Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Paroko wa Parokia ya Familia Takatifu – Mburahati, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Vitalis Kassembo akiwabariki Waamini waliotoa Zaka wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika iliyoadhimishwa parokiani hapo.

Viongozi wa Halmashauri ya Walei ya Parokia ya Mtakatifu Maximilian Maria Kolbe – Mwenge, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Adhimisho la Misa Takatifu.

Waamini kutoka Parokia mbalimbali za Jimbo Katoliki la Mtwara, wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu iliyoadhimishwa hivi karibuni katika viwanja vya Kanisa Kuu jimboni humo. (Picha zote na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Chama Cha Pool Tanzania (Tanzania Pool Association: TAPA) kimepata mwaliko kwa wachezaji binafsi kushiriki mashindano ya JOY Grand Masters Final yatakayofanyika kuanzia Machi 24 hadi 29 mwaka huu huko Qinhuangdao nchini China.
Katika mashindano hayo, Tanzania itawakilishwa na Melckzedeck Amadeus aliyemaliza kama mchezaji bora wa Bara la Afrika katika mashindano ya Afrika yaliyofanyika Afrika Kusini mwaka 2023.
Msemaji wa Chama hicho Akida Kilango alisema kuwa mchezaji atakayependa kushiriki katika mashindano hayo anaweza kupata fursa hiyo kwa kujigharamia nauli ya ndege kwenda na kurudi, malazi, pamoja na chakula.
Alisema kuwa mchezaji huyo atatakiwa kuwasiliana na TAPA ili kuweka mambo sawa juu ya ushiriki wake.
TAPA itamsaidia katika upatikanaji wa nyaraka muhimu ikiwemo mwaliko kwa ajili ya safari na itagharamia gharama ya kupata VISA.

DAR ES SALAAM

Na Nicholaus Kilowoko

Wamiliki wa timu ya soka ya wanawake inayoshiriki Ligi ya Wanawake Tanzania Bara, Amani Queens yenye maskani yake mkoani Lindi, wameamua kuiuza timu yao kutokana na ukata wa kifedha ambao umesababaisha washindwe kuiendesha.
Wakizungumza kutokana na kukutana na changamoto hiyo, wamiliki hao walisema kuwa mpira kwa sasa unahitaji fedha, hivyo wao ilifika wakati wanakosa kabisa stahiki za wachezaji, hali ambayo imewafanya waamue kuiuza timu hiyo.
Walisema kuwa kipindi cha nyuma walikuwa wanaomba michango kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuiendesha timu hiyo, lakini kwa sasa imefikia mwisho na kuamua kuiuza timu hiyo kwa Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ.
Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa Lindi, Hosea Lugano alisema kuwa kutokana na mwenendo mbovu ulikokuwa nao timu hiyo, wamiliki wake walimaua kuiuza timu hiyo kwa wawekezaji wengine ambao ni JWTZ.

