Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Wanachama wa Moyo Mtakatifu wa Yesu, kutoka Parokia mbalimbali za Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakisali kabla ya kuanza Mkutano wao Mkuu wa Jimbo uliofanyika katika Ukumbi wa Kristo Mfalme, Parokia ya Kristo Mfalme, Tabata, jimboni humo.

Waamini wa Parokia ya Roho Mtakatifu – Segerea, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Kupokelewa na Kuteuliwa kwa Wakatekumeni 37, iliyoadhimishwa hivi karibuni parokiani hapo.
(Picha na Mathayo Kijazi)

Waamini wa Parokia ya Mtakatifu Yohane Mtume na Mwinjili, Tegeta Kibaoni, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa katika Adhimisho ya Misa Takatifu ya Dominika ya Kwanza ya Kwaresma iliyoadhimishwa parokiani hapo.

Viongozi wa Chama cha Moyo Mtakatifu wa Yesu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wakiongoza Sala kumshukuru Mungu baada ya Mkutano wao Mkuu wa Jimbo uliofanyika katika Ukumbi wa Kristo Mfalme, Parokia ya Kristo Mfalme, Tabata, jimboni humo. (Picha zote na Yohana Kasosi)

Na Joseph Mihangwa

LIPOISHIAI
...Ni utawala wa Chama dola na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Ingawa tumeingia mfumo wa Vyama vingi, Katiba inanuka harufu ya Chama kimoja kiasi cha watu wengine kukiita Chama kilichoshinda “Chama dola”, wakati ukweli dola si ya Chama, bali ni ya wananchi!.

