia sana katika kuiinua Ulaya katika nyanja zote. Hata na safari za uvumbuzi ambazo ziliwachukua hadi Asia na Marekani, zilitokana na maendeleo ya elimu toka vyuo hivi.

Elimu ya Teolojia na Falsafa yatukuka:
Wakati huu Elimu ya Dini, au Teolojia, ndiyo ilikuwa elimu mama. Mtakatifu Anselmo aliandika kwamba falsafa (au elimu dunia) ni mjakazi wa Teolojia (au elimu dini). Mfumo wa elimu dini wa wakati huo uliitwa  scholasticism.

Ulaya ilikuwa imeunganika katika Kanisa moja, Imani moja na Falsafa moja. Ye yote aliyefundisha kinyume na imani hiyo, alikuwa ni mzushi, na alistahili kufa.

 Hata hivyo, ndani ya Imani hiyo palikuwa na uhuru mkubwa sana wa kufikiri, kutafiti na kubuni vitu mbalimbali ili mradi yote ni kwa ajili ya kujenga ufalme wa Mungu, na siyo kinyume chake.

Waalimu waanzilishi wa elimu hii walikuwa Mtakatifu Anselmo (1033-1109, Abelard (1079-1142), na Peter Lombard. Mwalimu mkubwa aliyeitwa daktari wa kimataifa (universal doctor) alikuwa Mtakatifu Alberto Mkuu (1193-1280.

Alberto alikuwa mtaalamu wa elimu dini, falsafa; fizikia na elimu nyingine za dunia. Aliweza kuoanisha elimu yote kwa pamoja na kuielekeza kwa Mungu.

Walimu wakuu wengine walikuwa Mtakatifu Bonaventura Mfansiskani, ambaye alitumia njia ya Mtakatifu Augustino, na mwanafalsafa wa zamani Mgiriki, Plato, kuelezea mambo ya dunia, akianzia kwa Mungu na uumbaji kwenda chini.

Mwingine alikuwa Mdominikani Mtakatifu Tomaso wa Akwino, ambaye alitumia njia ya Mtakatifu Alberto Mkuu kwa kutumia mwanafalsafa wa zamani Mgiriki, Aristotle akielezea mambo yote ya dunia kuanzia matukio ya binadamu ya kila siku, na kuelekea juu kwa Mungu.

Mtakatifu Tomaso vile vile alitunga nyimbo nyingi nzuri zinazoimbwa hadi leo kama ‘Lauda Sion Salvatore, Pange lingua gloriosa, Adorote devote, n.k. Nyimbo hizi zimetafsiriwa sasa katika kila lugha ambako Ukatoliki umefika.

Elimu ya Scholarsticism  iliunganisha elimu zote chini ya elimu ya Mungu (Teolojia). Wanateolojia hawa walitumia waalimu mashuhuri  wa elimu zote za zamani kutoka kwa Socrates, Plato, Aristotle, Archmides na wengine. Walionyesha wazi kwamba kila tamaduni inaweza kutumia mapokeo ya busara ya babu zao kuelezea Imani katika Mungu na Kristo.

Kufufuka kwa Roho ya Dini:
Maadili ya kidini sasa yalikubaliwa na kila mmoja na kuwa alama ya ustaarabu. Mifano ya kuigwa au mashujaa wa jamii walikuwa ni watakatifu, maaskari watawa (knights) wenye nadhiri za kutetea wanyonge, watu waliokwenda kupigana vita vitakatifu kukomboa Yerusalemu, na watu waliojitoa kwa Mungu kwa namna moja au nyingine.

Haki za watu zililindwa na kutetewa. Hadithi zilizosimuliwa au kutungwa wakati huo zilikuwa ni zile za  ushupavu wa kidini. Kwa kifupi, fasheni ya siku hizo ilikuwa kujenga ufalme wa Mungu.

Mashirika ya watawa yalichangia sana katika mwamko huu wa kidini. Mwaka 1000 BK palikuwepo Shirika la Wabenedictini tu, lakini kufika mwaka 1400, palikuwapo Mashirika mengi sana ya Watawa kwa ajili ya matakwa mbalimbali ya wakati huo.

Mashirika haya yote yalikuwa chini ya ulinzi wa Baba Mtakatifu. Shirika lililofungua dimba ni Monasteri ya Kluni.