Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Hassan Shaw; Mchenza kinanda mahiri Vijana Jazz

Na Mwandishi wetu

Miaka ya nyuma kuna mtu alikuwa anaitwa Hassan Shaw ambaye alijulikana sana nchini hasa kwa wapenzi wa bendi ya Vijana Jazz ambao walimshuhudia kijana uyo wakati akitekenya Kinanda.
Alibonyeza Kinanda hicho na kumjengea umaarufu katika nyimbo za  ‘Shingo Feni’, ‘Penzi haligawanyiki’ na ‘Wifi zangu mna mambo’ ambazo zilikuwa zikiimbwa kwa sauti nyororo na mwanadada Kida Waziri katika ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni Jijini Dasr es Salaam.
Jina lake kamili ni Hassan Shaw Rwambo, aliyezaliwa Septemba 25, 1959 jijini Dar es Salaam. Alianza kujifunza kupiga gita na wenzie kando kando ya Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma, wakitumia magita ya tajiri mmoja aliyekuwa na meli ya uvuvi.
Aliporudi Dar es Salaam akakutana na mwanamuziki Zahir Ally Zorro, Zahir Ally yaelezwa kwamba ndiye aliyeboresha upigaji wake wa gita kiasi cha kukubaliwa kupiga gita la rhythm katika bendi yaya pili  Afro 70, iliyokuwa ikiitwa PAMA Band  iliyokuwa ikiongozwa na Patrick Balisidya.
Ni chini ya malezi ya Patrick akajifunza kupiga Kinanda baadaye mambo ya muziki na kujiunga na cha Ufundi cha Dar Technical College.
Mwaka 1980 alijiunga na bendi ya Vijana Jazz kama mpiga Kinanda ambako akilikutana na wanamuziki wengi akina John Kitime, Abuu Semhando kwa upande wa drums, mwimbaji wa wa kike Kida Waziri, Saad Ally Mnara na Hamisi Mirambo. Wengime walikuwa akina   Rashidi Pembe, aliyekuwa kipuliza Saxophone, Hassan Dalali na  Hamza Kalala walikuwa wapiga gita la Solo.
Ikimbukwe kwamba Hassan Dalali anatajwa humu ndiye yule baadaye akawa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Sports.
Mwaka 1990 alijiunga na Orchestra Safari Sound (OSS), chini ya  Muhidini Mwalimu Gurumo na Abel Balthazar. Huko OSS alikutana na wanamuziki wengine akina Benno Villa Anthony na Mhina Panduka ‘Toto Tundu’ambao walikuwa waimbaji.
Katika kujitafutaia maisha Hassan Shaw akaamua kuhamia Visiwani Zanzibar na kujiunga na bendi iliyokuwa ikipiga katika Hoteli ya Mawimbini.
Sifa zake za kubonyeza Kinanda zilipelekea kuitwa katika bendi ya Washirika Tanzania Stars. Alipotua hapo akakutana na wanamuziki wakali wakiwemo waimbaji mahiri akina Zahir Ally, Ally Choki Rwambow, Musemba wa Minyugu, Tofi Mvambe, na Abdul Salvador ‘Faza kidevu’ ambaye alikuwa na ‘manjonjo’ ya kupiga kinanda akitumia kidevu chake. Ndiyo sababu ya kuitwa ‘Faza Kidevu’
Shaw katika maisha yake hukupenda ujanja ujanja, hivyo kwa bahati mbaya katika bendi hiyo kulitokea kutokuelewana baina ya wanamuziki. Yeye kama kiongozi wa bendi, ikambidi aachie ngazi ili kuepusha bendi kuzidi kujichanganya.
Baada ya hapo mpulizaji mahiri wa tarumbeta, Nkashama Kanku Kelly alimuita ili ajiunge na bendi yake ya The Kilimanjaro Connection. Kanku Kelly na Hassan Shaw wameona nyumba moja  Kanku akiwa ni mume wa dada wa mke wake.
Kanku alimvumilia sana kwa kuwa hapo awali hakuwahi kufanya kazi ya kukopi nyimbo za wanamuziki wengine wakubwa duniani. Akiwa Connection alijifunza kukopi nyimbo nyingi za wanamuziki  wa kimataifa duniani.
The Kilimanjaro Connection ilikuwa inazunguka kwenda  kupiga muziki kwenye  hoteli  mbalimbali katika nchi za Malaysia, Singapore, Indonesia, Thailand na Japan, jambo ambalo kwake yeye ilikuwa  faraja kubwa.
Pamoja na Kanku Kelly, Shaw alishirikiana vyema na wamanuziki wengine akina Mafumu Bilal, Maneno Uvuruge, Burhan Adinan,  Shomari Fabrice, Bob Sija, na Faliala Mbutu. Wengine walikuwa Ray Sure boy, Delphin Mununga na Ramdhani Kinguti ‘System’
Baadaye Hassan Shaw, na wanamuziki wenzake Ramadhani Kinguti ‘ System’ na Burhan Muba wakafikia maamuzi ya kuanzisha kundi dogo la muziki wakitumia ala iitwayo Sequencer keyboards, wakiicha The Kilimanjaro Connection ya Kanku Kelly.
Kundi hilo likajiita Jambo Survivors Band ambalo baadaye likaaza safari za kuzunguka nchi mbalimbali kupiga muziki katika hoteli za kitalii. Ilifanya kazi katika nchi za Oman, Fujairah, Umoja wa nchi za Falme za Kiarabu (U.A.E), Singapore, Malaysia na Thailand.
Hassan Shaw kamwe hatowasahau maishani mwake ni pamoja na  Zahir Ally Zorro, Marehemu Patrick Balisdya, Waziri Ally, Ramadhani Kinguti ‘System’, Burhan Muba na Kanku Kelly kwa kuwa ni wao walomfikisha  hapo alipo.
Alipokuwa nchini Malaysia, alishindwa kupiga nyimbo baada ya kutoweka nyimbo zote  kichwani mwake.
Kama walivyo wanamuziki wengine wenye mafanikio, Shaw anapenda vijana kujifunza kupiga ala za muziki ili kufikia ndoto zao za kuwa wanamuziki wa kukubalika kimataifa. Pia amewataka vijana kutokata tamaa pale wanapokutana na vikwazo bali watafute jinsi ya kujinasua.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.