Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Banki Mkombozi yapanda hadhi

Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande akipiga kengele kuashiria kupandishwa hadhi kwa Benki ya Mkombozi kutoka Soko la Ukuzaji Mitaji la DSE (EGM) na kwenda kwenye Soko Kuu la Uwekezaji (MIMS) katika hafla iliyofanyika Kambarage House jijini Dar es Salaam. (Picha na Mathayo Kijazi) Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande akipiga kengele kuashiria kupandishwa hadhi kwa Benki ya Mkombozi kutoka Soko la Ukuzaji Mitaji la DSE (EGM) na kwenda kwenye Soko Kuu la Uwekezaji (MIMS) katika hafla iliyofanyika Kambarage House jijini Dar es Salaam. (Picha na Mathayo Kijazi)

DAR ES SALAAM

Na Mathayo Kijazi

Benki ya Biashara ya Mkombozi imepandishwa hadhi kutoka Soko la Ukuzaji Mitaji la Dar es Salaam Stoke Exchange(DSE) (EGM) na kwenda Soko Kuu la Uwekezaji (MIMS).
Akizungumza katika hafla ya kuipandisha hadhi Benki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande alisema kuwa benki hiyo imepanda kutoka hatua moja kwenda nyingine ndani ya muda mfupi.
“Hongereni sana Mkombozi Bank kwa hatua hii mliyofikia, kwa sababu mmepanda hadhi kutoka hatua moja kwenda nyingine ndani ya muda mfupi sana…msiridhike na hatua hiyo mliyoifikia, kwa sababu kuna maneno yanasema ‘Mpanda patosha, huvuna pa mkwisha,”alisema Chande.
Naibu Waziri Chande aliwasihi watendaji wa Benki hiyo kutoridhika na hatua waliyofikia, badala yake waendelee kufanya uhamasishaji ili Benki iendelee kukua.
Aidha, Chande aligusia pia suala la riba kwa wanaochukua mikopo, na kusema kuwa Serikali inaendelea kulifanyia kazi suala hilo, ili riba inayochukuliwa, isiwe ya kuwaumiza wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Mkombozi, Respige Kimati, alisema kuwa Benki hiyo imewekeza nguvu nyingi ili kuanza kutoa gawio kuanzia mwakani 2025.
Alisema pia kuwa Benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kuungana na Serikali katika kuwashika mkono watu waliopatwa na majanga mbalimbali ndani ya jamii.
Kimati aliongeza kuwa Benki ya Mkombozi kwa sasa imepiga hatua kubwa ikilinganishwa na miaka 10 iliyopita, ina wakala zaidi ya 1000 kote nchini.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.