ENDELEA...
Mhimili wa Chama na Ujamaa kati ya mitatu umekwishavunjika; Sera za Ujamaa na kujitegemea zimevunjwa na Azimio la Zanzibar mwaka 1992; nao mfumo wa Chama kimoja umeuawa na mfumo wa Vyama vingi vya siasa tangu mwaka 1992. Mfumo huu na ule wa uchumi huria, havikuwa katika mawazo ya watunga Katiba ya 1977. Ndiyo maana, Katiba ya sasa inakinzana kwa sehemu kubwa na mengi yanayotokea nchini.
Tunachosema hapa ni kwamba madaraka makubwa ya Rais asiyeambilika, yalidumu na kuweza kufanya kazi tu kwa msaada wa mafiga mawili yaliyovunjika – [Ujamaa na Chama kimoja], na kwamba, maadam sasa msaada huo haupo tena, madaraka makubwa ya Rais yataendelea kuelea na kupwaya kwa vigezo vyovyote vya utawala wa Sheria, demokrasia na utawala bora. Na pale Rais atajaribu kutenda kwa ubunifu wake binafsi kinyume na haya, hataepuka kuitwa “dikteta”.
Tunaambiwa, nchi yetu inafuata mfumo wa Utawala wa “Westminster”, unaozingatia Mgawanyo wa Madaraka.  Chini ya mfumo huo, muhimili mmoja wa Serikali unakatazwa kuingilia kazi za muhimili mwingine ili kila muhimili uchunge mwenendo wa muhimili mwingine.  Dhana hii sasa ipo kwa jina tu kama tutakavyoona hivi punde.
Marekebisho ya hapa na pale yaliyofanyika baadaye kwenye Katiba hayakugusa madaraka ya Rais, lakini badala yake, kadri sekta ya umma ilivyozidi kupanuka na ukuu wa mfumo wa Chama kimoja kujiimarisha, ndivyo jinsi madaraka ya Rais yalivyozidi kuwa makubwa. 
Aliweza kutumia nyundo ya Chama wakati huo huo kama Rais wa Nchi, na aliweza kutumia pia ngao ya Rais kulinda Chama wakati huo huo kama Mwenyekiti wa Chama. Rais wa Nchi na Mwenyekiti wa Chama Taifa kilikuwa na hadi leo ni kitu kimoja. Na ndiyo sababu ya Chama madarakani kuitwa “chama dola”! Kwa sababu hii, madaraka ya Rais yalipanuka kinyemela kuanzia na Katiba ya Nchi, hadi kwenye Katiba ya Chama cha Siasa tawala. Kwa sababu hii, Rais asiyeambilika [The Imperial Presidency], anachukuliwa kama moja ya nguzo au misingi mikuu mitatu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, inayoendelea kutumika hadi leo.
Uhalali wa madaraka makubwa ya Rais kwa mtazamo wa Watawala wa enzi hizo, ulikuwa ni kuharakisha maendeleo kwa njia ya “udikteta” wa Mkuu wa Nchi, ili asiulizwe ulizwe.  Mtazamo huu unadumu hadi leo.
Na katika kutekeleza hilo, Katiba ilitungwa kwa lengo la kuweka madarakani mtawala mwenye nguvu za imla, kwanza kuonesha kwamba Watanganyika sasa walikuwa huru kuweza kuendesha mambo yao wenyewe.
Pili, ilikuwa ni kuwezesha Serikali kuingilia kikamilifu [na bila ya kuhojiwa] katika maisha ya kijamii na kiuchumi ya wananchi, ili kuharakisha maendeleo kwa nguvu na imla ya kiutawala kwa “kushikisha adabu” waliohoji mwenendo wa nchi na wa watawala katika “kusukuma gurudumu la maendeleo.”
Maandalizi ya uchaguzi wa kwanza wa Rais asiyeambilika yalianza Juni 18 mwaka 1962 kwa kuandikisha wapiga kura 1,800,000 katika majimbo 50 ya uchaguzi. Wagombea walikuwa wawili – Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Chama cha TANU, na Bwana Zuberi Mtemvu, Rais wa Chama cha African National Congress – ANC. Uchaguzi ulifanyika Novemba 1, 1962 ambapo Mtemvu alishindwa vibaya kwa kupata kura 21,276, na Mwalimu Nyerere alipata kura 1,127,978.
Kuanzia hapo, Katiba ya nchi imekuwa ikiandikwa au kurekebishwa kukiwa na uwepo wa Rais, Mwalimu Nyerere vichwani mwa Waandishi wa Katiba. Hali haijabadilika.  Katiba yetu [ibara ya 63] inamfanya Rais kuwa sehemu ya Bunge la nchi kama njia ya kudhibiti demokrasia, kinyume na dhana ya Mgawanyo wa madaraka. Na ingawa mamlaka yote ya kutunga Sheria yamo mikononi mwa Bunge [ibara 64], lakini muswada wa Sheria hauwezi kuwa Sheria mpaka utiwe sahihi na Rais. Hakuna muda maalum aliopewa Rais kwa ajili hiyo; anaweza kukalia muswada kwa muda wowote atakavyo, kana kwamba yuko juu ya Wananchi kupitia Bunge.
