Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

BASHE: Rais hataki utani kilimo cha umwagiliaji

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (Mb), akizungumza wakati wa kukabidhi Mradi wa Umwagiliaji wa Bonde la  Luiche, Mkoani Kigoma lenye ukubwa wa hekta 3000 kwa Mkandarasi M/S CRJE (East Africa) LIMITED ya Dar es Salaam, kwa ajili ya ujenzi wa bwawa na skimu ya umwagiliaji. Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (Mb), akizungumza wakati wa kukabidhi Mradi wa Umwagiliaji wa Bonde la Luiche, Mkoani Kigoma lenye ukubwa wa hekta 3000 kwa Mkandarasi M/S CRJE (East Africa) LIMITED ya Dar es Salaam, kwa ajili ya ujenzi wa bwawa na skimu ya umwagiliaji.

KIGOMA

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amewahakikishia Watanzania kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuleta mapinduzi kwenye Sekta ya Umwagiliaji, hivyo miradi yote aliyoahidi itatekelezwa.
Waziri Bashe alisema hayo wakati akizungumza na wadau wa umwagiliaji katika eneo la mradi wa Luiche, ambapo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha utekelezaji  wa mradi huo.
“Leo tumefanya uzinduzi wa Mradi Mkubwa wa Umwagiliaji katika Bonde la Luiche Wilayani Kigoma katika Mkoa wa Kigoma. Miradi hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 60 itakwenda kunufaisha zaidi ya wakulima 9312 kupitia Kilimo cha Umwagiliaji,”alisema Bashe.
Waziri Bashe alisisitiza kwamba utekelezaji wa miradi hiyo unaofanywa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, si hadithi, bali umelenga  kuinua Sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji, na kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.
Aliitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kujipanga kuhakikisha wanatekeleza miradi hiyo, na wananchi wapuuze wanaowalaghai kuuza mashamba.
Aliongeza kuwa wizara inamshukuru Rais Dk. Samia kwani anafanya kwa vitendo na hataki utani katika kilimo cha umwagiliaji.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa alimshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha utekelezaji wa mradi wa Bonde la Luiche, ambao umekuwa ukizungumzwa tangu nchi ilipopata Uhuru, na kwamba uwekezaji huo mkubwa uliofanywa na serikali unakwenda kuleta mapinduzi makubwa kiuchumi kwa wananchi wa Kigoma.
Mndolwa pia ametumia fursa hiyo kupokea maagizo ya Waziri wa Kilimo.
“Mradi huu ni mkubwa na utazingatia uwekaji wa miundo mbinu muhimu kama barabara na itazingatia kulinda vyanzo vya maji na mazingira”, alisema Mndolwa.
Mndolwa pia aliongeza kuwa Tume ilipokea maelekezo ya Serikali  kuwa mradi ujumuishe ujenzi wa   ghala, nyumba ya watumishi, pamoja na Ofisi ya Umwagiliaji.
Akiwasilisha Taarifa ya Umwagiliaji kwa Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Umwagiliaji Mkoa wa Kigoma, Katuta Mustang, alisema kwamba Mkoa wa Kigoma una eneo linalofaa kwa umwagiliaji lenye ukubwa wa hekta 147,000 ukiwa na skimu 59 za umwagiliaji skimu 6 pekee ndizo zilizoendelezwa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Salum Kalli alisema serikali itahakikisha ulinzi wa mradi huo.
Akimkaribisha Waziri wa Kilimo, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto Thobias Andengenye, aliishukuru serikali kwa uwekezaji Mkubwa unaofanywa katika Mkoa wa Kigoma, kupitia kilimo cha umwagiliaji.
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Ngenda Shabani Kirumbe,alimshukuru raid Dk. Samia Suluhu Haasan kwa kufanikisha utekelezaji wa Mradi wa Luiche.
Mradi wa Luiche upo katika wilaya ya kigoma, mkoa wa Kigoma. Mradi huu unajumuisha vijiji vya Kamara, Simbo, Kaseke, Nyamori, Msimba, Matiazo pamoja na Kagera. Mradi huu utakuwa na  ya hekta 3000 zitakazomwagiliwa baada ya ujenzi kukamilika. Mradi huu wa Luiche umegawanyika katika mikataba miwili ambayo ni Mkataba wa ujenzi wa bwawa pamoja na mkataba wa ujenzi wa skimu ya umwagiliaji.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.