Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Usiyoyajua kuhusu Ligi Kuu Bara 2023/24

DAR ES SALAAM

Na Arone Mpanduka

Katika Makala haya tunaangazia baadhi ya takwimu muhimu zilizojitokeza kwenye msimu wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara wa 2023/24 uliomalizika Mei 28 mwaka huu, huku Yanga ikiibuka na ubingwa wa 30 kihistoria.
MABEKI NA PASI ZA MABAO
Beki wa pembeni wa Yanga, Yao Kwasi na wa Azam FC Lusajo Mwaikenda ndio vinara wa kupiga pasi nyingi za mabao kuliko mabeki wote walioshiriki Ligi Kuu kwa msimu huo wa 2023/24 uliomalizika.
Kila mmoja amepiga pasi saba za mabao (assist). Beki wa kushoto wa Simba Mohammed Hussein amepiga pasi sita, Pascal Msindo (Azam FC), Nickson Kibabage (Yanga) na Rahim Shomari (KMC) kila mmoja amepiga pasi 5 za mabao kwa msimu mzima.
MABAO MENGI NDANI YA BOKSI
Kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum ndiye kinara wa kufunga mabao mengi zaidi akiwa ndani ya boksi la mpinzani. Ikumbukwe kuwa wapo wachezaji ambao wanaweza kufunga nje ya boksi kwa kupiga mashuti makali. Feisal amefunga jumla ya mabao 17 akifuatiwa na Aziz Ki ambaye amefunga 15 ndani ya boksi huku Waziri Junior wa KMC akifunga 11.
MABAO MENGI NJE YA BOKSI
Aziz Ki ndiye kinara kwenye hilo, baada ya kufunga mabao 6 nje ya boksi, huku akifuatiwa na Nicolaus Gyan wa Singida Fountain Gate aliyefunga mabao matatu.
AZIZI KI NA MABAO YAKE
Mabao 21 yaliyofungwa na kiungo mshambuliaji wa timu ya Yanga, Stephane Aziz Ki yamepiku mabao ya jumla ya timu tatu zilizoshiriki Ligi hiyo. Timu alizozipiku Aziz Ki ni Geita Gold (18), Dodoma Jiji (19), na Tabora United (20), ambazo zimemaliza msimu zikiwa hazijafikisha mabao 21 ya kufunga, huku akilingana idadi ya mabao ya kufunga na timu ya JKT Tanzania (21).
KIWANGO CHA UFANISI
Yanga imemaliza msimu ikiwa na kiwango bora cha ufanisi cha asilimia 88.88 ambacho ni kikubwa zaidi kuwahi kutokea tangu Ligi Kuu Tanzania Bara ianzishwe mwaka 1965. Asilimia hizo hupatikana kwa kuchukua namba 30(idadi ya mechi), kisha unazidisha mara 3(pointi za ushindi) ambapo jibu linakuja 90, na kisha unatoa 10(pointi ilizokosa Yanga msimu mzima) na kupata 80.
Baada ya hapo unachukua 80 unaweka juu ya 90(pointi za jumla za msimu) na kuzidisha mara 100 ili kupata asilimia za ufanisi.
TIMU YENYE ‘CLEAN SHEET’NYINGI
Achana na hati safi (clean sheet) ya golikipa mmoja mmoja, hapa tunazungumzia timu nzima ya mpira katika msimu uliopita ambayo kwa ujumla wake ubora wa safu ya ulinzi unakuwa na mchango wa kuifanya isiruhusu bao lolote kwenye mechi nyingi.
Yanga ndiyo inayoongoza kuwa na clean sheet nyingi zaidi(20) ikifuatiwa na Coastal Union ya Tanga(16). Ikumbukwe pia kuwa timu hizo zilichezesha makipa tofauti tofauti kwenye msimu mzima ambapo Yanga iliwatumia Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery na Metacha Mnata ingawa Diarra alitumika kwenye mechi nyingi kuliko wenzake, na Coastal ikimtumia zaidi Ley Matampi.
TIMU YENYE PASI NYINGI
Yanga inaongoza kwa kupiga jumla ya pasi 10,830 kwenye mechi zote 30 za msimu, ikifuatiwa na Azam FC iliyopiga pasi 10,084 huku Simba ikiwa nafasi ya tatu kwa kupiga pasi 9890.Yanga pia imepiga kona nyingi (200) ikifuatiwa Simba ambayo ilipiga kona 165 msimu mzima.
TIMU ILIYOPOTEZA MECHI NYIGI
Mtibwa Sugar ya Morogoro ndiyo kinara kwa kupoteza mechi nyingi msimu uliopita baada ya kupoteza mechi 19 na kusababisha washuke Daraja.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.