Endapo atakataa kutia sahihi muswada asioutaka, na Bunge likashikilia msimamo wake juu ya muswada huo, Rais ana uwezo wa kulivunja Bunge na kuitisha uchaguzi mpya. Haya ni madaraka makubwa mno kwa Rais dhidi ya wawakilishi wa wananchi. Maana yake ni kwamba ingawa Bunge laweza kupitisha Muswada wa Sheria, ukweli Rais ndiye anayetunga Sheria kwa sababu ana hiari ya kukataa au kukubali Muswada wa Bunge na asiulizwe.
Rais anapogeuka kuwa Mtunga Sheria, Bunge lifanye kazi gani? Ili kulinda hadhi na ukuu wa Bunge linalowasilisha wananchi, busara inaelekeza Bunge lidhibiti bajeti yake, Tume yake ya Utumishi ina uwezo wa kupitisha miswada kuwa Sheria inapotiwa sahihi na Spika.
Kama ilivyokuwa kwenye Katiba ya Jamhuri [1962] kwa Rais kuongoza nchi atakavyo, na kuwa halazimiki kupokea ushauri wa mtu yeyote, Katiba ya sasa [ibara 37] bado inampa ridhaa hiyo, na hawezi kuhojiwa au kushtakiwa kwa vitendo vyovyote alivyofanya akiwa Rais na baada ya hapo [Ibara 46]. Pengine ni kwa sababu hii zama zetu, kumekuwa na vitendo visivyoendana na maadili ya taifa kwenye Ikulu bila ya woga, vilivyomfanya Baba wa Taifa apige kelele kwa kusema “Ikulu ni mahali patakatifu, panatakiwa paheshimiwe”, na akaonya pasigeuzwe pango la wafanyabiashara na walanguzi.
Kama lengo la kuwepo mihimili mitatu [Utawala, Mahakama na Bunge], ni pamoja na kuimarisha demokrasia, demokrasia itatoka wapi mhimili wa utawala unapodhibiti mihimili mingine?. Inapokuwa hivyo, kwa nini tuendelee kudai tunafuata mfumo wa demokrasia wa kibunge [Parliamentary Democracy], wakati vitendo vinaonesha kinyume chake?
Rais ndiye anayeteua Jaji Mkuu na Majaji [wanaosimamia mhimili wa Mahakama], Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Viongozi wengine. Kitendo cha kuteua chenyewe pekee kinamaanisha kwamba wateule hao wanawajibika kwake. Na kwa sababu hiyo mhimili wa kulinda haki [Mahakama], unawajibika kwa Rais pia. Hii inakwenda kinyume na dhana nzima ya mgawanyo wa madaraka na ya utawala wa Sheria kwa ujumla, kwa Rais kudhibiti Bunge na Mahakama, pamoja na Watendaji wake.
Kwa kusema haya, hatumaanishi kwamba kwa watawala kuvuka mipaka ya Kikatiba mara kwa mara hakuzai matunda siku zote, bali kwamba panatakiwa tamko thabiti lenye kueleweka juu ya aina ya demokrasia tunayopaswa kufuata kuweza kujipima na kuweza kupimwa pia kimataifa. Uhuru na demokrasia si lelemama, bali “UHURU”, kama alivyosema Baba wa Taifa, “ni KAZI”.
Tafsiri ya neno “demokrasia” ni pana kwa kuzingatia mahali na mazingira ya nchi. Lakini, kama Katiba ya Nchi ni hati yenye “utakaso”, na pia dira na ramani ya madaraka ya kuzingatiwa na kila mtu, basi, mfumo unaosimikwa na Katiba hiyo unapaswa kufahamika, kuzingatiwa na kuheshimiwa na wote; kinyume chake Katiba na demokrasia inageuka kuwa kejeli kwa wananchi wanaoitunga wakitarajia kwa matarajio kuona inafanya kazi. Ilivyo sasa, nchi yetu inafuata mfumo gani wa demokrasia: demokrasia ya [ukuu wa] kibunge, demokrasia ya kinasaba au ukuu wa kivikundi kwa misingi ya vyama vya siasa?
Tuseme nini zama hizi za siasa na uchumi huria na kwa Serikali kuachia nguvu za “soko” kusimamia sera na uchumi wa nchi na hivyo maisha ya watu, inapotokea mhimili wa Bunge na Utawala kuungana kuwa kitu kimoja?. Uhuru wa Mahakama utatoka wapi, kwa mfano, kwa kulazimisha chungu cha mstakabali wa nchi na demokrasia kukaa juu ya mafiga mawili badala ya matatu?
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
0713-526972

