VATICAN CITY, Vatican
Baada ya Maaskofu, Watawa, familia nzima, vijana, wanafunzi, wanandoa, Wamisionari, wahamiaji, wakimbizi wa kivita, mwaka huu 2024 ni Papa mwenyewe ameamua kutayarisha tafakari ya Njia ya Msalaba ya siku ya Ijumaa Kuu katika njia ya Uwanja wa Colosseum (Magofu ya kizamani ya mateso ya Wakristo wa kwanza.
Hii ni kwa mara ya kwanza katika kiti cha upapa cha Jorge Mario Bergoglio (Papa Fransisko).
Kusali pamoja na Yesu katika njia ya Msalaba ndiyo tema iliyochaguliwa kwa ajili ya tafakari itakayoambatana na vituo kumi na vinne vinavyokumbuka njia ya Yesu kuelekea Golgotha.
Tena inayotufanya kuelewa tabia ya “kutafakari kwa kina juu ya maandiko hayo ambayo, kama vile Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican ilivyosisitiza, kwamba itakuwa “Kitendo cha kutafakari na kiroho, na Yesu katikati.” Yeye atembeaye katika njia ya Msalaba na anajiweka katika safari pamoja nasi. Yote yanalenga sana kile ambacho Yesu anapitia wakati huo na ni wazi kwamba inapanua mada ya mateso ....”
Kwa njia hiyo rejeo la matukio la sasa litakuwa nalo moja kwa moja, kama katika miaka mingine ya nyuma ambapo wakimbizi, waathirika wa biashara ya binadamu au watu kutoka nchi katika vita walihusika, au, mwaka 2023, na ushuhuda na midahalo iliyochukuliwa kutoka katika nchi walizojeruhiwa na ambapo Papa alitembelea wakati wa ziara zake za kitume.
Hata kama katika Njia hii ya Msalaba, miunganisho yake ni mipana zaidi, ikiwa ni maombi ya marejeo yanapanuka... Sala haiendi kwa kundi la watu, bali kwa hali. Kwa hakika, chaguo ni kuunganishwa na Mwaka wa Sala ambao Baba Mtakatifu Fransisko amechagua kuutangaza kuwa maandalizi ya Mwaka wa Jubilei 2025, katika tukio ambalo, kama alivyokuwa amesema, kwanza kabisa lina tabia ya kiroho.
Kuhusu uwepo wa Papa Fransisko kwenye Njia ya Msalaba, kwa kuzingatia hali ya afya ya Papa na kushuka kwa joto jijini Roma, hakuna uthibitisho au kukanusha kutoka katika Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican: kile ambacho tayari kilitangazwa hapo awali kinabaki, ambacho ni kwamba Papa atakuwa huko Ijumaa usiku katika Palatine.
“Kwa sasa hakuna mabadiliko ikilinganishwa na yale ambayo tayari yametazamiwa.” Maandishi ya tafakari yatasambazwa siku ya Ijumaa tarehe 29 Machi 2024 na siku hiyo hiyo kutakuwa na maelezo zaidi juu ya nani atabeba Msalaba, kando ya barabara za kale karibu na Colosseum. Hakika watu wanaobeba msalaba wameunganishwa na kutafakari katika kila kituo.”
Mwaka 2013, kwa Njia ya Msalaba ya kwanza ya upapa wake, Papa Francisko alikabidhi tafakari kwa kundi la vijana wa Lebanon chini ya uongozi wa Kardinali Béchara Boutros Raï; (un gruppo di giovani libanesi sotto la guida del cardinale Béchara Boutros Raï;) mwaka 2014 ilikuwa ni zamu ya Asofu Mkuu Giancarlo Maria Bregantini,) wa Campobasso-Boiano; (rej. ( monsignor Giancarlo Maria Bregantini); mnamo mwaka 2015, Askofu Mstaafu Renato Corti, wa Jimbo la Novara;(rej. monsignor Renato Corti,); Mwaka 2016, alikuwa ni Kadinali Gualtiero Bassetti, Askofu mkuu wa Perugia-Città della Pieve, (rej. cardinale Gualtiero Bassetti,) na mwaka uliofuata alichaguliwa kuwa rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI.).
Mwaka 2017, Papa Fransisko alichagua msomi wa kibiblia wa Ufaransa Anne-Marie Pelletier (rej. Anne-Marie Pelletier,) mwanamke wa kwanza kushinda Tuzo ya Ratzinger, kama mwandishi wa tafakari kumi na nne.