DAR ES SALAAM

Na Arone Mpanduka

Mwaka 2024 umeingia, huku wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakiwa wanakimbizana na wingi wa wasikilizaji na watazamaji kupitia mitandao ya kijamii.
Kwa mwaka jana 2023, zipo nyimbo nyingi zilizokuwa mstari wa mbele kwa kusikilizwa zaidi na watu pamoja na kutazamwa zaidi kwenye televisheni na mitandao ya kijamii.
Tumaini Letu linakuletea orodha ya baadhi ya nyimbo zilizofanya vizuri kwa mwaka jana.Ninasema baadhi kwa sababu zipo zingine nyingi zilizotikisa kwa mwaka jana.
JUX FT DIAMOND PLATNUMZ - ENJOY
Wimbo huu umevunja rekodi zake zote, kuanzia audio, video mpaka mapokezi ya mtaa, Enjoy ime-takeover kila mahali. Ikiwa na uchanga wa mwezi mmoja YouTube, Video ya Enjoy imekusanya watazamaji milioni 20 huku audio yake ikisikilizwa zaidi ya mara milioni 11 kwenye mtandao huo.
Enjoy ambayo ni kolabo na Diamond Platnumz, inavunja rekodi ya kuwa video na audio kubwa za Jux tangu aanze kuachia muziki kidigitali.
MBOSSO - AMEPOTEA
Mei 11, 2023 ndiyo tarehe ambayo Mbosso aliiachia video ya wimbo huo YouTube. Video ya Amepotea ilitosheleza kuwepo kwenye YouTube chaneli ya Mbosso bila kusindikizwa na audio wala lyrics video.
Video pekee iliyoachiwa YouTube imetazamwa kwa zaidi ya mara milioni 9.6 huku audio yake Boomplay ikiwa na wasikilizaji milioni 13.8 sambamba na milioni 3.25 Audiomack. Jumla ya streams za Amepotea ni milioni 26.75.
DARASA - NO BODY
Darassa aliziachia Mind Your Business, Dead Zone na moja kati ya nyimbo zake zilizofanikiwa kuwafikia watu wengi zaidi hata tuweze kusema kuwa Nobody ni miongoni mwa nyimbo zilizofanya vizuri mno mwaka huu.
Nobody iliyoachiwa Februari 24, ndio wimbo pekee wa msanii wa Hip Hop/Rap ulioweza kukusanya zaidi ya streams nyingi mwaka huu.
Kupitia Nobody peke yake, Darassa ameweza kukusanya zaidi ya wasikilizaji milioni 26.37. Video ya Nobody ambayo YouTube ina watazamaji zaidi ya milioni 1.5, haijafanya vizuri kama audio yake ambayo YouTube imesikilizwa zaidi ya mara milioni 7 na zaidi ya mara milioni 14.2 Boomplay na milioni 3.17 Audiomack.
JAY MELODY - SAWA
wimbo wake ‘Nakupenda’ na chorus yake kwenye ‘Puuh’ ya Billnass.
Baada ya matokeo chanya ya kazi hizo mbili, Jay aliufanya ‘Sawa’ kuwa wimbo wake wa pili kwa mwaka huo. Mpaka hivi sasa audio na video za Sawa zimekusanya watazamaji milioni 17.5 YouTube. Kwa upande wa Boomplay wimbo huu ulioachiwa Februari 27, umewafikia zaidi ya wasikilizaji milioni 36.9 na milioni 3.58 ‘Audiomack’.
Namba zinazoifanya jumla ya wasikilizaji wa wimbo huu kufikia milioni 57.98
ZUCHU - NANI
Ndani ya wimbo huu Zuchu ameshirikiana na mama yake mzazi, Khadija Kopa na msanii Innoss B kutoka nchini Congo, na hadi mwaka 2023 unamalizika, wimbo huo ulikuwa na zaidi ya watazamaji milioni 10.
Wimbo huu umejizolea umaarufu hasa kwa watoto wadogo ambao wengi walipenda staili yake ya uimbaji ambayo inaendana na nyimbo za watoto.
DIAMOND PLATNUMZ - YATAPITA
Diamond aliazimia kuumiliki mwaka 2023 kwa kufanya maajabu mengi na aliuanza mwaka na Yatapita. Wimbo ambao umekusanya zaidi ya streams milioni 44 YouTube video na audio, milioni 22.9 Boomplay na milioni 2.7 Audiomack. Streams za Diamond Platnumz kwenye orodha hii zinahesabika kuwa milioni 69.67.
Yatapita ni wimbo wa Diamond ambao umekusanya namba za wasikilizaji wengi kuliko nyimbo nyingine ambazo mkali huyo amefanya mwaka huo.
ALI KIBA FT MARIOO - MKE WA MTU SUMU
Akishirikiana na Marioo, Ali Kiba alitoa wimbo huo Julai mwaka jana, na kushika hatamu katika maeneo mbalimbali ya starehe bila kusahau vituo vya redio na televisheni. Kwa mfano kwenye youtube, wimbo huo umemaliza mwaka 2023 ukiwa na zaidi ya watazamaji milioni 6.
HARMONIZE - SINGLE AGAIN
Wimbo huu ulioachiwa siku ya wapendanao, umekusanya zaidi ya streams milioni 72.86, kwa mujibu wa namba za video na audio ya YouTube, ‘Audiomack’ na BoomPlay, Harmonize ndiye msanii mwenye wimbo unaokusanya wasikilizaji wengi zaidi ukiwa unachangia asilimia 15.7 ya streams zote kwenye orodha hii.
RAYVANNY FT MISSO MISONDO - KITU KIZITO
Mnamo mwezi Desemba 2023, video ya wimbo huu ilitoka. Rayvanny alijizolea mashabiki wengi kupitia wimbo huo kwa kipindi kifupi tu cha mwezi mmoja kabla yam waka kuisha hasa baada ya kuwashirikisha vijana machachari walioibuka na ubunifu kutoka Mtwara.
Misso Missondo ni jina la kimuziki la kijana mmoja DJ wa mtaani aliyeamua kubuni kundi lake maarufu kama ‘wazee wa makoti’ ambao huko kijijini walikuwa wakijipatia umaarufu kwa kucheza kwenye sherehe mbalimbali.
Staili yao ni ya singeli ingawa wameweka ubunifu wa kurudia beats za nyimbo za kawaida zilizowahi kuchezwa na wasanii wengine na kisha wao huingiza maneno yao na kucheza kwa staili yao tofauti. Singali zao zinasifika kwa ustaarabu bila kutumia lugha za matusi.