MWANZA

Na Paul Mabuga

Zawadi ya  tuliyopewa na Mungu ya huduma,  uhai na maisha ya mpendwa wetu Edward Lowassa, tuliyemhifadhi katika nyumba yake ya milele hivi majuzi huko Monduli, Mkoani Arusha ina mengi ya kutufundisha, lakini zaidi ni kwamba kila binadamu anazaliwa na haki ya kusifiwa, isipokuwa huwa inaporwa na ndiyo maana inahitaji kulindwa na kutetewa.
Kwamba, binadamu hatapata sifa kwenye familia yake au watu wa karibu nae basi ataitafuta nje yao. Wakati mwingine matokeo yanaweza kujenga uhitaji wa kuilinda haki hiyo huku wengine wakiibomoa katika ushindani ambao unajaa vitimbwi. Lakini wakati mwingine, sifa hutolewa bila kufurahisha wengine.
Kuna picha jongefu fupi mtandaoni ambapo mwongeaji hamasa, anayejitambulisha kwa jina la Michael Maundi, anajizungumzia yeye kama mfano ambapo anasema, tangu wakati anasomasoma shule ya msingi nafasi yake kwenye mitihani  ilikuwa ya 160 na 180, na hata alipofaulu kwenda kidato cha kwanza shule ye sekondari Kibasila mama yake alimuuliza, “huko darasani kwenu hakuna Michael Maundi Mwingine?” Akimaanisha mama yake alikuwa haamini kama amefaulu.
“Watu wote na hasa watoto wadogo walio nyumbani tunapenda sana sifa, tusipoipata nyumbani ama shuleni tunaitafuta mitaani! Mtaa unasifia, mtaa ukipakata kete [dawa za kulevya], mtaa unakuambua mwanangu umetisha… hata .. uki[anaonyesha ishara ya kuvuta bangi] mtaaa unakuambia mwanangu mwanangu, yaani wewe bonge la Mwambaaa!” anasema akionyesha umuhimu wa kuwasifia  watoto kabla ya kupata zile zisizo na maana.
“Mtoto anafanya kitu kikubwa nyumbani  wewe hata hushangilii, hustuki,[ inatakiwa] hata kama unakijua unashangaa, heee umejuaji mwanangu! Mtoto anapata moyo wa kutafuta vitu vingine kujua ili kuhadithia, … siyo anakuja kukuelezea kuhusu mto Kirumi uko hivi na hivi, halafu wewe unamvwambia, kwa hiyo wewe ndiyo umejua leo!” anaeleza Maundi katika kadamnasi inayomtazama katika picha hiyo fupi jongefu.
Kinyume chake anasema mwalimu wake wa darasa la saba wakatti anapata hesabu alama saba kwa hamsini kwenye mtihani wa kwanza,alimwambia Maundi una akili sana ili huitumii vuzuri. Wa pili alipopata 11 ya hamsini, akamyanyua juu na kumwambia, wewe ni nomaa, wewe ni mkemia mkuu, na mtihani uliofuata alipata alama zote.
“Mtoto mdogo atakuja kukupa kile [anachokiona] unachokiamini! Ukimuaminisha anaweza [ukimsifia unampa deni kubwa sana, … lakini kimuambua mjinga  mpumbavu mende paka .. atakuwa akijisemea hata mama anajua kuwa mimi ni paka!” anasema Maundi na kuongeza kuwa watu wengi duniani wamefanya makubwa kutokana na kulelewa katika miingi hiyp ya motisha ya kusifiwa.
Pia kuna majadiliano katika mtandao wa facebook  kupitia uzi mmoja ulioanzishwa na chombo kimoja cha habari nchini Kenya, ambapo inaonekana hoja ni Tanzania angalau kucheza Afcon 2023 iliyomalizika hivi karibuni, ambapo mmoja wa wachangiaji raia wa nchi hiyo ya awali anaandika katika hali ambayo inaonyesha pengine kutofurahia sifa za nchi yake ya jirani.
“Jirani hana dollar, jirani hana umeme, jirani hajui kizungu, jirani hakushinda hata mechi moja Afcon, jirani ana shida kweli kweli,” analeza Ogeto Nyamwange katika mtandani huo. Wapo pia engi waolichangia katika mtazamo huo. Mtanzania Caroline P Mwaipungu  anajibu, “Majirani mnajikutaga wazungu etu? Kama wa ulaya vile wakati hatutofautiani shida… eti kuzungu nini?? Mko na umbea mwingi loo!
Ingawa ni utani wa kawaida ambao hata umekuwepo kwa muda sasa kati ya raia wa nchi hizi lakini umekuwa hauna madhara. Zaidi utani huu ni kielelezo cha namna ambavyo binadamu anahitaji sifa, na anapohisi inachukuliwa anaona kuna haja ya kuilinda.
Usishangae binti akiingia gharama ya usafiri kurudi nyumbani kubadili mavazi baada ya kuambiwa aliyoyavaa hayajampendeza. Tunaponunua nguo tunalipia kupendeza siyo mavazi. Hii ni hoja ya kale kina binadamu alivyo.
Tukirejea katika enzi za uhai wake Lowassa  licha kusifiwa ambako kwa hakika kulijengwa na kupendwa kutokana na wasifu wake, na hata kuwa kipenzi cha watu, lakinini pia ni ukweli kuwa katika kipindi chake cha kazi na maisha aliukutana na bête noire [tanka bete nwaa], ikiwa na maana ya hali ya  kuchukiwa na sehemu fulani ya jamii..
Katika pande zote alizokuwa katika kazi zake, alikuwa kipenzi  na kupewa  sifa kem kem kwa upande mmoja huku kwa upande mwingine akipata bête noire.  Upande mmoja wa binadamu hao hao wakimpa sifa na kumtetea kwa nguvu zote wakati wa pili ukizipopoa sifa hizo ili kumpa bête noire kwa kila gharama yoyote.
Kitu kimoja cha msingi ni kwamba wakati kunyang’anywa kwa haki ya asili ya kusifiwa kunaweza kusababisha athari za kiafya katika maisha ya binadamu, lakini mara nyingi tumekuwa hatujali na  hatutoki mbele na kuwanusuru.  Watu walioporwa sifa wanazostahili kwa haki tumekuwa  tunasubiri wakati wakiaga dunia ili kuwasifia.
Na adui mkubwa wa sifa kwa mwanadamu ni ubinafsi ambao kila mmoja wetu anao. Yaani tunajijali zaidi kwanza sisi, na tunapoona ubinafsi wetu unatishia sifa zetu, tunapambana hata kama katika kufanya hivyo tunawanyang’anya wengine stahiki zao. Siyo lazima kila sifa imfurahishe mwingine, lakini inapaswa kuwa haki ya mmiliki.

