Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

‘Wekezeni maadili mema kwa Watoto’

Baada ya Adhimisho ya Misa Takatifu ya Kutabaruku Kanisa la Parokia ya Kung’ara kwa Yesu Kristo, Mbezi Mshikamano, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi anaoneshwa mchoro wa nyumba ya Mapadri inayojengwa parokiani hapo. (Picha na Yohana Kasosi) Baada ya Adhimisho ya Misa Takatifu ya Kutabaruku Kanisa la Parokia ya Kung’ara kwa Yesu Kristo, Mbezi Mshikamano, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi anaoneshwa mchoro wa nyumba ya Mapadri inayojengwa parokiani hapo. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mathayo Kijazi

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, amesema kuwa jamii isipobadilika na kuwekeza katika maadili mema kwa watoto wao, Ulimwengu utawateka.
Askofu Mkuu Ruwa’ichi alisema hayo katika Adhimisho la Misa Takatifu ya kutoa Sakramenti ya Kipaimara iliyokwenda sanjari na Kutabaruku Kanisa la Parokia ya Kung’ara kwa Yesu Kristo, Mbezi Mshikamano, iliyokuwa ikifahamika awali kama Parokia ya Mtakatifu Yohane Paul II, Mbezi Mshikamano.
Aidha, Askofu Mkuu Ruwa’ichi alimwagiza Paroko wa Parokia hiyo kuhakikisha watoto wote walioimarishwa wanatengenezewa utaratibu mzuri wa kuendelea na mafunzo ya Imani Katoliki, ili waweze kuimarika zaidi katika Imani hiyo.
Wazazi na walezi walikumbushwa pia kufahamu kwamba kwa sasa Dunia imekengeuka, hivyo ni wajibu wao kuhakikisha kwamba wanawekeza Imani kwa watoto wao, kwani kwa kushindwa kufanya hivyo, Ulimwengu utawekeza kwa watoto hao, na hivyo watapotezwa.
“Wekezeni maadili mema kwa Watoto wenu, hasa katika wakati huu ambapo dunia hii imemezwa na mambo mabaya kwa sababu msipowekeza sasa, dunia itawekeza kwako,” alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi.
Askofu Mkuu aliongeza kuwa hali ya maisha ya Dunia hasa katika suala la maadili, limekuwa baya akiisihi jamii kuwalea watoto katika misingi thabiti ya kiimani, ili watoto hao wasije kutekwa na Ulimwengu.
Awali katika homilia yake Askofu Mkuu Ruwa’ichi, aliwasisitiza Waamini hao kuwa kama walivyojenga kanisa zuri, wanatakiwa pia kuwa wazuri na wenye kujaa neema kutoka ndani ya mioyo yao.
“Wewe ni kanisa, wewe ni hekalu, wewe ni makao ya Roho Mtakatifu. Sasa kama mmejenga kanisa zuri, hebu kwanza muanze ninyi wenyewe kuwa wazuri. Muanze kujifunza kuwa watu mliojaa neema. Msiruhusu Mioyo yenu, akili zenu, dhamiri zenu, na nafsi zenu zijae masizi ya dhambi,” alisema Askofu Ruwa’ichi.
Aidha, aliwakumbusha Waamini wa parokia hiyo kufahamu kwamba kanisa na altare vinapopakwa mafuta ya Krisma, vinakabidhiwa mikononi mwa Mungu ili aviweke rasmi kwa ajili ya mambo yanayomhusu Yeye na watu wake.
Askofu Mkuu aliwataka Wakristo hao kulitumia kanisa hilo kwa ibada stahiki na kwa heshima inayostahili, akiwaonya wale wasioelewa kwamba wako wapi, watambue wako mahali patakatifu.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.