Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

‘Saidieni wahitaji, hamtafilisika’

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu, akimkabidhi cheti mmoja wa vijana wa Parokia ya Mtakatifu Rita wa Kashia – Temboni, jimboni humo, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu. Kushoto kwa Askofu, ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Festo Ngonyani. (Picha na Mathayo Kijazi) Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu, akimkabidhi cheti mmoja wa vijana wa Parokia ya Mtakatifu Rita wa Kashia – Temboni, jimboni humo, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu. Kushoto kwa Askofu, ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Festo Ngonyani. (Picha na Mathayo Kijazi)

DAR ES SALAAM

Na Mathayo kijazi

Imeelezwa kuwa kila mmoja anatakiwa kujiwekea utaratibu wa kuwasaidia wahitaji, badala ya kujilimbikizia mali, ikiwemo fedha, kwani hakuna aliyefilisika kwa kutoa msaada kwa wenye shida.
Wito huo ulitolewa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu wakati wa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara kwa vijana 53 katika Parokia ya Mtakatifu Rita wa Kashia – Temboni, jimboni Dar es Salaam.
“Elisha alivyopewa ile mikate, angeamua kubaki nayo peke yake, lakini aliona kubaki nayo siyo sawa, akaamua kuwagawia wengine. Kwa hiyo ndugu zangu Waamini, nawaomba sana tujiwekee utaratibu huo wa kuwashirikisha wengine, kwa sababu hiyo itasaidia kutuwekea hazina mbinguni,” alisema Askofu Mchamungu.
Aliongeza kuwa fedha haziwezi kumkumbuka mtu aliyezimiliki kwa muda mrefu, bali atakapoamua kuwasaidia wengine, watamkumbuka na kumwombea hata akiwa hayupo duniani.
Alisema pia kuwa hata kama watu wanajitahidi kufanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato, watambue kwamba hawatakiwi kuwa wabinafsi na mali wanazozipata, kwani uhai walio nao na nguvu za kufanya hivyo, wamepewa na Mungu.
Aliongeza kuwa wapo watu ambao Mungu amewajalia kuwa na fedha ili zitumike kwa ajili ya kuwasaidia wengine, hivyo ni vyema kutekeleza wajibu huo wa kusaidiana.
Aliwasisitiza vijana kutowaacha wazee wahangaike kwa kutokuwasaidia, akiongeza kuwa kupitia Adhimisho hilo la Misa Takatifu ambayo pia ni Siku ya Kuwakumbuka Wazee, wajitahidi kuwasaidia.
Wakati huo huo alitoa wito kwa Waamini kwa pamoja kutokuwasahau wazazi wao waliopo vijijini, kwani wakiwakumbuka, kuwajulia hali, na kuwasaidia, wazee wao watafarijika.
Vile vile, alisema kuwa yeyote anayewasaidia wazazi wake, hubarikiwa, bali anayewaacha wakihangaika na kuteseka, hawezi kufanikiwa katika kila analolifanya.
Alitoa wito kwa Waimarishwa wa Sakramenti Takatifu ya Kipamiara, kuishi maisha ya kumpendeza Mungu na wanadamu, akiwataka kufahamu kwamba, ‘Kipaimara, siyo kwa heri Kanisa’.
Kwa upande wake Paroko wa Parokia hiyo, Padri Festo Ngonyani alimshukuru Askofu Msaidizi Mchamungu kwa Adhimisho hilo la Misa Takatifu ya kuwaimarisha vijana 53 wa parokia hiyo.
Padri Ngonyani aliongeza kwamba siyo tu kwa ajili ya Kipaimara, bali hata kwenda kuwasalimia kwa mara nyingine, watafarijika kumuona.
Naye Katibu wa Halmashauri ya Walei wa Parokia hiyo, George Kashushura aliwakumbusha wasimamizi kuwafanya vijana hao kuwa ni sehemu ya familia zao.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.