DAR ES SALAAM

Na Arone Mpanduka

Hivi karibuni mwigizaji maarufu Carl Weathers, anayejulikana zaidi kwa uhusika wake kama Apollo Creed katika filamu nne za kwanza za “Rocky,” alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 76.
Familia yake ilinukuliwa ikisema Weathers alifariki kwa amani akiwa usingizini.
Carl Weathers alizaliwa Januari 14 mwaka 1948. Ni mwigizaji wa filamu na ni mchezaji mpira wa miguu wa zamani wa Kiamerika-Kanada.
Huenda akawa anafahamika zaidi kwa jina la Apollo Creed alilotumia kutoka katika mfululizo wa filamu ya The Rocky aliyocheza na nyota maarufu wa filamu, Sylvester Stallone maarufu kama Rambo.
Weathers alizaliwa mjini New Orleans, Louisiana. Alipata elimu yake katika shule ya St. Augustine High School na baada ya hapo alielekea katika Chuo Kikuu cha San Diego.
Nje ya maswala ya uigizaji, Weathers vilevile ni mwanachama wa Big Brothers na ni mmoja wa wanakamati ya Olympic ya Marekani. Mnamo mwezi wa Aprili ya mwaka wa 2007, Carl alimuoa Jennifer Peterson, mwandaaji wa documentary.
MAISHA YA SHULE
Weathers alicheza mpira wa miguu katika nafasi ya ulinzi akiwa chuoni. Alianza taaluma yake ya chuo mwaka 1966 katika Chuo cha Long Beach City, ambapo mwaka huo hakucheza soka kutokana na jeraha la kifundo cha mguu alilopata alipojikwaa kwenye ukingo uliozunguka njia ya kukimbia alipokuwa akijifua kwa mazoezi na mchezaji mwingine wa nyuma.
Kisha akahama na kuchezea Chuo Kikuu cha Jimbo la San Diego, na kuwa mwandishi wa barua kwa Waazteki wa Jimbo la San Diego mnamo 1968 na 1969, akiwasaidia Waazteki kushinda Pasadena Bowl mwaka 1969, akimaliza na rekodi ya 11-0, na nafasi ya 18 .
Katika Jimbo la San Diego, Weathers ambaye alifikiria kuigiza, na amekuwa akiigiza hata akiwa shuleni katika somo la sanaa ya maigizo.
KAZI ZAKE ZA FILAMU
Mbali ya “Rocky,” Weathers pia aliigiza katika filamu zingine maarufu kama “Predator” pamoja na Arnold Schwarzenegger na “Happy Gilmore” ya Adam Sandler.
Katika kipindi cha kazi yake ya zaidi ya miaka 50 huko Hollywood, alionekana katika zaidi ya filamu na vipindi 75 vya televisheni. Mwaka 2021, aliteuliwa tuzo ya Emmy kwa ajili ya uhusika wake katika “The Mandalorian.”
Pia aliongoza vipindi viwili vya mfululizo wa Star Wars, pamoja na vipindi vya “Law & Order” na “Chicago Med.” Pia alijulikana kwa filamu zingine kama “Action Jackson,” “Close Encounters of the Third Kind,” “Eight Crazy Nights,” “Little Nicky” na mfululizo wa “Toy Story.”
Familia yake pia ilisema kuwa Weathers, ambaye alianza kazi yake kama mchezaji wa mpira wa kikapu wa NFL, “alikuwa mtu bora.” “Kupitia michango yake katika filamu, televisheni, sanaa na michezo, ameacha alama isiyofutika na anataambulika duniani kote na vizazi vyote,” familia yake ilisema.
“Alikuwa ndugu mpendwa, baba, babu, mpenzi, na rafiki.” Mchezaji wa NFL aliyegeuka muigizaji alikuwa stadi katika kuigiza filamu za vitendo na vichekesho, akionekana katika filamu mbalimbali kama “Arrested Development” hadi “The Mandalorian,” ambapo aliigiza katika misimu yote mitatu ya mfululizo huu maarufu wa Disney.
Mcheza filamu mwenzake wa zamani, gwiji wa filamu za aksheni na gavana wa zamani wa California Arnold Schwarzenegger, alimsifu Weathers kwenye mtandao wa kijamii iliyojulikana zamani kama Twitter: “Carl Weathers atakuwa daima ni hadithi. Mwanamichezo bora, muigizaji mzuri, na mtu mkuu. “Tungekuwa hatuwezi kutengeneza ‘Predator’ bila yeye. Na hakika tusingekuwa na wakati mzuri wa kutengeneza filamu hiyo.”
Weathers, aliyezaliwa mwaka 1948 huko New Orleans, alianza kazi yake ya kucheza mpira wa kikapu katika Chuo Kikuu cha San Diego State, ambapo pia alisoma uigizaji, kabla ya kujiunga na timu ya Oakland Raiders mwaka wa 1970.
Mwigizaji wa “Breaking Bad” Giancarlo Esposito alisema: “Nitamkosa sana rafiki yangu mpendwa na ndugu Carl Weathers. Wewe ni kweli mmoja wa watu wazuri zaidi ambao nimepata heshima na furaha ya kutumia muda nao!”
Katika video iliyotumwa kwenye Instagram, mwenzake wa “Rocky” Sylvester Stallone alisema Weathers alikuwa “sehemu muhimu ya maisha yangu, mafanikio yangu... Nampa sifa nyingi.” “Singeweza kamwe kufanya kile tulichofanya na ‘Rocky’ bila yeye. Alikuwa mzuri kabisa,” Stallone aliongeza katika heshima ya kihisia. Katika mahojiano na gazeti la Detroit News mwaka jana, Weathers alijiita “mtu mwenye bahati”.

