Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Usiyoyafahamu kuhusu AFCON

Uwanja wa Alassane Ouattara. Uwanja wa Alassane Ouattara.

DAR ES SALAAM

Na Arone Mpanduka

Fainali za Mataifa ya Afrika, maarufu kama (Africa Cup of Nations: AFCON) za mwaka 2023 zinaendelea nchini Ivory Coast ambapo zilianza Jumamosi ya Januari 13 mwaka huu.
Fainali hizo zinafanyika mwaka huu 2024 licha ya kuitwa za mwaka 2023, kwa sababu zilipaswa kufanyika mwaka jana.
Timu mbalimbali zimeanza kwa kuonyesha ushindani wa hali ya juu hasa zile ambazo hazikutazamiwa na wengi kama zingefanya vizuri mbele ya miamba inayotamba mara zote.
DOLA BILIONI MOJA
Hiki ni kiasi ambacho taifa la Ivory Coast limetumia katika kufanikisha fainali hizo, licha ya kupitia magumu katika miaka ya nyuma. Ikumbukwe kuwa taifa hilo lilikuwa likikabiliwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe, hali ambayo ilisababisha uchumi wake kutetereka.
Hakuna mtu aliyetarajia kama Ivory Coast wangeandaa fainali kubwa kama hizo bila kuwa na ushirikiano wa taifa lingine lolote. Kiasi hicho kimesaidia katika kukamilisha mambo mbalimbali kama vile ujenzi, matengenezo na ukarabati wa viwanja, miundombinu ya barabara, hospitali, hoteli za hadhi kubwa nk.
AKWABA
Ukifuatilia kwa umakini fainali hizi, kuna kikatuni utakuwa unakiona uwanjani kikiwa kinapita huku na kule. Muonekano wake ni kama tembo mwenye mkonga mdogo kwenye uso wake.
Kikatuni hicho kinafahamika kwa jina la Akwaba ambalo linatokana na neno la lugha ya kabila la Baoulé, likiwa na maana ya ‘welcome’ kwa Kiingereza na kwa Kiswahili ni karibu.Hii ikiwa na maana ya kuwakaribisha watu wote wanaotamani kushudia fainali hizo katika nchi ya Ivory Coast.
WIMBO WA AKWABA
Akwaba pia ni wimbo rasmi wa mashindano ambao umeimbwa kwa ushirikiano wa msanii wa Nigeria Yemi Alade, rapa wa Misri Mohamed Ramadan, na bendi ya muziki kutoka Ivory Coast ya Magic System.
Wimbo huu una mchanganyiko wa mahadhi ya afrobeat, rap, na zouglou, unaojumuisha mchanganyiko wa kipekee wa muziki uliokita mizizi katika utamaduni wa mashindano.
POKOU
Ni mpira rasmi wa mashindano ambapo jina hilo limamuenzi gwiji wa soka wa Ivory Coast, Laurent Pokou (marehemu), anayesifika kwa mafanikio yake ya historia ya kufunga mabao matano katika mechi moja ya ushindi wa 6-1 dhidi ya Ethiopia wakati wa mashindano ya mwaka 1970.
Mpira huo ndiyo ule tunaouona kwenye mashindano hayo yanayoendelea huko Ivory Coast, ambao una rangi nyeupe iliyonakshiwa na mchanganyiko wa rangi za bendera ya taifa hilo.
Mpira huo umetengenezwa kwa kiwango cha juu na kampuni mahiri ya vifaa vya michezo duniani ya Puma. Hivyo hata mpira huo unajulikana kama Puma Pokou.
ALASSANE OUATTARA
Ni uwanja pekee mkubwa kuliko yote inayotumika katika fainali za AFCON nchini humo. Uwanja huu upo mjini Abidjan na unaingiza watazamaji elfu sitini.Jina la uwanja huu linatokana na heshima ya Rais Alassane Ouattara.
Ndiyo uwanja uliotumika kwenye mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji Ivory Coast na Guinea Bissau na wenyeji kushinda 2-0.
LAURENT POKOU
Ni uwanja mwingine unaoingiza watazamaji elfu ishirini ambao umepewa jina la gwiji mshambuliaji wa zamani wa taifa hilo ambaye nimemuelezea huko juu.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.