VIENNA, Austria
Mkuu wa timu ya Mercedes, Toto Wolff, ambaye pia anamiliki theluthi moja ya mabingwa wa zamani wa mbio za magari atasalia katika jukumu lake hadi angalau mwaka wa kwanza wa mabadiliko ya sheria kuu ya F1.
Toto Wolff, ambaye ni raia wa Austria, ametia saini mkataba mpya wa kusalia kama Mkuu wa Timu na Mtendaji Mkuu wa Mercedes F1, na kumwezesha kumaliza hadi mwisho wa msimu wa 2026.
Wolff, ambaye anamiliki sehemu sawa ya theluthi moja ya timu ya F1 na INEOS na Mercedes-Benz, alisema kuwa watatu hao waliamua wafanye hivyo tena, huku wakipanga njia ya kurejea kilele cha mchezo huo.
Wolff ameshikilia jukumu kuu la timu pamoja na umiliki wa hisa katika Mercedes tangu ajiunge nayo kutoka Williams mwaka wa 2013, na kuwaongoza kwenye rekodi ya Mashindano nane ya Wajenzi tangu mwaka 2014 hadi 2021, kabla ya wapinzani wao Red Bull kumaliza ubabe wao.
Kulikuwa na uvumi juu ya mustakabali wa Wolff katika nafasi ya bosi wa timu ya kila siku huko Mercedes, lakini mzee huyo wa miaka 52 anahisi bado ndiye mtu bora zaidi kwa nafasi hiyo, maoni yaliyoshirikiwa na Sir Jim Ratcliffe, Mtendaji Mkuu wa INEOS, na Mwenyekiti wa Mercedes-Benz Ola Kallenius.
“Nadhani jambo muhimu zaidi kati yetu sisi watatu, ni kwamba tunaaminiana,” alisema Wolff.

LEDDS, Uingereza
Helen Housby MBE amejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 14 cha Vitality Roses kitakachoshiriki Kombe la Mataifa ya Vitality kati ya Januari 20 na 21 na Januari 27 na 28.
Katika uwanja wa OVO Arena Wembley na First Direct Arena mjini Leeds wikendi mbili, Uingereza itamenyana na Australia, New Zealand na Uganda katika mchuano wa siku nne.
Mchezaji mwingine Nat Metcalf pia anarejea kikosini baada ya kuchukua mapumziko ya muda mrefu kufuatia kumalizika kwa Kombe la Dunia la Netiboli ambapo England walimaliza washindi wa pili kwa Australia.
Vitality Roses wanaingia kwenye shindano hilo wakiwa nyuma ya ushindi wa 2-1 wa Vitality Netball Series dhidi ya Afrika Kusini mnamo Desemba.
Kabla ya mchuano huo, Kocha Mkuu wa Vitality Roses, Jess Thirlby alisema kuwa Mashindano ya mwezi Januari daima yanatoa fursa nzuri kwao na Kombe hilo la Mataifa litakuwa mtihani mwingine mzuri kwa kikosi chao cha vijana, chenye vipaji dhidi ya mabingwa wa dunia Australia, nambari mbili duniani.
“Pamoja na muundo mkali wa wikendi mbili za mechi za mfululizo dhidi ya mitindo tofauti ya uchezaji na fainali ya kushindana, imewekwa kuwa jukwaa bora la kuendelea kuonyesha kile ambacho timu yetu inaweza kufanya,” alisema Jess.

