Marsiglia, Ufaransa
Kikundi cha Wananchi walio katika hali ngumu ya maisha wenye kupokea msaada kutoka kwa Watawa wa Shirika la Masista wa Mama Teresa wa Kalkuta, wamepata faraja baada ya kutembelewa na Baba Mtakatifu.
Akiwa huko Marsiglia, Baba Mtakatifu alitembelea kwa faragha Nyumba ya Masista wa Mama Teresa wa Kalkuta huko Mtakatifu Mauront, ambako kikundi cha watu walio katika hali ngumu ya kiuchumi, wanasaidiwa na watawa hao.
Katika ushuhuda wake Sista Crosvita alibainisha kuwa kwa kila mtu wanayemwona, ni kama Kristo.
Akizungumza na wanakikundi hao, Baba Mtakatifu alisema kuwa kuishi kama ndugu ni unabii.
Akiwa mjini Marsiglia, Baba Mtakatifu alifanya mkutano wa faragha na baadhi ya watu walio katika hali ngumu ya kiuchumi uliofanyika katika Nyumba ya Wamisionari wa Upendo, watawa wa Mama Teresa wa Calkutta, huko Mtakatifu Mauront, moja ya vitongoji kati ya watu maskini zaidi nchini Ufaransa.
“Asante kwa makaribisho yenu, kwani sisi sote ni ndugu, hii ni muhimu, mara nyingi ustaarabu wetu unatuongoza kuishi kama maadui au wageni… ishara ya kinabii ni kuishi kama ndugu na huu ni unabii, ule wa udugu unaokwenda zaidi wa mawazo ya kisiasa na kidini,” alisema Baba Mtakatifu Fransisko.
Kwa upande wa Sista Crosvita, alimmsimulia Baba Mtakatifu kwa hisia kali kwamba, kwani kwa miaka miwili akiwa mjini Marsiglia yeye na Masista wenzake, wamekuwa wakiendesha jiko la kupika supu kwa ajili ya maskini, ambalo linakaribisha watu 50 kwa wakati mmoja, mara tatu hadi nne kwa siku, kuanzia saa 3. 30 hadi 5.30, na katika siku moja inaweza kuwafikia watu 250.
Alisema kuwa watu hao ni maskini zaidi wengine wanaishi mitaani, ambao hivi karibuni kundi la watu wamefika kutoka Sudan, hawana pa kukaa, wanalala mitaani, na wengine hawana chakula.