MADRID, Hispania
Mshindi wa medali ya fedha ya dunia ya mita 5,000 nchini Uhispania, Mohamed Katir, amepigwa marufuku kwa miaka miwili na Kitengo cha Uadilifu cha Riadha baada ya kukiri kukiuka sheria ya kupinga matumizi ya dawa za kusisimua misuli.
Katir, 25, alisimamishwa kazi kwa muda wiki iliyopita baada ya kukosa vipimo vitatu vya dawa za kuongeza nguvu katika muda wa miezi 12 na marufuku yake itaendelea hadi tarehe 6 Februari 2026, na hivyo kumtoa nje ya Michezo ya Olimpiki ya Paris.
Pia atakosa Mashindano ya Dunia huko Tokyo mnamo 2025, baada ya kushinda medali ya shaba katika mbio za mita 1500 mnamo 2022, na fedha katika mbio za mita 5,000 mnamo 2023.
Awali, Katir alisema kuwa atakata rufaa dhidi ya kusimamishwa kwake kwa muda, lakini wiki hii alikiri makosa kwa kushindwa kueleza aliko tarehe 28 Februari, 3 Aprili na 10 Oktoba, 2023.
Mkuu wa Shirikisho la riadha Brett Clothier, alisema katika kuelekea Paris 2024, ili kuhakikisha usawa, AIU itatekeleza mpango wa kina na unaoongozwa na akili nje ya mashindano kwa wanariadha mashuhuri duniani kote.