DAR ES SALAAM

Na Arone Mpanduka

Fainali za Mataifa ya Afrika, maarufu kama (Africa Cup of Nations: AFCON) za mwaka 2023 zinaendelea nchini Ivory Coast ambapo zilianza Jumamosi ya Januari 13 mwaka huu.
Fainali hizo zinafanyika mwaka huu 2024 licha ya kuitwa za mwaka 2023, kwa sababu zilipaswa kufanyika mwaka jana.
Timu mbalimbali zimeanza kwa kuonyesha ushindani wa hali ya juu hasa zile ambazo hazikutazamiwa na wengi kama zingefanya vizuri mbele ya miamba inayotamba mara zote.
DOLA BILIONI MOJA
Hiki ni kiasi ambacho taifa la Ivory Coast limetumia katika kufanikisha fainali hizo, licha ya kupitia magumu katika miaka ya nyuma. Ikumbukwe kuwa taifa hilo lilikuwa likikabiliwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe, hali ambayo ilisababisha uchumi wake kutetereka.
Hakuna mtu aliyetarajia kama Ivory Coast wangeandaa fainali kubwa kama hizo bila kuwa na ushirikiano wa taifa lingine lolote. Kiasi hicho kimesaidia katika kukamilisha mambo mbalimbali kama vile ujenzi, matengenezo na ukarabati wa viwanja, miundombinu ya barabara, hospitali, hoteli za hadhi kubwa nk.
AKWABA
Ukifuatilia kwa umakini fainali hizi, kuna kikatuni utakuwa unakiona uwanjani kikiwa kinapita huku na kule. Muonekano wake ni kama tembo mwenye mkonga mdogo kwenye uso wake.
Kikatuni hicho kinafahamika kwa jina la Akwaba ambalo linatokana na neno la lugha ya kabila la Baoulé, likiwa na maana ya ‘welcome’ kwa Kiingereza na kwa Kiswahili ni karibu.Hii ikiwa na maana ya kuwakaribisha watu wote wanaotamani kushudia fainali hizo katika nchi ya Ivory Coast.
WIMBO WA AKWABA
Akwaba pia ni wimbo rasmi wa mashindano ambao umeimbwa kwa ushirikiano wa msanii wa Nigeria Yemi Alade, rapa wa Misri Mohamed Ramadan, na bendi ya muziki kutoka Ivory Coast ya Magic System.
Wimbo huu una mchanganyiko wa mahadhi ya afrobeat, rap, na zouglou, unaojumuisha mchanganyiko wa kipekee wa muziki uliokita mizizi katika utamaduni wa mashindano.
POKOU
Ni mpira rasmi wa mashindano ambapo jina hilo limamuenzi gwiji wa soka wa Ivory Coast, Laurent Pokou (marehemu), anayesifika kwa mafanikio yake ya historia ya kufunga mabao matano katika mechi moja ya ushindi wa 6-1 dhidi ya Ethiopia wakati wa mashindano ya mwaka 1970.
Mpira huo ndiyo ule tunaouona kwenye mashindano hayo yanayoendelea huko Ivory Coast, ambao una rangi nyeupe iliyonakshiwa na mchanganyiko wa rangi za bendera ya taifa hilo.
Mpira huo umetengenezwa kwa kiwango cha juu na kampuni mahiri ya vifaa vya michezo duniani ya Puma. Hivyo hata mpira huo unajulikana kama Puma Pokou.
ALASSANE OUATTARA
Ni uwanja pekee mkubwa kuliko yote inayotumika katika fainali za AFCON nchini humo. Uwanja huu upo mjini Abidjan na unaingiza watazamaji elfu sitini.Jina la uwanja huu linatokana na heshima ya Rais Alassane Ouattara.
Ndiyo uwanja uliotumika kwenye mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji Ivory Coast na Guinea Bissau na wenyeji kushinda 2-0.
LAURENT POKOU
Ni uwanja mwingine unaoingiza watazamaji elfu ishirini ambao umepewa jina la gwiji mshambuliaji wa zamani wa taifa hilo ambaye nimemuelezea huko juu.

