Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Tengenezeni mahusiano na Mungu, asema Padri

Wakatekumeni waliopokelewa katika Parokia ya Roho Mtakatifu – Segerea, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wakiwa na Wasimamizi wao wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Kupokelewa na Kuteuliwa kwao, iliyoadhimishwa hivi karibuni parokiani hapo. (Picha na Mathayo Kijazi) Wakatekumeni waliopokelewa katika Parokia ya Roho Mtakatifu – Segerea, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wakiwa na Wasimamizi wao wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Kupokelewa na Kuteuliwa kwao, iliyoadhimishwa hivi karibuni parokiani hapo. (Picha na Mathayo Kijazi)

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Paroko wa Parokia ya Roho Mtakatifu – Segerea, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Denis Kunambi amewataka Wakristo kutumia kipindi cha Kwaresma kutengeneza vyema uhusiano kati yao na Mungu.
Padri Kunambi alisema hayo wakati wa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Kupokelewa na Kuteuliwa kwa Wakatekumeni 37, iliyoadhimishwa parokiani hapo.
“Tumieni kipindi hiki cha Kwaresma kuanza upya na kutengeneza vyema uhusiano yenu na Mungu. Licha ya kwamba hizi siku 40 ni zenye changamoto kubwa, lakini kumbukeni kwamba hata Kristo alijaribiwa,” alisema Padri huyo.
Aliongeza kuwa nguvu ya Mungu ni kubwa katika maisha ya Wakristo, huku akiwasihi kufahamu kwamba adui shetani hawezi kuishinda nguvu hiyo.
Padri Kunambi alisema kuwa kipindi cha Kwaresma ni cha kujichotea neema na baraka, kwani Mama Kanisa anamwezesha kila mmoja kuipokea neema hiyo.
“Ndugu zangu, kipindi hiki cha Kwaresma ni cha kujichotea neema na baraka, kwa sababu Mama Kanisa anamwezesha kila mmoja kuipokea neema na baraka hiyo katika maisha yake…
“Hiki ni kipindi cha kulitafakari Neno la Mungu, hasa katika nguzo kuu tatu, ambazo ni sala, kufunga, pamoja na majitoleo,” alisema Padri Kunambi.
Aliwasisitiza Waamini kutokuwa wazembe wa kuikimbilia Sakramenti ya kitubio, huku wakijitafakari na kuona kwamba nini kinachowasababisha kutokuikimbilia Sakramenti hiyo.
Padri Kunambi aliwataka kutafakari na kuondoa vizuizi vinavyowafanya washindwe kupokea matakatifu, ili waweze kubadilika.
Wakati huo huo aliwataka Wakatekumeni hao kuwa waaminifu, huku wakiwa tayari kumshuhudia Kristo siku zote za maisha yao.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.