Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Mtangulizeni Mungu katika maisha-Rai

Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, akimpa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara mmoja wa vijana 153 waliopata Sakramenti hiyo kwenye Misa Takatifu iliyoadhimishwa Parokia ya Mtakatifu Augustino, Salasala jimboni humo. Kulia kwa Kardinali ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Peter Assenga. (Picha na Yohana Kasosi) Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, akimpa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara mmoja wa vijana 153 waliopata Sakramenti hiyo kwenye Misa Takatifu iliyoadhimishwa Parokia ya Mtakatifu Augustino, Salasala jimboni humo. Kulia kwa Kardinali ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Peter Assenga. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, amewataka Waamini wamtangulize Mungu, wanapofanya jambo lolote, ili wapate neema kamili.
Kardinali Pengo alisema hayo katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara kwa vijana 150, iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Augustino – Salasala, jimboni Dar es Salaam.
“Watu wengi huwa wanapenda kujifanyia mambo wanayoyajua wao, na kuamua kumuacha Mungu. Ukijifanyia kitu bila kumtanguliza Mungu huwezi kufanikiwa,” alisema Kadrinali Pengo na kuongeza, “Hata kama unatamani na wewe uje kuwa Rais wa Taifa hili la Tanzania, au unataka uje kuwa mfanyabiashara mkubwa katika nchi hii, lazima umtangulize Muumba wako ambaye ni Mungu Baba iliyekubariki ili uweze kufaulu vizuli.”
Aliwasihi vijana waliopokea Sakramenti Takatifu ya Kipaimara kufahamu kwamba, sasa wamekuwa Wakristo kamili, akiwasisitiza kuyazingatia mafundisho ya Kanisa ili waendelee kudumu katika imani.
Kwa upande wake Paroko wa Parokia hiyo, Padri Peter Assenga aliwaomba wazazi na walezi wa vijana hao wasihame imani yao Katoliki, kwani ndiyo imani ya kweli.
Alimshukuru Kardinali Pengo kwa kuwapatia vijana hao Sakramenti Takatifu ya Kipaimara.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei wa parokia hiyo, Boniface Ngowi alisema kuwa kwa sasa Parokia hiyo imepata mafanikio makubwa, kwani wamejenga kanisa jipya kubwa ambalo lilitabarukiwa na Kardinali Pengo, alisema kuwa wao kama Parokia, wamejenga nyumba kubwa ya kisasa ambayo ilibarikiwa na kuzinduliwa na Askufu Mkuu wa Jimbo hilo, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.