DAR ES SALAAM

Na Arone Mpanduka

Katika miaka ya zamani, mipira ya kuchezea soka ilikuwa inajazwa upepo tu, na kisha timu kuchezea, lakini sasa hali imekuwa tofauti.
Sasa hivi ipo mipira ya kiteknolojia ambayo kabla ya kutumika uwanjani, lazima uifanyie vitu viwili ambavyo ni kujaza upepo na kuchaji.
Teknolojia hiyo ilianza mwaka jana mwishoni katika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini Qatar.
Mipira hiyo ndani yake imewekewa ‘chip’ maalumu, ambazo zinahitaji kuwa na nishati ya umeme ili kufanya kazi kwa usahihi.
Mipira hiyo ya kuchaji ilitengenezwa na kampuni ya Adidas, ina sensa ndani yake, ambayo inakusanya takwimu mbalimbali, kasi na uelekeo wa mpira, na kutuma ujumbe kwenye mashine za VAR kutambua kama kuna mchezaji ameotea (offside) au la.
Mfano kwenye fainali za mwaka jana, mipira ilikuwa ikichajiwa kama simu za mkononi, ambazo zilichomekwa kwenye umeme kabla ya mechi za Kombe la Dunia kuanza huko Qatar, na baada ya hapo waamuzi husika walikuwa wakikagua kila kitu na kuruhusu itumike. Hii ni tofauti na zamani ambapo kazi ya mwamuzi ilikuwa kukagua kiwango cha upepo tu.
Sensa iliyopo ndani ya mpira huo, inapewa nguvu na betri ndogo, ambayo uwezo wake wa kukaa na chaji wakati ukitumika ni saa sita na chaji itadumu kwa siku 18 kama hautakuwa unatumika.
Uzito wa sensa hiyo ni gramu 14 ambayo kazi yake ni kufanya uwelekeo wa mpira, huku ikiwa imeunganishwa na kamera mbalimbali zilizopo uwanjani ili kuwasaidia waamuzi juu ya mchezaji kuotea, na mambo mengine.
Mpira utakapopigwa kwa mguu, kichwa, kurushwa hata ukiguswa tu, meseji 500 zinakuwa zimetumwa ndani ya sekunde moja.
Data zinatumwa kwa wakati na haraka, kupitia antena za mtandao zilizowekwa kuzunguka uwanja wa mchezo, na hivyo kuhifadhiwa kwenye kompyuta kwa ajili ya matumizi inapohitajika.
Kama mpira utatoka nje ya eneo na kuingizwa mpira mwingine uwanjani, mfumo unakamata haraka na data zinanaswa zenyewe bila ya kuhitaji usaidizi wa kibinadamu.
Adidas imetengeneza mpira mwepesi na wenye kasi kubwa, kitu ambacho kilimfanya beki wa England, Kieran Trippier kufichua kuwa umekuwa ukimpa shida kwenye kupiga mipira ya adhabu ndogo.
Alisema kwamba kila alipojaribu kupiga mpira wakati wa adhabu ndogo, aligundua kuna utofauti, lakini hata hivyo hicho hakiwezi kuwa kisingizio katika jambo lolote.
Alisema kuwa mipira ipo tofauti, siyo suala la joto wala kitu kingine, na kwamba ikitumika nguvu kubwa kupiga mipira hiyo, ni rahisi kupaa.
Kwa miaka kadhaa, kampuni hiyo ya Adidas imekuwa ikitengeneza mipira mbalimbali yenye teknolojia ya kushangaza watu katika michuano mikubwa.
Kuna wakati walishawahi kutengeneza mipira yenye ‘sensor’ ndani yake, ambayo ilikuwa maalum kwa ajili ya kugundua kama mpira umevuka mstari wa goli.Na hii ilikuwa inaambatana na saa maalum anayovaa mwamuzi, ambayo ilikuwa inatetemeka kama ishara kwamba mpira umevuka mstari wa goli.
Kama saa ya mwamuzi haitetemi, ni dhahiri kwamba mpira haujavuka mstari, na mwamuzi hawezi kukubali goli.