Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Ujue mchezo wa Raga na maajabu yake

DAR ES SALAAM

Na Deus Helandogo

Raga, maarufu kama Rugby, ni mchezo ulioanzishwa mwanzoni mwa karne ya 19 katika Mataifa ya Uingereza na Marekani, na una namna nyingi ya kuchezwa, kama vile kwa kutumia mikono pamoja na miguu, huhusisha wachezaji 15 kwa kila upande wa timu shindani
Mchezo huu ni maarufu sana kwenye Mataifa ambayo yana shabihiana kiutamaduni na Taifa la Uingereza, ikiwemo Umoja wa Jumuiya ya Madola kama vile Austalia, Kenya, Afrika Kusini, Canada na Namibia, kwenye baadhi ya Mataifa mchezo huu ni mchezo ambao una sifa ya kuwa mchezo wa Kitaifa
Raga ilianza pamoja na mchezo wa mpira wa miguu, na baadae sheria za michezo hiyo miwili zikatofautiana  na kuwa michezo miwili tofauti. Raga ikabaki ikichezwa kwa kutumia mikono na miguu, huku mpira wa miguu akaanza kuchezwa  kwa kutumia miguu tu
Mpira unaotumika kuchezea Raga umetengenezwa kwa mfumo wa umbo mviringo, mithili ya yai unaoweza kubebeka na kukimbia nao, ukiwa mkononi, na inapotokea kuurusha haumsumbi mchezaji huurusha kwa haraka
Takwimu zinaonesha kuwa mchezo huu umezidi kukua kwa kasi ulimwenguni  kwani huchezwa na kila jinsia na umri wowote. Mwaka 2023, ilithibitika kuwa zaidi ya watu milioni kumi (10) hucheza  mchezo huu  duniani kote.
Na katika kipindi hicho, watu milioni 8.4 walikuwa wamesajiliwa na Chama cha mchezo huo duniani ambacho kifupi chake ni (IRFB), na Mataifa 116 yana vyama vinavyoongoza mchezo wa Raga duniani kote.
Kuanzia miaka ya 1863, mchezo huu ulikuwa unachezwa kama ridhaa kwa kujifurahisha zaidi, na siyo kazi rasmi ambayo ilikuwa na maslahi, mpaka ilipofika mwaka 1995 ndipo sheria mpya zilitungwa na kuurasimisha mchezo huu ambapo ulianza kulipa wachezaji, makocha  na waamuzi,  hivyo watu wakaanza kunufaika na mchezo wenyewe.
Mchezo wa kwanza wa Raga wa Kimataifa  ulichezwa mnamo 27 Machi, 1871 kati ya Scotland na Uingereza huko Edinburgh, Scotland ilishinda mchezo huo kwa bao moja, hadi kufikia mwaka 1881, ambapo Ireland na Wales zilikuwa na timu za uwakilishi katika mashindano ya Kimataifa
Mashindano muhimu zaidi katika mchezo wa Raga ni Kombe la Dunia la Raga, mashindano ya wanaume, ambayo yamekuwa yakifanyika kila baada ya miaka minne tangu kuzinduliwa kwa michuano hiyo mnamo mwaka 1987.
Afrika Kusini ndiyo Mabingwa watetezi baada ya kuifunga New Zealand 11-12 katika fainali ya Kombe la dunia la Raga 2023 nchini Ufaransa.
Lakini katika historia, Afrika Kusini ina idadi kubwa zaidi ya kushinda makombe, kwani imeshinda Kombe la Dunia mara nne (1995, 2007, 2019 na 2023).
New Zealand imeshinda taji hilo mara tatu (1987, 2011 na 2015); Australia imeshinda mara mbili (1991 na 1999); na Uingereza mara moja (2003).
England ndio timu pekee kutoka Kaskazini mwa Bara la Ulaya ambayo imeshinda Kombe la dunia la Raga
Kombe la Dunia la Raga limeendelea kukua tangu kuanzishwa kwake mwaka 1987 kwani mashindano ya kwanza, ambayo timu 16 zilishiriki ilionyeshwa kwa nchi 17, na jumla ya watazamaji milioni 230 wa televisheni, walishuhudia. Mauzo ya tiketi wakati wa hatua za bwawa na fainali za mashindano hayo, yalikuwa chini ya milioni Kombe la Dunia la mwaka 2007 lililoshindaniwa na nchi 94, na mauzo ya tiketi yalikuwa  3,850,000.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.