MWANZA
Na Paul Mabuga
Zawadi ya tuliyopewa na Mungu ya huduma, uhai na maisha ya mpendwa wetu Edward Lowassa, tuliyemhifadhi katika nyumba yake ya milele hivi majuzi huko Monduli, Mkoani Arusha ina mengi ya kutufundisha, lakini zaidi ni kwamba kila binadamu anazaliwa na haki ya kusifiwa, isipokuwa huwa inaporwa na ndiyo maana inahitaji kulindwa na kutetewa.
Kwamba, binadamu hatapata sifa kwenye familia yake au watu wa karibu nae basi ataitafuta nje yao. Wakati mwingine matokeo yanaweza kujenga uhitaji wa kuilinda haki hiyo huku wengine wakiibomoa katika ushindani ambao unajaa vitimbwi. Lakini wakati mwingine, sifa hutolewa bila kufurahisha wengine.
Kuna picha jongefu fupi mtandaoni ambapo mwongeaji hamasa, anayejitambulisha kwa jina la Michael Maundi, anajizungumzia yeye kama mfano ambapo anasema, tangu wakati anasomasoma shule ya msingi nafasi yake kwenye mitihani ilikuwa ya 160 na 180, na hata alipofaulu kwenda kidato cha kwanza shule ye sekondari Kibasila mama yake alimuuliza, “huko darasani kwenu hakuna Michael Maundi Mwingine?” Akimaanisha mama yake alikuwa haamini kama amefaulu.
“Watu wote na hasa watoto wadogo walio nyumbani tunapenda sana sifa, tusipoipata nyumbani ama shuleni tunaitafuta mitaani! Mtaa unasifia, mtaa ukipakata kete [dawa za kulevya], mtaa unakuambua mwanangu umetisha… hata .. uki[anaonyesha ishara ya kuvuta bangi] mtaaa unakuambia mwanangu mwanangu, yaani wewe bonge la Mwambaaa!” anasema akionyesha umuhimu wa kuwasifia watoto kabla ya kupata zile zisizo na maana.
“Mtoto anafanya kitu kikubwa nyumbani wewe hata hushangilii, hustuki,[ inatakiwa] hata kama unakijua unashangaa, heee umejuaji mwanangu! Mtoto anapata moyo wa kutafuta vitu vingine kujua ili kuhadithia, … siyo anakuja kukuelezea kuhusu mto Kirumi uko hivi na hivi, halafu wewe unamvwambia, kwa hiyo wewe ndiyo umejua leo!” anaeleza Maundi katika kadamnasi inayomtazama katika picha hiyo fupi jongefu.
Kinyume chake anasema mwalimu wake wa darasa la saba wakatti anapata hesabu alama saba kwa hamsini kwenye mtihani wa kwanza,alimwambia Maundi una akili sana ili huitumii vuzuri. Wa pili alipopata 11 ya hamsini, akamyanyua juu na kumwambia, wewe ni nomaa, wewe ni mkemia mkuu, na mtihani uliofuata alipata alama zote.
“Mtoto mdogo atakuja kukupa kile [anachokiona] unachokiamini! Ukimuaminisha anaweza [ukimsifia unampa deni kubwa sana, … lakini kimuambua mjinga mpumbavu mende paka .. atakuwa akijisemea hata mama anajua kuwa mimi ni paka!” anasema Maundi na kuongeza kuwa watu wengi duniani wamefanya makubwa kutokana na kulelewa katika miingi hiyp ya motisha ya kusifiwa.
Pia kuna majadiliano katika mtandao wa facebook kupitia uzi mmoja ulioanzishwa na chombo kimoja cha habari nchini Kenya, ambapo inaonekana hoja ni Tanzania angalau kucheza Afcon 2023 iliyomalizika hivi karibuni, ambapo mmoja wa wachangiaji raia wa nchi hiyo ya awali anaandika katika hali ambayo inaonyesha pengine kutofurahia sifa za nchi yake ya jirani.
“Jirani hana dollar, jirani hana umeme, jirani hajui kizungu, jirani hakushinda hata mechi moja Afcon, jirani ana shida kweli kweli,” analeza Ogeto Nyamwange katika mtandani huo. Wapo pia engi waolichangia katika mtazamo huo. Mtanzania Caroline P Mwaipungu anajibu, “Majirani mnajikutaga wazungu etu? Kama wa ulaya vile wakati hatutofautiani shida… eti kuzungu nini?? Mko na umbea mwingi loo!
Ingawa ni utani wa kawaida ambao hata umekuwepo kwa muda sasa kati ya raia wa nchi hizi lakini umekuwa hauna madhara. Zaidi utani huu ni kielelezo cha namna ambavyo binadamu anahitaji sifa, na anapohisi inachukuliwa anaona kuna haja ya kuilinda.
Usishangae binti akiingia gharama ya usafiri kurudi nyumbani kubadili mavazi baada ya kuambiwa aliyoyavaa hayajampendeza. Tunaponunua nguo tunalipia kupendeza siyo mavazi. Hii ni hoja ya kale kina binadamu alivyo.
Tukirejea katika enzi za uhai wake Lowassa licha kusifiwa ambako kwa hakika kulijengwa na kupendwa kutokana na wasifu wake, na hata kuwa kipenzi cha watu, lakinini pia ni ukweli kuwa katika kipindi chake cha kazi na maisha aliukutana na bête noire [tanka bete nwaa], ikiwa na maana ya hali ya kuchukiwa na sehemu fulani ya jamii..
Katika pande zote alizokuwa katika kazi zake, alikuwa kipenzi na kupewa sifa kem kem kwa upande mmoja huku kwa upande mwingine akipata bête noire. Upande mmoja wa binadamu hao hao wakimpa sifa na kumtetea kwa nguvu zote wakati wa pili ukizipopoa sifa hizo ili kumpa bête noire kwa kila gharama yoyote.
Kitu kimoja cha msingi ni kwamba wakati kunyang’anywa kwa haki ya asili ya kusifiwa kunaweza kusababisha athari za kiafya katika maisha ya binadamu, lakini mara nyingi tumekuwa hatujali na hatutoki mbele na kuwanusuru. Watu walioporwa sifa wanazostahili kwa haki tumekuwa tunasubiri wakati wakiaga dunia ili kuwasifia.
Na adui mkubwa wa sifa kwa mwanadamu ni ubinafsi ambao kila mmoja wetu anao. Yaani tunajijali zaidi kwanza sisi, na tunapoona ubinafsi wetu unatishia sifa zetu, tunapambana hata kama katika kufanya hivyo tunawanyang’anya wengine stahiki zao. Siyo lazima kila sifa imfurahishe mwingine, lakini inapaswa kuwa haki ya mmiliki.