Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Askofu Mchamungu atema cheche

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu akikabidhi funguo za kanisa kwa Paroko mpya wa Parokia ya Mtakatifu Maria Salome-Kimara, Padri Boniface Omondi, baada ya kumsimika wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika iliyofanyika parokiani hapo. (Picha na Yohana Kasosi) Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu akikabidhi funguo za kanisa kwa Paroko mpya wa Parokia ya Mtakatifu Maria Salome-Kimara, Padri Boniface Omondi, baada ya kumsimika wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika iliyofanyika parokiani hapo. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Viongozi wa Dini na Wanasiasa nchini, wanatakiwa kuzingatia hekima ili waweze kutenda vyema, kwani wasipokuwa na hekima, watasababisha vurugu na taharuki katika jamii kwa kuongea mambo mabaya dhidi ya watu wengine, hata kama mambo hayo hayapo.
Hayo yalisemwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu, wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Maria Salome, Kimara, jimboni Dar es Salaam, iliyokwenda sanjari na kumsimika Parokoa mpya wa parokia hiyo, Padri Boniphace Omondi.
“Wazingatie hekima, kwani watatenda kama vile Mungu anavyotaka, asiye na hekima anaweza kuingia katika mambo ya ulevi, hana cha maana sana sana ataongelea ya wengine na tena ya ajabu ajabu,”alisema Askofu Mchamungu, baada ya kumsimika Parokia mpya, Padri Omondi.
Viongozi wasiokuwa na hekima fujo:
Akiwazungumzia Viongozi wa Kanisa na Serikali ama Wanasiasa, Askofu Mchamungu alisema,
“Katika Nchi Rais aliyemaliza muda wake anapoondoka anakuja  mwingine yule aliyestaafu hatakiwi kuingilia mambo ya Rais aliyopo madarakani, anapaswa kuendelea na shughuli zake bila kumwingila mwingine, hiyo ndiyo itakuwa hekima,”alisema Askofu Mchamungu.
Askofu Mchamungu alibainisha kuwa hata katika Kanisa, Viongozi wakiwemo Maaskofu na Maparoko wanapomaliza muda wao na kustaafu, wanapaswa kutulia na kuendelea na shughjuli zao bila ya kuwaingilia wengine ambao wapo madarakani, kwani kwao kufanya hivyo, hiyo ndiyo hekima, lakini kinyume chake ni vurugu katika jamii.
“Hata katika Kanisa, Askofu anapomaliza muda wake na kustaafu, kwa mwenye hekima, anapaswa kutulia na kuendelea na shughuli zake huko aliko, bila kumuingilia mwingie ambaye yupo madarakani, endapo atamwingi maana yake atakuwa amekosa hekima, na hiii italeta vurugu, kwani atakuwa anafanya uchochezi kwa kusema wengine vibaya, hata kama mambo husika hayapo,”alisema Askofu Mchamungu na kuongeza,
“Katika Parokia, hata Paroko aliyemaliza muda wake, naye ni hivyo hivyo, anapaswa kukumbatia hekima na kuendelea na kazi zake, bila ya kumuingilia mwingine ambaye anayeendelea na kazi zake katika Parokia,”alisema.
Kwa mujibu wa Askofu Mchamungu, Kiongozi wa namna hiyo asiyeingilia wenzake kwenye majukumu madarakani, ndiye anayoonekana kuwa mwenye hekima...popote pale, lakini endapo atakwenda kinyume, atakuwa mchochezi dhidi ya mwenzake.
“Kiongozi mjinga ni yule mwenye kupita chini chini na kuchochea watu kwa kusema maneno mengi ya uongo dhidi ya viongozi waliopo madarakani... hiyo ni mbaya, kwani hata Mtume Paulo mwenyewe anataka tuache kufanya hivyo, na kutekeleza mapenzi ya Mungu.”
Aidha, Askofu Mchamungu aliwataka Waamini kuhakikisha katika nafasi zao, wanakumbatia hekima ya Mungu, na kuendelea na kazi zao bila ya kuwaingilia wenzao waliopo madarakani na kuwafanyia vurugu za chini kwa chini katika nafasi zao za Uongozi, kwani kufanya hivyo, ni kusababisha vurugu katika uongozi.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.