Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Askofu awaonya Waamini vigeugeu

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, akitoa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara kwa kijana mmoja wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozari Takatifu, Makongo Juu wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti hiyo. Katikati ni Paroko wa Parokia hiyo, ambaye pia ni Mkurugezi wa Tumaini Media, Padri Joseph Massenge. (Picha na Yohana Kasosi) Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, akitoa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara kwa kijana mmoja wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozari Takatifu, Makongo Juu wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti hiyo. Katikati ni Paroko wa Parokia hiyo, ambaye pia ni Mkurugezi wa Tumaini Media, Padri Joseph Massenge. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mathayo Kijazi

Imeelezwa kuwa moja kati ya dhambi kubwa zinazowasakama wanadamu, ni kigeugeu, wakiaswa kuishi maisha yaliyo mema, huku wakijihami dhidi ya ugeugeu.
Hayo yalisemwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi wakati wa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara kwa vijana 78 katika Parokia ya Bikira Maria wa Rozari Takatifu – Makongo Juu, jimboni humo.
“Moja kati ya dhambi kubwa zinazowasakama wanadamu, ni kigeugeu. Kwa hiyo ndugu zangu, nawaomba sana mjiepushe dhidi ya ugeugeu,” alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi.
Aliwataka waamini hao kuacha tabia ya kwenda kwa waganga wa kienyeji kuaguliwa ili wafanikiwe, akiwasihi kuendelea kumtegemea Yesu Kristo kila wakati, kwani Kristo hapendi njia za mkato katika kufanikiwa.
Aidha, aliwasihi kujifunza kuundwa kwa njia za kuwajibika, akisema kuwa hiyo ndiyo njia pekee itakayowaepusha na njia za mkato.
Katika homilia yake Askofu Mkuu Ruwa’ichi, aliwataka Waamini kuacha uzembe, akiwasisitiza kuwa watu wa kupokea Neno la Mungu na mwili wa Kristu katika maisha yao.
“Tuache uzembe, tuwe watu wa kulishwa Neno la Mungu, na tuwe watu wa kupokea mwili wa Kristu, yaani Ekaristi Takatifu. Hayo mawili, tuyapokee katika hali ya kuwa na Roho safi. Tusipokee Neno la Mungu na mwili wa Kristu katika hali ya Roho zenye masizi, Roho zilizosakamwa na dhambi;
Alisema pia kuwa Mkristo hatakiwi kuona aibu kutokana na kujaa neema, bali aone aibu kutokana na kusakamwa na dhambi katika maisha yake.
Aidha, Askofu Mkuu Ruwa’ichi aliwasihi Waamini kutohangaikia chakula chenye kupita, bali wajitahidi kuhangaikia chakula chenye kudumu, ambacho ni Mapenzi ya Mungu, kwani yeyote anayekula chakula hicho, amekula chakula cha uzima.
Kwa upande wake Paroko wa Parokia hiyo, Padri Joseph Massenge, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tumaini Media alimshukuru Askofu Mkuu kwa kuadhimisha Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara.
Padri Massenge aliwakumbusha wasimamizi kuwasaidia watoto hao kupokea Sakramenti ya Kitubio, kwani asiyepokea Sakramenti hiyo, ni sawa na mtu asiyeoga.
“Wasimamizi nawaomba sana, wasaidieni watoto hawa kupokea Sakramenti ya Kitubio, kwa sababu asiyepokea Sakramenti ya Kitubio, ni sawa na mtu asiyeoga. Na kama mnavyojua, mtu asiyeoga ananuka, si ndiyo jamani,” alisema Padri Massenge.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei wa Parokia hiyo, Deogratius Mwarabu alimshukuru Askofu Mkuu, huku akimkabidhi kiasi cha fedha Shilingi milioni moja iliyoandaliwa na Parokia hiyo, ikiwa ni kumpongeza kwa Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu huyo.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.