HAMBURG, Ujerumani
Mechi ya Ujerumani ya Bundesliga 2 kati ya Hansa Rostock na Hamburg, ilikatizwa hivi karibuni baada ya magari mawili yaliyoingia uwanjani baada ya dakika 10, yakitoa moshi wa bluu na nyeupe.
Kumekuwa na matukio kama hayo kote Ujerumani katika kupinga mpango uliopendekezwa wa kuuza hisa katika haki za Bundesliga kwa mwekezaji wa hisa za kibinafsi.
Mechi nne kati ya tano za Bundesliga Jumamosi zilikatizwa na maandamano, huku mashabiki wakirusha sarafu za chokoleti na marumaru uwanjani.
Maandamano hayo ni kujibu mpango kutoka kwa DFL, kundi la vilabu vya Ujerumani vinavyoandaa Bundesliga, kuuza sehemu ya 8% ya haki za Televisheni za siku zijazo ili kubadilishana na kuingiza mtaji kusaidia soko na kukuza ligi kote ulimwenguni.
Pendekezo hilo liliidhinishwa na theluthi mbili ya vilabu vya Ujerumani mwezi Desemba, ingawa makundi ya wafuasi yameitisha kura nyingine.

DAR ES SALAAM

Na Arone Mpanduka

Wachezaji saba wa Kitanzania wanaoshiriki Ligi Kuu soka Tanzania Bara wanaongoza kwa kufunga mabao ya mapema zaidi kuliko katika mechi za duru la kwanza za Ligi hiyo.
Ligi hiyo ya timu 16 tayari imemaliza raundi 15 za duru la kwanza hivi karibuni, na hivyo kuanza mechi za duru la pili la Ligi hiyo.
Nyota hao wazawa waliofunga mabao ya mapema katika mechi mbalimbali ni Mudathir Yahaya(Yanga), Sospeter Bajana(Azam FC), Yassin Mgaza(Dodoma Jiji), Awesu Awesu (KMC), Ibrahim Ajib (Coastal Union), Zidane Sereri(Dodoma Jiji) na Feisal Salum(Azam FC).
Mudathir Yahaya wa Yanga ndiye anayeongoza kwa kufunga bao la mapema zaidi kuliko wengine baada ya kufunga bao katika sekunde ya 44 kwenye mchezo wa Februari 17 dhidi ya KMC ambapo Yanga ilishinda 3-0 kwenye dimba la Jamhuri mjini Morogoro.
Sospeter Bajana wa Azam FC anafuatia kwa kufunga bao la mapema katika sekunde ya 54 dhidi ya JKT Tanzania, ambapo Azam ilishinda 2-1 siku ya Desemba 11 mwaka jana kwenye uwanja wa Azam Complex.
Awesu Awesu wa KMC alifunga bao katika dakika ya kwanza na sekunde 33 kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa FC katika dimba la Uhuru jijini Dar es salaam, ambapo KMC ilishinda mabao 3-2 Desemba pili mwaka jana.
Ibrahim Ajib aliifungia Coastal Union bao la mapema kwa njia ya penati katika dakika ya kwanza na sekunde 42 na kuipa pointi zote tatu timu yake baada ya mchezo kumalizika kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji kwenye dimba la Mkwakwani jijini Tanga.
Penati hiyo pia imekuwa ya mapema zaidi kutokea kwenye Ligi hadi sasa, baada ya kutokea katika sekunde ya 15 tu, kabla ya Ajib kufunga kwenye dakika ya kwanza.
Mchezaji Yassin Mgaza wa Dodoma Jiji alifunga bao katika dakika ya kwanza na sekunde 55 wakati walipocheza na wenyeji Tabora United kwenye dimba la Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabora ambapo hata hivyo Dodoma ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa 2-1.
Kiungo wa Dodoma jiji Zidane Sereri pia alifunga bao la mapema katika dakika ya pili dhidi ya KMC, huku Feisal Salum wa Azam FC akifunga bao katika dakika ya 3 dhidi ya Tabora United.
Kwa upande wa wachezaji wa kigeni waliofunga mabao ya mapema ni Zozuzoua Pacome na Kennedy Musonda, wote kutoka Yanga waliofunga katika dakika ya 3 kwenye mechi tofauti.